Prof. Anna Tibaijuka atangaza kutogombea tena Ubunge, asema hakuna wa kumshinda zaidi ya Mungu

Wahaya wameanza utani na Mungu.
Wamejisahu kuwa kila kitu ni wao ee, tetemeko la ardhi wao,naniino waliambiwa wao,ile ingine nayo waliambiwa ni wao, njaa wazee wa watu nayo wao, sasa huyu mama anataka washushiwe tena lingine tena,waambie na...........hata hilo lao. Mkumbukeni majibu ya jamaa kwenye ule mkutano ule kuwa Tanzania...................
 
Aende tu mama wa mamilioni ya mboga

Ukipanua.....wanatamani.....unavyozidi kupanua wanazidi kutamani
unasemaje wewe?
IMG_20190703_095015.jpg
 
Hayo maneno ya sijui hakuna nini wala nini.. labda kashauriwa na naninii wake atoke tu kwasababu atashindwa kwa kishindo kwamba.. hata za maoni anajua hatapita. Bora angesema maneno ya kupumzika hayo ya kuachia vijana bila mbwembwe..
Sorry!unamjua Tibaijuka?!unapajua muleba?!!! Nimeuliza tu.
 
Si ajabu hata hiyo 2020 asifike hivi hizi ndimi zetu tumeshindwa kabisa kuzidhibiti ?
 
Bora ametoka.

Ila walau amefanya kitu kwenye hiyo wilaya ya muleba hasa upanuzi wa Barabara ya muleba mjini, pamoja na ujenzi wa Barabara ya rubya.soko la ndizi, nk
Sio wengine wakina ndugai hawafanyi lolote kule Dodoma.
 
Ata kwenye Elimu mama Anna amejitahidi sana
 
Ata kwenye Elimu mama Anna amejitahidi sana
Yap amejitahidi kupakumbuka kwao.

Nadhani ndo mwenye ghorofa refu kuliko yote Bukoba mjini pale mlimani .

Shule yake Alexander kajumulo na Ile ya muleba.
Hata nyumba yake kijijini sio haba.

Ana haki ya kujisifia Kwa kweli.
 
Sorry!unamjua Tibaijuka?!unapajua muleba?!!! Nimeuliza tu.

Eleza unalotaka kueleza ili unibadili niliyoandika.. ungekuwa na la maana la kuandika husimgeniuliza maswali ya huko mkoani kwenu.. sijui kijijini kwenu.. watu wa kabila hilo maringo yamewajaaa tu.. angetemwa.. anaondoka kwa kuwa hajapeea kazi.. mama wa mgawo wa zile pesa.. fis...
 
Mwigulu is young, usiongee kiujumla. Labda changamoto zingine tu jimboni kwake zimtoe
HONGERA SANA KWA MAMA YETU PROFESA ANNA TIBAIJUKA KWA KUTANGAZA KUSTAAFU UBUNGE BAADA YA KUONA UMRI UMESOGEA

HIVYO BASI WATU KAMA AKINA MWIGULU NCHEMBA, NDUGAI, MWAKIEMBE MJIUZULU KUGOMBEA UBUNGE MAANA UMRI WENU UMEENDAA MTUACHIE VIJANA
 
Mwanasiasa Mkongwe na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka ametangaza kutogombea tena Ubunge wa Jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020

Akitangaza nia hiyo Prof. Tibaijuka amesema "2020 nang’atuka Ubunge, sisi ni kizazi cha Mwalimu, sistaafu kwamba kuna Mtu wa kunishinda, wa kunishinda mimi labda Mungu”

Hii ni mara ya pili kwa Prof. Anna Tibaijuka kutangaza nia hiyo, aliwahi kueleza nia yake ya kung'atuka katika siasa mwaka 2017

Alisema kuwa ataendelea kuwepo kwenye jamii lakini ni wakati wa kuwapa nafasi vijana na maarifa yao yataendelea kutumika kwenye ushauri katika kusonga mbele
" Labda" Mungu ndio anaweza kumshinda?!!......Hii ni kufuru!
 
Wamejisahu kuwa kila kitu ni wao ee, tetemeko la ardhi wao,naniino waliambiwa wao,ile ingine nayo waliambiwa ni wao, njaa wazee wa watu nayo wao, sasa huyu mama anataka washushiwe tena lingine tena,waambie na...........hata hilo lao. Mkumbukeni majibu ya jamaa kwenye ule mkutano ule kuwa Tanzania...................
We utakuwa unapungukiwa akili au hazimo kabisa, ni lini wahaya walilia njaa??
 
Bora ametoka.

Ila walau amefanya kitu kwenye hiyo wilaya ya muleba hasa upanuzi wa Barabara ya muleba mjini, pamoja na ujenzi wa Barabara ya rubya.soko la ndizi, nk
Sio wengine wakina ndugai hawafanyi lolote kule Dodoma.
Mkuu ndugai ana loji kule, kilimo kwa mfano na vituo kadhaa vya mafuta ya taa. Umeme wa rea pia umepita kule kijijini. Oo kuna shamba la miti pia.
 
Back
Top Bottom