Procedures za kushitaki/kufungua kesi

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Hallow wandugu,
Mimi ni miongoni mwa wale ambao ni mbumbumbu ya sheria, je nikitaka kumshitaki mtu/kikundi/kampunu nk natakiwa nifanyeje, is it just a matter of going mahakamani na kutoa maelezo kwa ninaekusudia kumshtaki or what, naomba msaada wenu
 
unataka kushitaki wamekufanyia nini, je ni kesi ya madai au ni keshi ya jinai? yaani, wamekutendea kosa la jinai? au una madai nao ya aina fulani hivi sasa unataka mahakama iamue wakulipe?...

kama ni madai unawadai kitu, hiyo ni kesi utakayoianzisha wewe mwenyewe. lakini kama ni kosa la jinai wamekutendea, sio wewe utakayewapeleka mahakamani, ila Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Republic) ambao wana dhamana ya kukulinda wewe kama raia wake, watakushitakia hao watu badala yako. ila unachotakiwa kufanya ni kupeleka hilo jambo polisi, polisi watawakamata hao watu na kuwafungulia shitaka la jinai, mahakamani atakayeendesha shitaka hilo ni Public prosecutor (PP) au state attorney (kulingana na eneo ulipo kwani state attorneys hawajaenea tz nzima, sehemu zingine polisi baadhi wanaact kama public prosecutors, baadaye mashitaka yote yataendeshwa na mawakili wa selikali tu).
 
unataka kushitaki wamekufanyia nini, je ni kesi ya madai au ni keshi ya jinai? yaani, wamekutendea kosa la jinai? au una madai nao ya aina fulani hivi sasa unataka mahakama iamue wakulipe?...<br />
<br />
kama ni madai unawadai kitu, hiyo ni kesi utakayoianzisha wewe mwenyewe. lakini kama ni kosa la jinai wamekutendea, sio wewe utakayewapeleka mahakamani, ila Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Republic) ambao wana dhamana ya kukulinda wewe kama raia wake, watakushitakia hao watu badala yako. ila unachotakiwa kufanya ni kupeleka hilo jambo polisi, polisi watawakamata hao watu na kuwafungulia shitaka la jinai, mahakamani atakayeendesha shitaka hilo ni Public prosecutor (PP) au state attorney (kulingana na eneo ulipo kwani state attorneys hawajaenea tz nzima, sehemu zingine polisi baadhi wanaact kama public prosecutors, baadaye mashitaka yote yataendeshwa na mawakili wa selikali tu).
<br />
<br />
Safi sana mkuu kwa kuelezea vizuri upande makosa ya jinai vipi upande wa madai usisaha na limitation of time,
 
Wadau, nimekutana na uzi huu nikiwa natafuta namna ya kufungua kesi ya madai ambapo nimekuta muulizaji hakuweza kupewa majibu ambayo naamini yangeweza kuwa msaada kwangu na kwa wengineo. Please kwa mwenye ufafanuzi atusaidie hapa. Nahitaji kumshitaki mtu niliyeingia naye mkataba wa pikipiki na kudai kuwa iliibiwa.
 
Kosa la wizi ni jinai ndugu
 
Nataka kufungua madai, nahitaji nilipwe hela yangu iliyobaki maana mkataba ulikuwa haujaisha. Ilibaki miezi mitatu kumaliza.
 
Andaa madai yako na uyapeleke mahakamani, KWA hela hiyo haihitaji wakili, we nenda MAHAKAMA ya mwanzo iliyo karibu nawe, utawaeleza watakufungulia
 
Back
Top Bottom