Basi la Princes Muro latekwa, abiria wavuliwa nguo, waporwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,077
2,000

Na Abdallah Amiri, Igunga

BASI la Kampuni ya Princes Muro, lenye namba za usajili T 551 BQP, ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Kahama, mkoani Shinyanga, limetekwa na majambazi usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Igogo, Wilaya Igunga, mkoani Tabora.

Akizungumza na gazeti hili, abiria wa badi hilo ambaye alijeruhiwa na majambazi hao kichwani, Bw. Brayandi Sangatwa (67), alisema wakiwa njiani kabla ya kufika Kijiji cha Igogo, basi hilo liliharibika ambapo mafundi walianza kulitengeneza hadi saa saba usiku.

“Baada ya matengenezo kukamilika, tulianza safari na baada ya kufika kijijini hapo, tulikuta mawe makubwa yakiwa yamepangwa katikati ya barabara na kuanza kushambuliwa kwa mawe.

“Hawa majambazi walikuwa na fimbo, mapanga pamoja na mawe, abiria wote tuliamuriwa kushuka mmoja mmoja, kuvua nguo zote
na kulala kifudifudi, majambazi walichukua fedha zetu na simu
za mkononi,” alisema Bw. Sangatwa.

Aliongeza kuwa, yeye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya
miguu hivyo aliwaomba majambazi hao ashuke pole pole
kutoka ndani ya basi hilo.

Alisema jamabazi hao hawakukubaliana na ombi hilo hivyo waliamua kumvuta kwa nguvu, kumtoa ndani ya basi na kumwamuru atoe fedha zote.

“Niliwajibu sina fedha zozote wakaamua kunipiga fimbo kichwani, kuchukua sh. 80,000 na kuniachia simu ya mkononi ambayo nilikuwa nimeilalia katika mkono wa kushoto,” alisema.

Alidai baada ya majambazi hao kufanya unyama huo, walitokomea kusikojulikana wakiwa na simu pamoja na fedha walizopora kwa abiria na kuwaacvhia nuo zao.

Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Wilaya ya Igunga, Godfrey Kisila, alisema walipokea majeruhi watano saa 10 usiku ambao walikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.

Alisema kati ya majeruhi hao, wanne walitibiwa na kupewa ruhusa, lakini Bw. Sangatwa, bado anaendelea kupatiwa matibabu na amelazwa katika wodi namba nane hospitalini hapo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu, alithibitisha kutekwa kwa basi hilo na kudai kuwa, kiwango cha fedha na simu zilizoibiwa na majambazi hao bado hakijajulikana na juhudi za kuwasaka wahusika waliofanya kitendo hicho zinaendelea.

Aliwaomba wananchi kutoa ushirtikiano kwa Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. Basi
hilo lilikuwa linaendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina
la Bw. Makiselu Madi.

Aliliagiza jeshi hilo wilayani humo kuhakikisha mabasi yote hayatembei usiku ambapo dereva yoyote ambaye atakiuka
agizo hilo akamatwe na kuchukuliwa hatua.
 

pembe

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,091
2,000
Poleni wananchi. Usiku mabasi yawe na polisi wa kuwasindikiza.
 

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,563
2,000
Rafiki yangu ni muhanga wa utekaji huo. Kosa kubwa lipo kwa abiria.. Wahusika wa gari walitaka kulala pale Igunga ila abiria wengi wakagoma. Wakalazimisha kwenda tu..Alikuwepo abiria mmojawapo ambaye inasemekana alihusika kuchonga utekaji huo. Jamaa huyo ndio aliongoza kusisitiza dereva aendelee na safari.
 

alexmahone

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
483
250
Bora wamewaachia uhai wenu.,hyo michina waliochukua haitawafika mbali..Mbaya vile wamewadhalilisha kuwavua nguo ila nafuu pia kwakuwa hawakuwapa mtihani wa kuchagua kuolewa au kufa.,maana tungekuwa tunaongea mambo mengine hapa.
Mzee Sangatwa unavyoonekana ulikuwa m-bishi kidogo bila shaka ungechagua kifo.,ila nikukumbushe usiwe unawaomba majambazi wakuonee huruma,usitarajie watakuelewa katika matatizo yako kwakuwa wanayoyawaza kichwani mwao ni kuua kama watakutana na kizuizi mawazo hayo huwapa hasira kwa mtu yoyote anayejaribu kuwaongelesha kwa muda mrefu maana wanamuoa kuwa anawachelewesha.
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
Bora wamewaachia uhai wenu.,hyo michina waliochukua haitawafika mbali..Mbaya vile wamewadhalilisha kuwavua nguo ila nafuu pia kwakuwa hawakuwapa mtihani wa kuchagua kuolewa au kufa.,maana tungekuwa tunaongea mambo mengine hapa.
Mzee Sangatwa unavyoonekana ulikuwa m-bishi kidogo bila shaka ungechagua kifo.,ila nikukumbushe usiwe unawaomba majambazi wakuonee huruma,usitarajie watakuelewa katika matatizo yako kwakuwa wanayoyawaza kichwani mwao ni kuua kama watakutana na kizuizi mawazo hayo huwapa hasira kwa mtu yoyote anayejaribu kuwaongelesha kwa muda mrefu maana wanamuoa kuwa anawachelewesha.

mzee sangatwa amekupata,yupo wodini hapa anaperuz JF,anacheeeeeeeka
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
'Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyeeeeewe,,talalaaa,mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyeeeeewe.
Hao wenye pea hawakuzaliwa naaaazoooooooo,hao wenye magazri hawakuzaliwa naaaaayooooooo.
TUJITUMEEEEEEE,KUFANYA KAZIIIIII,KWANI KAZIIIII NDO MSINGI WA MAISHA YAKOX2'
BANZA STONE NA TOT achimenengule
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,135
2,000
Umenikumbusha lile tukio la wale majambazi waliowaimbisha wimbo wa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.
 

COURTESY

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
2,008
1,225
Ndio maana mi huwa nasafiri na gun yangu,siku wakijaribu wataisoma namba,huwa nikilenga sikosi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom