Prof. Ibrahim Lipumba atangaza kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CUF Taifa

Professor amefunguka. Kuna kitu sio kizuri nyuma ya ukawa na kama ilivyo ada vijana watahusisha hizi mambo na chama tawala kama ilivyotokea kwa Dr Slaa. I'm still doubting lowassa and his team behind him.
 
Nakumbuka mwaka 2010 wapinzani waligomea kuapishwa kwa raisi,Lipumba aliunga mkono.Napata Shaka anaweza kutumiwa na wapinzani wa UKAWA kudhoofisha mapambano ya mabadiliko.Naamini Lowasa sio msafi na pia viongozi wa UKAWA si safi pia.Lakini kuna wakati wa kuleta mabadiliko tunahitaji kuungana na adui.Kila la Kheri Prof,aluta continua Ukawa hadi tufike

Kuiondoa CCM ya Magufuli ambaye siyo mla rushwa, ni mcha Mungu na pia ni mchapa kazi na kumwingiza mla rushwa aliyeshindikana CCM, Lowassa, pamoja na mla rushwa wa BOT ambaye aliikimbia shule Mbowe, ni sawa na kuruka mkojo wa mtoto na kujitumbukiza kwenye choo cha shimo kilichojaa vinyesi vilivyokomaa.
 
Acha u.p.u.m.b.a.v.u. wewe. Unaanza kukandya utafiri unajua sababu ambayo imemfanya achukue maamuzi haya. Ni ujinga kulaumu wakati hujui kwa nini kaamua hivi. Unajua madudu gani yamefanyika kule au wewe mawazo yako ni kuchukua madaraka tu. Tumia akili uliyo nayo. Inawezekana kabisa amejiuzuru kwa manufaa ya nchi na wananchi wake, who knows. Wewe unajua wafanya biashara wale wana mlengo gani. Usitake tutoe matusi bure hapa.
Niliwahi kuainisha baadhi tu ya sababu ambazo zimemfanya Prof kujiuzuru, tafadhali rejea. Na zipo sababu nyingine nyingi tu ambazo zikiwekwa wazi sasa hivi ukawa itapasuka vipande vipande. Kwa interest ya nchi wewe pita kimya kimya, tena usirudi tena huku

Mkuu, usitishe watu hapa, kila mtu ana uhuru wa kuhoji au kutoa maoni yake na sio lazima yafanane na ya kwako. Lipumba kasema sababu za kujiuzulu kwake au unataka kusema wewe peke yako ndiye ujuaye?.

Huyo Lipumba si ndiye aliyesema kuwa Lowassa sio fisadi na kwamba tatizo ni mfumo? au alivyokuwa anasema hivyo alikuwa ameshikiwa bastola? Huo kama sio unafiki ni kitu gani?

Lipumba si alikiri msikitini kumsaidia Kikwete kuingia Ikulu 2010 kuokoa jahazi? Huo kama sio unafiki ni nini? Unamzuiaje mtu yeyote kusema kwamba kujiuzulu kwa Lipumba ni muendelezo wa upungufu wa akili alio nao.

Ni wazi kama msomi alipaswa kuja na sababu iliyoenda shule na sio kusema kuwa tatizo ni kukaribishwa kwa wanaCCM waliokuwa wanapinga rasimu ya Warioba. WanaCCM wangapi wamekuja CDM miezi mitatu iliyopita mbona hakujiuzulu?

Alitusumbua sana kumpata mgombea wa UKAWA kwa sababu za uchu wa madaraka na kuona yeye ni bora kuliko wengine...ndio maana duniani kote hamna Rais Professor kwa sababu hawashauriki na wanasumbua.

Asituletee za kuleta hapa, aende akafanye utafiti huko..hajui siasa, ndio maana alitaka kugombea mara ya tano pamoja na ukweli kwamba hana influence na hakubaliki na wengi..
 
Aiseee sasa alikuwa anafanya nini pale siku ya kumtangaza Lowasa... hawa watu bana wanatuvunja moyo sisi wapiga kura... mtu umeshindwa 95,2000,2005,2010 bado tu wataka na wewe khaaa

...Nadhani mnaanza kuona jinsi UKAWA/CHADEMA zinavyoanza kumeguka taraaatibu! Sasa na bado subirini mpaka mwisho ndio mtakuja kuona dhamira kamili ya Lowassa kwenye nchi hii na kwenye Siasa za Tanzania. Ombeni Mungu hii Political decision aliyofanya Prof. Ibrahim Lipumba isije ikamfanya Dr kufanya maamuzi makubwa zaidi...

Tatizo mlilonalo wanachama wa CHADEMA/UKAWA ni kwamba mnaamini sana maneno ya Viongozi wenu so wait and see on whats coming next maana haya ni mahesabu tu yaliyofanyika baada ya kujulikana psychological profiles za viongozi wenu...Mjipange na Plan B mapeema sana chama na umoja wenu mlishaua siku mlipo mkaribisha Lowassa na kuuza chama! Upinzani umekufa rasmi Tanzania, na natabiri mapema kabisa kwamba CHADEMA/UKAWA watapoteza majimbo mengi kwenye uchaguzi huu.

Upinzani bado sana Tanzania, Ongereni CCM endeleeni kutawala nchi kwa maana Wapinzani hawapo Serious wanaendekeza njaa na fisadi Lowassa kawaweza ipasavyo kwa mabilioni machache...
 
Swali langu moja tu
Hivi hii nchi anaeonekana fisad ni 1 tu?
Wht abt team escrow wote waliorudishwa na ccm kwny kura za maoni?

Watz tuanze kufikiri upya
 
Kuiondoa CCM ya Magufuli ambaye siyo mla rushwa, ni mcha Mungu na pia ni mchapa kazi na kumwingiza mla rushwa aliyeshindikana CCM, Lowassa, pamoja na mla rushwa wa BOT ambaye aliikimbia shule Mbowe, ni sawa na kuruka mkojo wa mtoto na kujitumbukiza kwenye choo cha shimo kilichojaa vinyesi vilivyokomaa.

Naheshimu maoni yako ila naamini kwakuwa kwake CCM na serikalini hata kama nakuwahi kula rushwa(japo sina uhakika) ila kuna wakati alitumika kama muhuri kupitisha maovu.Kama samaki mmoja akioza wote wameoza.Dr Pombe hawezi kujiita msafi hivyo ile hali alikuwa ni sehemu ya mfumo.
 
Huyo anafanyakazi ESRF na hii taasisi ndio inafanya shughuli nyingi za kisera na mipango ya nchi hii. Amekuwa kwenye conflict of interest miaka mingi bila watu kutambua.
 
Natamani kujua chanzo cha habari hii! lakini hata hivyo kaulimbiu pamoja na kukubaliwa na chama kwamba itumike, kwa kawaida ni pendekezo la mgombea!

Sasa hapo CHADEMA ndio itakuwa inapingana na maelezo yake kwamba tatizo sio lOWASA BALI MFUMO WA CCM KWAMBA NI MBAYA HALAFU TUNABEBA TENA MIFUMO YA CCM KUTOKA KWA lOWASA NA KUILETA CHADEMA WAKATI MBOWE ALISEMA MTAMBADILISHA LOWASA HAPA BADO HAJAWA RAIS ATAKAPOKUWA RAIS SI ATAFANYA KILA KITU ANAVYOJISIKIA?
 
Ninachokijua juu ya Lipumba ni kwamba anekuwa akipata mgao kutoka ccm kwa kudumaza upinzani, sasa wana cuf wameshtuka anaanza kulaumu ukawa. Kuna uhusiano gani kati ya uenyekiti ndani ya cuf na ukawa? Kwani Lowasa ameingia ukawa kupitia cuf?

Hahaaaaa! Aende akalipe deni la magamba, yy alijua ukawa wanatania kumbe watu wako serious na kuing'oa ccm.
 
Leo tarehe 6 Agosti, 2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacock, mjini Dar es Salaam na kutangaza kwamba amejizulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Sisi kama Chama tumezipokea taarifa hizo na tunayaheshimu maamuzi yake. Ni haki yake ya kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona yana maslahi kwake.

Bila shaka, Profesa Ibrahim Lipumba amekifanyia kazi kubwa Chama chetu katika miaka 16 ambayo alikuwa Mwenyekiti wetu, nafasi iliyomfanya awe kiongozi wetu mkuu. Kwa nafasi yake hiyo, pia ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa demokrasia katika nchi yetu. Tunaithamini kazi hiyo na tutaendelea kumheshimu kwa utumishi wake mkubwa kwa Chama chetu na nchi yetu. Tunamtakia kila la kheri katika mipango yake ya baadaye.

Chama Cha Wananchi (CUF) ni taasisi na kinaendeshwa kitaasisi. Ndiyo maana maamuzi yake yote yamekuwa yakifanywa kitaasisi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama. Kwa msingi huo, pamoja na ukweli kwamba kuondoka kwa Profesa Lipumba katika safu ya uongozi kutaacha pengo hasa katika kipindi hichi ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tunawahakikishia wanachama na wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba Chama hichi hakitayumba.

Katika historia yake, CUF imepita katika dhoruba na misukosuko mingi lakini mara zote kimeonesha uwezo mkubwa wa kuhimili dhoruba na misukosuko hiyo na kukabiliana na athari zake. Hatuna chembe ya wasiwasi kwamba hata mtihani huu tutauvuka na tunaamini tutaibuka tukiwa Chama imara zaidi.

Katibu Mkuu ameagiza kuitishwa kwa vikao vya dharura vya Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa siku ya Jumapili, tarehe 9 Agosti, 2015 ili kujadili hatua hiyo na kufanya maamuzi juu ya hatua muafaka zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki hadi hapo Chama kitakapomchagua mwanachama mwengine kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti.

Katika kipindi hiki, Chama kinawataka wanachama na wapenzi wake wote kuwa watulivu na wavumilivu na kusubiri maelekezo ya vikao vya juu vya kitaifa vya Chama.

Mwisho kabisa, tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itaendelea na shughuli zake kama Chama na pia kama mshirika katika UKAWA ambayo CUF ilikuwa ni katika waasisi wake. Tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itatumia nguvu, uwezo, juhudi na maarifa yake yote kuhakikisha kwamba inaulinda UKAWA ambao unaonekana kuwa mwiba kwa CCM. Tunatambua kwamba kuna njama na mbinu kubwa na nyingi zinazofanywa na watawala kutaka kuuvuruga na kuuhujumu UKAWA wakidhani kwamba watapata manusura. Tumesema na tunaendelea kusema CCM mwaka huu hawana manusura. Watanzania wameamua kuwan'goa, na watan'goka Tanzania Bara na Zanzibar kupitia sanduku la kura tarehe 25 Oktoba, 2015. Wimbi hili kubwa la mabadiliko halizuiliki tena.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA
06 AGOSTI, 2015
 
Hivi lipumba ana umaarufu gani maana cuf zanzibar ipo strong bila lipumba na hata wanaoshinda ubunge huku bara ni nguvu zao wenyewe
 
Kuiondoa CCM ya Magufuli ambaye siyo mla rushwa, ni mcha Mungu na pia ni mchapa kazi na kumwingiza mla rushwa aliyeshindikana CCM, Lowassa, pamoja na mla rushwa wa BOT ambaye aliikimbia shule Mbowe, ni sawa na kuruka mkojo wa mtoto na kujitumbukiza kwenye choo cha shimo kilichojaa vinyesi vilivyokomaa.
Unamkubali Lowassa ndani ya moyo hadi ukaamua kuweka avatar ya image yake..lakini kwa nje unajifanya kumponda...teh teh teh
 
Naheshimu maoni yako ila naamini kwakuwa kwake CCM na serikalini hata kama nakuwahi kula rushwa(japo sina uhakika) ila kuna wakati alitumika kama muhuri kupitisha maovu.Kama samaki mmoja akioza wote wameoza.Dr Pombe hawezi kujiita msafi hivyo ile hali alikuwa ni sehemu ya mfumo.
Huyo mtu kauza nyumba za serikali kibao...

CAG alisema Tsh. Billioni 246 hazionekani katika bajeti ya wizara yake, unafikiri hiyo hela imepotea au imepotezwa?

Kapunguza upana wa barabara zilizojengwa akiwa kama waziri mwenye dhamana, na fedha zilizopatikana ziliingia kwenye mifuko ya watu...

Wadau watakwambia zingine kibao...
 
Yani hata siwaelewi hawa UKAWA,wanafanya nini sasa?,maana najionea mauza uza tuu toka Lowasa aingie UKAWA.
 
Back
Top Bottom