Prime ministers Sumaye miaka 12 vs Lowassa miaka 2 nani mzoefu?

Prime ministers Sumaye miaka 12 vs Lowassa miaka 2 nani mzoefu?

wananchi msiumize vichwa vyenu... Binafsi naweza kusema sumaye anazosifa za kushika nafasi kuu. Akiwa w/mkuu miaka miwili ya mwisho ya mzee rukhsa na baadae kuendelea na mzee mkapa tumeweza kuona juhudi zake na mapungufu yake kiasi lkn amethubutu chini ya uongozi wa mkapa kuifanya nchi kuheshimika kwa wananchi na nje ya nchi kwa kudhibiti mifumuko ya bei ambayo mpaka leo hii ambacho siwezi kusahau ni nauli ya daladala aliipokea kutoka kwa mzee mwinyi ikiwa ni sh 150/= na tukamaliza nayo katika utawala wake mpaka alipo mkabidhi kanali jakaya ambaye binafsi nasema ameliyumbisha taifa kupitia kwa msaidizi wake mr lowassa aka msanii nimuite hivyo.
Kinacho shangaza mr lowassa amekuwa na juhudi nyingi za kujifanya anauchungu wa nchi hii wakati si kweli.
Nisiseme mengi juu ya huyu mr lowassa kwani anajulikana ndani ya miaka mi2 tu ameharibu na kufikia kutimuliwa hii ni kutokana na kukosa uadilifu katika madaraka aliyokabidhiwa.
Hivyo basi nahitimisha kusema kwamba wananchi tusihadaike na mh. Huyu msanii maana hana jipya.
Kama tunataka kweli maendeleo basi bw. Sumaye anaweza kutokana na historia yake na pia la muhimu zaidi ni yuko fiti kiafya na anajiamini hana kashfa, na mtu wa watu maana nilishawahi kukutana nae duka moja mitaa ya samora sikuweza kuamini waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu kupita wote walio pita awe hana ulinzi wa kutisha kama anavofanya bwana msanii maana nae nilikutana nae mitaa yake ya obay akiwa na jopo la ulinzi nilishangaa mbona sumaye waziri mstaafu hana ulinzi kama huu?? Wakati huyu msanii kakaa miaka 2 tu mjengoni na kutimuliwa alafu ulinzi mkubwa loh??? Haya ni majanga
kiukweli kama wananchi tunataka maendeleo ya nchi hii basi nafasi iwe wazi kwa bw sumaye maana rekodi yake inajulikana. Tusifate ushabiki na njaa ya vijipesa mnavyohongwa makanisani na misikitini na sasa hivi kaingia mashuleni ili awakamate wazazi.
Kazi kwenu wananchi.

1. Mkuu kimsingi na kubaliana nawe kwa sehemu kwani Kashfa nyingi za Sumaye zilikuwa za kutungwa na ndo maan aliporudi kutoka masomoni Harvard alivitahadharisha vyombo vilivyokuwa vikimchafua kwamba kwa sasa vikiendelea viwe tayari kuakabiliana na mkondo wa Sheria kwani awali aliwavumilia kwakuwa alikuwa Kiongozi lakini kwa sasa hata sita kusafisha jina lake kisheria...na Kuthibitisha kwamba vyombo vile vilikuwa vikitoa habari za uzushi baada ya mkwara huo vilinyamaza.
2. Sehemu ya Pili kuhusu kufaa kwa Sumaye kugombea Urais sina Pingamizi iwapo ataomba kupitia vyama vya "watanzania" Hapa na maanisha vyama vinavyoongea lugha ya watanzania lakini iwapo ni kupitia CCM ni BIG NO CCM imeharibika beyond repair Kaka.
 
Halafu ndani ya hiyo miaka 2 tu madudu yaliyofanyika usipime ! Pangisha jengo la wananchi ( kwa uongo linaitwa la umoja wa vijana ), fukuza watendaji wa halmashauri bila utaratibu , richmond , inasemekana hii ndiyo kashfa kubwa kabisa kuwahi kumtokea waziri mkuu yoyote barani africa kabla na baada ya uhuru ! Halafu bado kuna midubwasha inampigia debe !
 
