Prison Break Season 6 Is Back!!!

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Baada ya 24 Legacy kuwa cancelled, wadau wakawa wanaitupia macho PB ambayo tangu kutoka kwa Season 5, hapakuwa na taarifa yoyote ikiwa pangekuwa na Season 6 au ingekuwa cancelled. Kwa muda mrefu, hapakuwa na kauli yoyote official... in fact, hadi sasa hakuna official statement ya kuwa itaendelea au cancelled.

Dana Walden, boss wa FOX aliwahi kunukuliwa akisema hata kama PB itarudi still haiwezi kuwa mwaka huu wala mwakani, huku akisisitiza wanataka iwe special na sio ya kutoa kila msimu!

Hata hivyo, waigizaji wenyewe wanaonekana bado wanaitamani. Michael Scofield kwa mfano, mwishoni mwa October ali-share idea for PB Season 6 ambayo aliiwakisilisha kwa creators wa PB. Hata hivyo, inaonekana creators hawakuwa interested na idea yake, at least kwa wakati huo!!

Idea ya Michael Scofield for Season 6 ni hii hapa:

PB01.png


Kwamba, 23 years Tag ambae pia ni genius tech billionaire, ni Super Fan wa Michael na Lincoln. Hakuna anachopenda kuona toka kwa ndugu hao wawili kama uwezo wao wa kutoroka kwenye magereza mbalimbali kuanzia Fox River (Season 1), Sona (Season 3) hadi Ogygia (Season 5).

Ili kufanikisha shauku yake hiyo, Tag anawateka Michael na Lincoln na kuwatupa kwenye jela ya vijana inayofahamika kama LOCKWITH HOME FOR BOYS. "Jela" hii ni abandoned facility ambayo kwa hivi sasa inamilikiwa na Tag mwenyewe huku akilenga kuitumia kwa lengo moja tu... kuwaona Michael na Lincoln wakifanya yale ya Season 1-5.

Na kwavile pesa kwake si tatizo, kijana mtukutu, au sociopath kama alivyoitwa na Michael, amefanikiwa kuligeuza eneo zima lenye ekari 1000 liendane na mandhari kama yale yaliyopata kutokea Season 1-5! Which means, ndani ya hizo ekari 1000, kuna Fox River, Sona na Ogygia.

Hiyo ilikuwa ndio idea ya Michael Scofield ambayo aliwasilisha kwa ajili ya season 6 lakini jamaa wakaipiga chini!!!

Lakini wakati bado hakuna taarifa rasmi, Lincoln ame-post kuashiri kwamba Seaon 6 inakuja!! Kisichofahamika ni kwamba watakuja kwa staili ipi hasa ukizingatia Season 5 iliishia Michael akiwa anapata full immunity na kurudi kwa familia.

PB02.png
 

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,630
2,000
Hivi script za hizi series/tamthilia zinaandikwa kama zile tamthilia zetu kama Hawala ya Fedha au?
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Hivi script za hizi series/tamthilia zinaandikwa kama zile tamthilia zetu kama Hawala ya Fedha au?
Hazifanani hata kidogo! Script za series zinafanana na za movie kwa 99.9 lakini, kwa format zipo tofauti kabisa na akina Hawala ya Fedha. Zaidi ya kuandika IGIZO LA KWANZA, IGIZO LA PILI.... sioni kingine kinachofanana linapokuja suala la format.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Sababu zipi zilipelekea 24hrs Legacy to be Cancelled..?
Fox hawakutoa sababu lakini viewership haikuwa mzuri... na suala la viewership linatumika sana ku-cancel au ku-renew show.

Hata hivyo, uzuri ni kwamba "franchise" ya 24 kama 24 bado haijawa cancelled na kwahiyo uwezekano wa kurudi upo!!! Taarifa ambayo waliitoa ni kwamba 24 Creators walikuwa wanaangalia namna ya kujazia nyama idea mzima ya 24 na baada ya hapo wanaweza kurudi tena na timu mpya!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom