Princes Muro iliyokua inaondoka Dar kwenda Musoma yenye Reg No T536 CYC tarehe 13 June 2017 imetufanyia uhuni ilipofika shinyanga mnamo saa tano usiku na kuamuru abiria kuhamishiwa Mohamed Trans kwa kisingizio inarudi kufaulisha abiria wa Dar Kwenda Bukoba kitu ambacho si kweli. Hii imekua tabia ya mabasi haya ya Princes Muro kufanya ushenzi huu. Tunaomba SUMATRA na vyombo vya usalama kufuatilia hili suala. Abiria tumegoma na tunataka haki itendeke.