Pamoja na kutumia nguvu zote kumridhisha aliyekutuma,mwambie sumaye anakumbuka shuka kumekucha? Yeye ndio aliyesimamia uuzaji wa nyumba za serikali,mwananchi,meremeta,kagoda nk anakumbuka?
 
Frederick Tluway Sumaye (amezaliwa 29 Mei 1950) alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 27 Novemba 1995 mpaka 28 Desemba 2005.

Mr.Zero hakuna atakayempa urais.Nakumbuka baada ya kumaliza miaka 5 ya mkapa wananchi walitamka waziwazi Sumaye asipewe tena u PM,Mkapa akajitetea kuwa sii busara kuwa na milolongo ya mawaziri wakuu wastaafu itakua ni kuongeza gharama kubwa tumwache tuu amalize kipindi chake!!!!in short hafai kabisa
 
Halafu ndani ya hiyo miaka 2 tu madudu yaliyofanyika usipime ! Pangisha jengo la wananchi ( kwa uongo linaitwa la umoja wa vijana ), fukuza watendaji wa halmashauri bila utaratibu , richmond , inasemekana ndiyo kashfa kubwa kabisa kuwahi kumtokea waziri mkuu yoyote barani africa kabla na baada ya uhuru ! Halafu cdo kuna midubwasha inampigia debe !
 
wananchi msiumize vichwa vyenu... Binafsi naweza kusema sumaye anazosifa za kushika nafasi kuu. Akiwa w/mkuu miaka miwili ya mwisho ya mzee rukhsa na baadae kuendelea na mzee mkapa tumeweza kuona juhudi zake na mapungufu yake kiasi lkn amethubutu chini ya uongozi wa mkapa kuifanya nchi kuheshimika kwa wananchi na nje ya nchi kwa kudhibiti mifumuko ya bei ambayo mpaka leo hii ambacho siwezi kusahau ni nauli ya daladala aliipokea kutoka kwa mzee mwinyi ikiwa ni sh 150/= na tukamaliza nayo katika utawala wake mpaka alipo mkabidhi kanali jakaya ambaye binafsi nasema ameliyumbisha taifa kupitia kwa msaidizi wake mr lowassa aka msanii nimuite hivyo.
Kinacho shangaza mr lowassa amekuwa na juhudi nyingi za kujifanya anauchungu wa nchi hii wakati si kweli.
Nisiseme mengi juu ya huyu mr lowassa kwani anajulikana ndani ya miaka mi2 tu ameharibu na kufikia kutimuliwa hii ni kutokana na kukosa uadilifu katika madaraka aliyokabidhiwa.
Hivyo basi nahitimisha kusema kwamba wananchi tusihadaike na mh. Huyu msanii maana hana jipya.
Kama tunataka kweli maendeleo basi bw. Sumaye anaweza kutokana na historia yake na pia la muhimu zaidi ni yuko fiti kiafya na anajiamini hana kashfa, na mtu wa watu maana nilishawahi kukutana nae duka moja mitaa ya samora sikuweza kuamini waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu kupita wote walio pita awe hana ulinzi wa kutisha kama anavofanya bwana msanii maana nae nilikutana nae mitaa yake ya obay akiwa na jopo la ulinzi nilishangaa mbona sumaye waziri mstaafu hana ulinzi kama huu?? Wakati huyu msanii kakaa miaka 2 tu mjengoni na kutimuliwa alafu ulinzi mkubwa loh??? Haya ni majanga
kiukweli kama wananchi tunataka maendeleo ya nchi hii basi nafasi iwe wazi kwa bw sumaye maana rekodi yake inajulikana. Tusifate ushabiki na njaa ya vijipesa mnavyohongwa makanisani na misikitini na sasa hivi kaingia mashuleni ili awakamate wazazi.
Kazi kwenu wananchi.

