Peaky blinders Season 6 uhusika halisi wa Tommy utakuwa ni ovu/mbaya zaidi.

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,549
188,736
Peaky blinders season 6 ni gangster TV show ambayo itakuwa ndio mwisho wa series hiyo na kama ilivyoonekana uhusika wa Tommy toka mwanzoni wa series alikuwa mtu aliyefanya maovu/uhalifu kwa lengo la kufanikiwa kabisa mambo yake hususani familia yao ya Shelby.

Kwa kuwa Peaky blinders season 6 itakuwa ndio mwisho wa show hii ya kiharifu na kutakuwa na mabadiliko/kugeuzwa kwa uhusika wa Tommy Shelby kwenye season hii ya mwisho na hapo ndipo waandaaji wa husika wa waigizaji unaenda kuonyesha makosa juu ya mabadiliko hayo kwa wapenzi wa series hiyo.

Toka mwanzo kabisa wa Peaky blinders inatoka mwaka 2013, ilianza kupendwa na kuwa na wafatiliaji wengi duniani na kupata mashabiki na tuzo nyingi, Ila mafanikio hayo ya Peaky blinders yalimpa picha ya Tommy Shelby na uhusika wake ni ndio utambulisho wake wa pekee kabisa kwenye season hiyo.

Season zilizopita Tommy Shelby alikuwa na matukio mengi na safari ya uhusika wake ndipo kusababisha kupendwa na watu wengi.

Mwanzoni kabisa series inaeleza namna alivyotoka kwenye Vita Vya Kwanza Vya Dunia na kufanikiwa kuwabadilisha wanajeshi wenzie kuanza shughuli za uhalifu huku kukiambatana na matukio mengi ya visasi, vurugu, kukwepa polisi, wanasiasa na hata yeye mwenyewe kupambana na hali yake mwenyewe kwenye mind maana ikumbukwe hakurudi kama alivyokuwa ameenda huko vitani.

Peaky Blinders season 6 itajaribu kumpa uhusika zaidi huku season yenyewe ikielekea mwisho kabisa. Episode ya mwisho ya season 5 ilimuonyesha namna alivyoshindwa kwenye mission yake na wakati huo huo alikuwa bado ana hali ngumu baada ya kumpoteza mkewe Grace, Na kumalizika huku akiwa amejiwekea bunduki kichwani huku akipiga kelele.

Mafanikio hayo ya Tommy kwenye uhusika wake pamoja na mabadiliko yote yaliyotokea kwa miaka kadhaa, yanamuweka katika mazingira magumu kwenye season 6.

Kwa ujumla Peaky blinders season 6 itamfanya awe na mabadiliko zaidi kwenye uhusika wake.



Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
View attachment 2131835
 
Ukitaka kuielewa nenda kaisome story yao kwanza, ile series inaongelea mambo ya kweli
Mzunguko wote huo wa nini. Henu nipe majina ya series kali za mwaka huu. Ujasusi mkono upelelezi uhalifu vyote kwa pamoja
Au hata za kuanzia mwaka jana za namna niliyoitaja hapo juu
 
Who Wants To Be In Heaven When You Can Be Sending Men To Fucking Hell?" - Arthur Shelby

Moja ya series Bora kabisa
 
Back
Top Bottom