Prison Break kurejea kivingine

dog 1

JF-Expert Member
Nov 20, 2015
228
575
Prison Break kurudi bila Michael Scofield na Lincoln Burrows.

Kulingana na Radio Times, sio Dominic Purcell wala Wentworth Miller wanaotarajiwa kurejea.

Mfululizo huu unaripotiwa kuandikwa na kutayarishwa na Elgin James wa Mayans MC, huku mtayarishaji wa Prison Break Paul Scheuring akifanya kama mtayarishaji mkuu.

Ikumbukwe kuwa The Original Prison Break iliigizwa na Wentworth Miller kama Michael Scofield na Dominic Purcell kama kaka Michael Scofield na Lincoln Burrows, ambao walipanga mpango wa kumtoa Burrows gerezani baada ya kushtakiwa kimakosa kwa uhalifu uliomfanya ahukumiwe kunyongwa. Kipindi hicho kiliendeshwa kwa misimu minne kati ya 2005 na 2009, baadaye kikarudi kwa sinema ya TV ya 2009 Prison Break

Ingawa bado ipo katika maandalizi ya mwanzo, wakati wa kuzinduliowa bado haujawekwa wazi wakielezwa kutafuta namna ya kuifanya wakitafuta waigizaji wengine watakaovaa uhusika wa Michael Scofield na Lincoln Burrows.

Kufikia sasa, maelezo yoyote kuhusu yaliyomo kwenye onyesho jipya la Prison Break hayajatolewa na wenngi wanajiuliza kama itaendana na ile ya mwanzo au laah, Hata hivyo, inaonekana kuwa wanajaribu kutafuta muunganiko wa waigizaji wapya huku wakiepuka makosa ya kipindi kifupi cha Prison Break msimu wa 5 maana pia wakati wa nyuma ni tofauti na wakati wa sasa, lakini pia wengi wanaamini Bila Michael na Lincoln onyesho hilo litaonekana la tofauti na hunenda lisivutie watu wengi, ingawa pia bado linaweza kufanyika bila wao.

Unatamani Prison Break irudi bila Michael Scofield, Lincoln Burrows, Sarah Wayne, T-Bag na wengine?? na Je nani alikuwa anakuvutia zaidi?

Chanzo: Bongo5
 
Kwani hao waandaji watapungukiwa nini wakija na tamthiliya nyingine? Kwani ni lazima iwe Prison break? Halafu Prison break isiyo na main character (Michael Scolfield), si itakuwa ni ya hovyo kupitiliza!!

Maana yake haitakuwa na tofauti na ile tamthiliya ya Kikorea ya IRIS kwenye toleo lake la pili! Ilipoteza mvuto, na ilikuwa haieleweki! Baada ya sterling kuigiza kuuwawa kwenye toleo la kwanza.
 
Mi asipokuwepo yule jamaa anaempenda sana demu wake ntaona imekua sio tena PB Bali ni Tamthilia ya KOMBOLELA
 
images.jpeg.jpg
 
Prison break ndio season ya miaka hiyo lakini matukio yake mpaka leo yana exist in real life.. jaribu kuangali matukio ya siri kikundi au watu kwenye mwanvuli wa serikali....

Unajua movie mbali namaigizo huwa inafundisha mambo mengi ambayo in real life unaweza apply mifumo hiyo, na ikafanya kazi

Kuna scene moja niliangalia jamaa walipotea ikafika mahali hawajui waendako, sasa katika kujua waende wapi ghafla walipita ndege weupe angani, hii ikawa ni ishara kwao hapo walipo au wakiwafata hao ndege kuna fukwe karibu yao. Kuna aina ya ndege ambayo huwezi kuwaona maeneno yeyote ambayo wasiyo na fukwe...
 
Back
Top Bottom