Nyie ndo mliofutiwa Ziro,namaanisha
1.Cleopa Msuya ndiye Wzr Mkuu ktk miaka 2 ya mwisho ya Mz Mwinyi
2.Kutembea na ulinzi ama pasipo ulinzi si kigezo ama sifa ya mtu kufaa kugombea urais
3.Sumaye kama kweli anataka kutuaminisha kuwa anafaa kuwa Rais wa nchi hii basi atulie aache kulialia,kwanini kila mtu anayewaza Urais analia kuchezewa rafu na Lowassa?Jibu ni moja,mwenzao yuko mbali sana na bila shaka wanaamka na kushangaa kuwa kuwa kulishakucha siku nyingi..EL MTAA MWINGINE
 
Mkuu mbona hata Lowassa wakati wake wa Uwaziri Mkuu hakufanya madudu. Unaweza ukalinganisha Uongozi wake wa Uwaziri Mkuu na Mh. Pinda??? Kama unazungumzia wizi basi unamtaja JK, Lowassa ni Kiongozi mzuri.

Binafsi sijawahi kumsikia Lowassa akitamka kuwa anautaka Urais,sawa hawa akina Sumaye,Sitta,Membe,Makamba wanaweweseka nini?Wana madhambi gani hadi wamhofu Lowassa kiasi hiki?Akitangaza si wataikimbia nchi!
 
Sumaye alikuwa kweli miaka 10..lakini maamuzi gani magumu aliwahi yaamua? I prefer lowassa even if...He is even better than ------
 
mtasema yote,..sumaye si size ya lowassa,.sumaye aendelee kubwabaja tu,.mpaka sasa matokeo ni lowasa 3 sumaye 0

ni kweli sumaye si sawa na lowassa sababu lowassa anajulikana kwa ufisadi wake so sumaye hawezi kufanana na fisadi. Heri werevu hujitambua mapema
 
Huu umeme unamwangwa kaa uharoo unagharama na mipango bro. Mmekaa mjini tu njooni sasa mwone huku bush
 
tatizo mwalla hujaangalia pande mbili. Tambua ya kwamba sumaye amefanya kazi na kiongozi ambaye ana misimamo mikali na ni mtu asiependa mzaha mzaha. Lowassa kipindi chake amefanya kazi na rais ambae amesahau majukumu yake ipasavyo. Kama kweli lowassa ni dhaifu basi tangu aache madaraka tungeona serikali imepiga hatua kubwa sana. Mpaka sasa tangu ajiudhuru maisha yamezidi kupanda juu.
hahahaaaa ustake nnuneeee miee......
Unataka kuniambia maisha yalikua mazuri wakati wa lowassa?? Hahahaaa wee bw tambua kuwa tena kwa ujumla kwamba lowassa ndio sehem kubwa ya matatizo ya nchi hii haswa ktk kipindi chake kabla hajafukuzwa kazi kizungu (kustaafishwa)huyu ni waziri mkuu wa mwisho kukalia kiti hicho kwa kipindi kifupi sana na pia ndie aliyeweza kuhabu mambo mengi tu kwa muda mfupi wa utawala wake so kwa mimi huwezi kniambia eti lowasa ni mtu jasiri.. Kweli ni jasiri haswa pale anapoona kuna mambo za fedha huwa anjituma ili afanikishe miradi yake na si kwa ajili ya nchi.
 
MWALLA bana, unaandika thread kwa swali, na immediately (post ya kwanza tu kwenye thread) unaanza kumpigia debe Sumaye.

Mngemshauri Sumaye anapoitisha waandishi wa habari, basi aongee mambo ya maana na si kuattack watu hovyohovyo
 
hivi huyu lowassa si ndo nyerere alimkataa.sasa watanzania tunasemaje tunamuenzi mwl.kwa kuendelea kukumbatia fisadi kama hili.Mi nadhan ni wakati wa kupata mtu sahihi.sina shaka na uadilifu wa muheshimiwa sumaye.binafsi namkubali sana..lowassa hana utu hata kidogo yan yuko radhi kutoa mabillion kunnua urais,swali la kujiuliza ni vipi atazirudisha?!!!
tulikuelewa

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom