Prof. Ibrahim Lipumba atangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF Taifa

Dr. Slaa na Prof. Lipumba wameshauona mpasuko mkubwa unaokuja. Maalim Seif anataka serikali tatu na EL ni muumini wa mbili ili awe rais wa ukweli i.e. IMPERIAL PRESIDENT... moto utawaka
 
Ninachoshukuru mie japo kidogo ni kwamba at last Prof ametambua kwamba hawezi kutawaliwa na akili ndogo ya watu kama Mbowe, deals makers japo amechelewa.
Na kwa hili, still he has got a case to answer mbele ya wana Cuf kwa kukiuua chama wakati huo akikipromote Chadema.
Alipaswa ashtuke mapema kujua nini kilichopo nyuma ya hao deals makers wa Chadema. Mbona wenye akili zao Slaa na Mnyika wanayapima maji kwanza kabla ya kuyaingia hata kama wanaishi nyumba ileile!!!
Amechelewa kuchukua maamuzi na kuwajibishwa na wanachama hatoweza kukwepa.


anaweza kuwa amefanya maamuzi sahihi lakini muda siyo sahihi ushiriki mchakato mwanzp mwisho ndo ajitoe kwa nini tusiseme kahongwa .
 
UKAWA ni umoja wa vyama vinavyounga mkono katiba ya Waryoba kwa Lowassa kukubali kugombea urais kupitia UKAWA bila shaka naye atakuwa amekubalina na katiba ya Waryoba hata kama mwanzoni alikuwa ana ikataa.

Hata alipokuwa CCM alikuwa ana fahamu malengo ya UKAWA ni yapi na alipohamia UKAWA alikuwa ana fahamu kuwa lengo moja wapo la UKAWA na ambalo lilikuwa chimbo la UKAWA ni kuunga katiba ya Waryoba.

Kwa vyovyote vile viongozi wa UKAWA akiwepo mwenyekiti wao ambaye ni Lipumba mwenyewe,sharti mojawapo ambalo watakuwa walimpa Lowassa siku alipokubali kuungana nao ni kuikubali katiba ya Waryoba.

Ninaamini hivyo kwa kuwa Lipumba wala kiongozi yeyote wa UKAWA hakuna hata mmoja aliyejitokeza kueleza masharti waliompa Lowassa wakati ana kwenda kujiunga UKAWA.

Na wala sitaki kuamini kuwa Lowassa ndiye aliyekuwa ana toa masharti yake kwa UKAWA ili apate nafasi ya kugombea urais kupitia UKAWA huku viongozi wa UKAWA wakikubaliana na masharti ya Lowassa kwa kuinamisha vichwa na kuinua vichwa kama kondoo wanaokwenda kutolewa kafara.

Wakati Lowassa ana fahamu kuwa kuikubali UKAWA ni kuikubali katiba ya Waryoba na kama Lowassa aliikubali UKAWA pasipo kuikubali katiba ya Waryoba hiyo siyo UKAWA tena na mtu ambaye ana takiwa aweke wazi kama Lowassa aliikubali UKAWA bila katiba ya Waryoba ni Lipumba mwenyewe.

Maadam Lipumba mwenyewe amekaa kimya na hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza kuweka wazi suala hilo ni wazi Lowassa atakuwa alimiza masharti yote ya UKAWA.

Kuiondoa CCM ya Magufuli ambaye siyo mla rushwa, ni mcha Mungu na pia ni mchapa kazi na kumwingiza mla rushwa aliyeshindikana CCM, Lowassa, pamoja na mla rushwa wa BOT ambaye aliikimbia shule Mbowe, ni sawa na kuruka mkojo wa mtoto na kujitumbukiza kwenye choo cha shimo kilichojaa vinyesi vilivyokomaa.



Magufuli ni mcha Mungu!!!!!!
Ndooooooooorooooooooobo wewe!!!!!

Hizo MB zako za kifurushi si bora ungenunua gazeti la udaku ukajipepea.

Mcha Mungu hawezi kuwekwa na wala rushwa na wauaji CCM walioiuza Loliondo na madini yote ya nchi hii.

Mcha Mungu hawezi kushabikia Rafu za kuua Demokrasia zinazofanywa na CCM kwa uwazi.

Mcha Mungu hawezi kuuza nyumba za serikali kwa hawara asiyekua mfanyakazi wa serikali.

Mcha Mungu hawezi kutoa matamko ya roho mbaya kwa wananchia maskini wa kutupwa.
Mcha Mungu hawezi kukaa kumya wakati vituo vingi vya mafuta vya waarabu na marafiki wa kitengo vikiwa vimejengwa barabarani huku nyumba za maskini zikivunjwa.

Mcha Mungu hawezi kutumia mali za serikali kujinadi wakati sio mbunge kwa sasa na bunge lilishavunjwa .
Na sifa ya waziri ni lazima awe mbunge.

Mcha Mungu hawezi kuendelea kung'ang'ania madaraka wakati ametuhumiwa kulitia hasara za mabilioni taifa kupitia wizara alizoongoza.

Mcha Mungu hawezi kuwa na majivuno.


Mcha Mungu atajulikani tarehe 25/10/2010 kwa kukataa goli la mkono ili kuepusha umwagikaji wa damu kwa watanzania . Mcha Mungu ni Yule anayependwa na wacha Mungu wengi.

Wacha Mungu(makapi) ni hawa:

Mizengo Pinda
Mwandosya
Mwakyembe
Asha Rozi Migiro
Jaji Ramadhani
Nyarandu
Sumaye
Samweli Sita
DR. Bilali.
Na Makapi yote yaliyokatwa na kutemwa na kundi la madalali wa nchi hii kwa manufaa ya familia zao.

Wacha Mungu wanatetewa na Mungu mwenyewe.
 
Naona upande wa pili hali inatengemaa taratiibu!
 

Attachments

  • 1438874651926.jpg
    1438874651926.jpg
    20.8 KB · Views: 139
Mbowe kaza buti baba lao tuko nyuma yako kuhasisha mabadiliko maana kamanda una wakati mgumu uliopanda nao meli moja wameshuka njiani kusaka tonge.
 
Sababu alizotaja hazina mashiko nafikiri kuna kitu ameficha. Moja ya kitu ambacho naona hakukubaliana na wenzake ni mgombea mwenza na mgombea urais wa UKAWA.

ALijiaminisha pengine kuwa anaweza kuwa kati ya nafasi mojawapo lakini ujio wa LOwassa ndani ya Chadema na ukawa umebadili upepo.

Bila kuwa mnafiki Lowassa kupewa nafasi ya kugombea urais kupitia UKAWA ni jambo sahihi na la maana na litaleta changamoto kubwa kwa CCM.
 
Naona mbwa wa JK (TISS) mpo kazini kejeli kama za msoga. Muda wa kibali poo bado

Kijana tulia mapeema, hacha kuwa na Presha usije ukatutoka kabla ya kufika Uchaguzi...Hao hao unaowatukana ndio wanaokufanya uwe huru na Amani ndani ya Tanzania...Hao hao ndio wanaokufanya uwe huru na kutuma msgs zako za kejeri hapo ulipo huku ukisubiri kula ugali wako na familia yako kwa Amani, utalala kwa Amani na huku ukisubiri siku ya kesho ambayo itakuwa na Amani...

Tazama kwa majirani zako wanavyoishi na utaziacha kejeri zako na kuheshimu Idara hii na kuzidi kuithamini...

Amka Sasa
 
Professor amefunguka. Kuna kitu sio kizuri nyuma ya ukawa na kama ilivyo ada vijana watahusisha hizi mambo na chama tawala kama ilivyotokea kwa Dr Slaa. I'm still doubting lowassa and his team behind him.
 
Profesa lipumba ni mnafiki tu hata kabla Lowasa hajajiunga na ukawa yeye na padri slaa walileta sintofahamu wakati wa kumchagua atakayepeperusha bendera ya ukawa. Yapite hivi yaende huko hata wangesimamishwa wao uraisi yasingepata.Yamenikera kweli ikiwezekana wahame na nchi kabisa
 
Hapana Daud kuishi na mtu ambaye cku zote mlimsema sana haileti maana,mwizi haachi tabia yake atarudia tu.Heri yao wameondoka mapema je wenginewanaofuata baadae..?
 
Huyu jamaa kujiuzuru katika kipindi hiki si bure... Bwana Lipumba inabidi abadili jina aitwe Lipumbavu.
 
Lipumba kama kweli anakitakia mema CUF akagombee ubunge tutamwelewa
Habari wakuu,
Baada ya sintofahamu ya jana, leo mwenyekiti wa CUF ameamua kujiuzulu nafasi yake kama mwenyekiti wa chama cha CUF, Prof Lipumba atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa CUF. Ameita waandishi wa habari na kuongea baada ya jana kuzuiwa na wazee.

Sababu ni kutokwenda sawa na wenyekiti wenza wa UKAWA kuhusu kumuunga mkono mtu na kuwapokea watu ambao wamehusika na kutengeneza rasimu ya katiba mpya ambayo yeye hakubuliani nayo na yeye anaunga mkono rasimu ya katiba ya jaji Warioba.

Atashiriki kupigia kampeni wagombea ukiacha Urais na alipoulizwa kuhusu kuhusu kuchukua uamuzi huu sasa kasema dhamira yake inamsuta na walipomuuliza kuhusu pesa kasema hata kumuita mgombea ambae atagombea kupitia UKAWA wanashutumiwa wamepokea pesa hivyo hilo halimsumbui bali dhamira yake na nia ya kuungana kuitetea rasimu iliyopigwa teke na CCM.
 
Sisi wananchi bado tuna imani na UKAWA.

Hawa waliotoka CCM wanatuongezea kura na mbinu za kuibomoa CCM, hivyo haturudi nyuma hata waseme vipi bado tupo ngangari kinoma hadi kieleweke mwaka huu.

CCM wanaweweseka na UKAWA, ni mwiba unawachoma kila kona ya miili yao.



ALUTA KONTINUA mpaka RIAMBA.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Mpaka oct tutaona mengi #tukutane octoba.
 
Dr. Slaa na Prof. Lipumba wameshauona mpasuko mkubwa unaokuja. Maalim Seif anataka serikali tatu na EL ni muumini wa mbili ili awe rais wa ukweli i.e. IMPERIAL PRESIDENT... moto utawaka

Hawajatutendea haki sisi wadau,ambao kwanza tunataka CCM izikwe.Hata mpasuko ukitokea mbeleni wakati CCM imeshazikwa sio mbaya tutaanza upya
 
Moto wa safari ya mabadiliko hauwezi kuzimwa na wanasiasa uchwara. Moto ni ule ule.
Lowassa tuko pamoja nawe mpaka mwisho wa safari hii.
 
sisi tunatafuta mtaji wa kura ili tuitoe ccm madarakani eti yeye Lipumba anasema tunakosea kuwakaribisha waliounga mkono katiba pendekezwa.
Sasa bila kuunganisha nguvu na kuifuta ccm madarakani tutaweza vipi kuipiga chini hiyo katiba pendekezwa??

kwakweli Lipumba ametoa sababu shallow mno.

Kumueka lowasa ni sawasawa na ccm b so hakuna ambalo mtakua mmefanya....
 
Back
Top Bottom