Nkomandomondo
Senior Member
- Jun 15, 2015
- 124
- 16
Dr. Slaa na Prof. Lipumba wameshauona mpasuko mkubwa unaokuja. Maalim Seif anataka serikali tatu na EL ni muumini wa mbili ili awe rais wa ukweli i.e. IMPERIAL PRESIDENT... moto utawaka
Ninachoshukuru mie japo kidogo ni kwamba at last Prof ametambua kwamba hawezi kutawaliwa na akili ndogo ya watu kama Mbowe, deals makers japo amechelewa.
Na kwa hili, still he has got a case to answer mbele ya wana Cuf kwa kukiuua chama wakati huo akikipromote Chadema.
Alipaswa ashtuke mapema kujua nini kilichopo nyuma ya hao deals makers wa Chadema. Mbona wenye akili zao Slaa na Mnyika wanayapima maji kwanza kabla ya kuyaingia hata kama wanaishi nyumba ileile!!!
Amechelewa kuchukua maamuzi na kuwajibishwa na wanachama hatoweza kukwepa.
UKAWA ni umoja wa vyama vinavyounga mkono katiba ya Waryoba kwa Lowassa kukubali kugombea urais kupitia UKAWA bila shaka naye atakuwa amekubalina na katiba ya Waryoba hata kama mwanzoni alikuwa ana ikataa.
Hata alipokuwa CCM alikuwa ana fahamu malengo ya UKAWA ni yapi na alipohamia UKAWA alikuwa ana fahamu kuwa lengo moja wapo la UKAWA na ambalo lilikuwa chimbo la UKAWA ni kuunga katiba ya Waryoba.
Kwa vyovyote vile viongozi wa UKAWA akiwepo mwenyekiti wao ambaye ni Lipumba mwenyewe,sharti mojawapo ambalo watakuwa walimpa Lowassa siku alipokubali kuungana nao ni kuikubali katiba ya Waryoba.
Ninaamini hivyo kwa kuwa Lipumba wala kiongozi yeyote wa UKAWA hakuna hata mmoja aliyejitokeza kueleza masharti waliompa Lowassa wakati ana kwenda kujiunga UKAWA.
Na wala sitaki kuamini kuwa Lowassa ndiye aliyekuwa ana toa masharti yake kwa UKAWA ili apate nafasi ya kugombea urais kupitia UKAWA huku viongozi wa UKAWA wakikubaliana na masharti ya Lowassa kwa kuinamisha vichwa na kuinua vichwa kama kondoo wanaokwenda kutolewa kafara.
Wakati Lowassa ana fahamu kuwa kuikubali UKAWA ni kuikubali katiba ya Waryoba na kama Lowassa aliikubali UKAWA pasipo kuikubali katiba ya Waryoba hiyo siyo UKAWA tena na mtu ambaye ana takiwa aweke wazi kama Lowassa aliikubali UKAWA bila katiba ya Waryoba ni Lipumba mwenyewe.
Maadam Lipumba mwenyewe amekaa kimya na hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza kuweka wazi suala hilo ni wazi Lowassa atakuwa alimiza masharti yote ya UKAWA.
Kuiondoa CCM ya Magufuli ambaye siyo mla rushwa, ni mcha Mungu na pia ni mchapa kazi na kumwingiza mla rushwa aliyeshindikana CCM, Lowassa, pamoja na mla rushwa wa BOT ambaye aliikimbia shule Mbowe, ni sawa na kuruka mkojo wa mtoto na kujitumbukiza kwenye choo cha shimo kilichojaa vinyesi vilivyokomaa.
Naona mbwa wa JK (TISS) mpo kazini kejeli kama za msoga. Muda wa kibali poo bado
Yani hata siwaelewi hawa UKAWA,wanafanya nini sasa?,maana najionea mauza uza tuu toka Lowasa aingie UKAWA.
Sababu ni nini?
Mbona yeye na Slaa wanataka tuzingua? Hivi hawa watu wamepewa nini hadi kutugeuka hivi.... walianza vizuri ila wanataka haribu mambo sasa
Habari wakuu,
Baada ya sintofahamu ya jana, leo mwenyekiti wa CUF ameamua kujiuzulu nafasi yake kama mwenyekiti wa chama cha CUF, Prof Lipumba atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa CUF. Ameita waandishi wa habari na kuongea baada ya jana kuzuiwa na wazee.
Sababu ni kutokwenda sawa na wenyekiti wenza wa UKAWA kuhusu kumuunga mkono mtu na kuwapokea watu ambao wamehusika na kutengeneza rasimu ya katiba mpya ambayo yeye hakubuliani nayo na yeye anaunga mkono rasimu ya katiba ya jaji Warioba.
Atashiriki kupigia kampeni wagombea ukiacha Urais na alipoulizwa kuhusu kuhusu kuchukua uamuzi huu sasa kasema dhamira yake inamsuta na walipomuuliza kuhusu pesa kasema hata kumuita mgombea ambae atagombea kupitia UKAWA wanashutumiwa wamepokea pesa hivyo hilo halimsumbui bali dhamira yake na nia ya kuungana kuitetea rasimu iliyopigwa teke na CCM.
Sisi wananchi bado tuna imani na UKAWA.
Hawa waliotoka CCM wanatuongezea kura na mbinu za kuibomoa CCM, hivyo haturudi nyuma hata waseme vipi bado tupo ngangari kinoma hadi kieleweke mwaka huu.
CCM wanaweweseka na UKAWA, ni mwiba unawachoma kila kona ya miili yao.
View attachment 273953
View attachment 273953
View attachment 273952
View attachment 273954
View attachment 273955
ALUTA KONTINUA mpaka RIAMBA.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Dr. Slaa na Prof. Lipumba wameshauona mpasuko mkubwa unaokuja. Maalim Seif anataka serikali tatu na EL ni muumini wa mbili ili awe rais wa ukweli i.e. IMPERIAL PRESIDENT... moto utawaka
sisi tunatafuta mtaji wa kura ili tuitoe ccm madarakani eti yeye Lipumba anasema tunakosea kuwakaribisha waliounga mkono katiba pendekezwa.
Sasa bila kuunganisha nguvu na kuifuta ccm madarakani tutaweza vipi kuipiga chini hiyo katiba pendekezwa??
kwakweli Lipumba ametoa sababu shallow mno.