Prime ministers Sumaye miaka 12 vs Lowassa miaka 2 nani mzoefu?

Prime ministers Sumaye miaka 12 vs Lowassa miaka 2 nani mzoefu?

Tatizo Mwalla hujaangalia pande mbili. Tambua ya kwamba Sumaye amefanya kazi na kiongozi ambaye ana misimamo mikali na ni mtu asiependa mzaha mzaha. Lowassa kipindi chake amefanya kazi na Rais ambae amesahau majukumu yake ipasavyo. Kama Kweli Lowassa ni dhaifu basi tangu aache madaraka tungeona Serikali imepiga hatua kubwa sana. Mpaka sasa tangu ajiudhuru maisha yamezidi kupanda juu.
 
Hapa kwa Sitta Kaka umenena.
Hili jamvi kuanzia sasa naona limeshavamiwa na misukule ya mitandao ya walafi magamba wa uraisi, wote wanaotajwa wamechangia kwa namna moja au nyingine kuiharibu nchi hii. Kifupi mtamani uraisi yeyote kutoka CCM ni janga la kitaifa kama alivyothibitisha mwenyekiti wa CCM JK mwenyewe kuwa chama hiki sasa hivi ni tia maji tia maji kutokana na uvundo wa rushwa unaokikabili. Huyu Sitta naye hafai kwani ni zao la mtandao wa Kikwete, alisitisha ghafla mjadala wa bunge juu ya ufisad wa Richmond na kulea ufisadi, anpenda visasi na kumshambulia Lowassa kwa sababu alikosa uwaziri mkuu, walimsaliti Mpendazoe yeye na Nape kwa kuanzisha CCK na kumsusia baada ya kupewa uwaziri, ni wachumia tumbo hawa.
 
Mwinyi alimaliza na mzee Msuya miaka 2 ya mwisho,Sumaye alikuwa PM kwa miaka 10 na si 12
 
Nani mzoefu au nani mharibifu zaidi?! Nijuavyo mimi wote walisimamia kukomaza rushwa na ubadhirifu mkubwa kabisa wa raslimali za Taifa. Sumaye alipoka mil 50 NSSF pasipo kustahili, akapoka shamba kubwa Kibaigwa, mikataba mibovu, akauza nyumba za serikali nk nk; Lowasa ukitaja Richmonduli inatosha; wote maharamia wakubwa; Sumaye ni bifu ya kukosa ujumbe wa halmashauri kuu CCM; ni wakunyonga taifa likawasahau tukasonga mbele period
 
Hapo hakuna lowasa wala sumai wote hawafai huyo sumai si ndo aliuza nchi na mshikaji wake mkapa mikataba mibovu.EPA.eti wakaleta nn ile ya Tanesco Net group solution.wakauza NBC kwa bei ya.kutupa akajikopesha hels za nssf na ndugu yake mkulo.wengi hamtakubali lakini jembe la ukweli na linalo jiamini nimmoja tu samuel sitta .angalia alivoongoza bunge mpaka mafisadi wakamtilia zengwe.angalia ansvoongoza wizara ya EA hawa jamaa walitaka chukua ardhi yetu lakini wamekoma mpaka wamechukia na kuamua kujitenga.jk alionambali kumpa hiyo wizara.

Nani anafaaa?#Team Sumaye#
 
Hili jamvi kuanzia sasa naona limeshavamiwa na misukule ya mitandao ya walafi magamba wa uraisi, wote wanaotajwa wamechangia kwa namna moja au nyingine kuiharibu nchi hii. Kifupi mtamani uraisi yeyote kutoka CCM ni janga la kitaifa kama alivyothibitisha mwenyekiti wa CCM JK mwenyewe kuwa chama hiki sasa hivi ni tia maji tia maji kutokana na uvundo wa rushwa unaokikabili. Huyu Sitta naye hafai kwani ni zao la mtandao wa Kikwete, alisitisha ghafla mjadala wa bunge juu ya ufisad wa Richmond na kulea ufisadi, anpenda visasi na kumshambulia Lowassa kwa sababu alikosa uwaziri mkuu, walimsaliti Mpendazoe yeye na Nape kwa kuanzisha CCK na kumsusia baada ya kupewa uwaziri, ni wachumia tumbo hawa.

Ahsante Mkuu kwa kufunguka zaidi, kwahiyo hapa tunaona kuwa Sitta naye alikuwepo upande wa JK wakati wa Richmond. Ndio maana nikamwambia Mtoa mada Mwalla kuwa kama ni Wizi huanzia kwa JK mwenyewe. Rais ambae amekuteua ni vigumu sana kukupa kazi na kuikataa. Kubwa zaidi mbona hata Lowassa mwenyewe alimtaja JK ndani ya Bunge!!
 
Sumaye akiwa rais mm nakuwa shoga
ARE YOU SERIOUS???
shoga.jpg
 
Naomba nieleweke siko kwa ajili yakumpigia mtu debe nipo kwa ajili ya kushuri nikiongozi yupi anae onekana atatufaa kwa kipindi kijacho .kashfa nyingi zimetajwa mara EPA.mara Richmond nk. Lakini tukisngalia upande wa SAMUEL SITTA eti kashfa yske ni kuanzisha CCJ .kwangu mimi naona huyo nikiongozi mzuri sababu alikwisha choshwa na ufisadi ndani ya ccm ndio maana akaamua njia mbadala kwaajili yakumkomboa mt.
 
CCM kazi mnayo sie ngoja tuwaache muzikane wenyewe

CDM waacheni hawa CCM wasije walaghai na ujinga wao lichama lile lile miaka 50 ya uhuru makao makuu ya wilaya mpaka leo hazina hata umeme,vijijini je?
 
yes!! Ni mtazamo wangu tu bw mkubwa... Ila mwenye kutambua hili ataelewa nini umuhimu wa watu hawa wa2 tunaowazungumzia hapa jamvini.. Wapo wengi tu kina mzee sita, membe, hata magufuli pia yumo nae hivyo kazi ni kwako broo

SUMAYE ANATAKA NNI SASA. MIAKA 10 ya U-PM. Alifanya nini. Mbona alijitajirisha sana. Alimtumia shemeji yake Bw. KEENJA kutumia makusanyo ya Kodi za JIJ LA DSM na kumjengea majumba huko KibaHa na
kwingine. Amenunua mashamba MAKUBWA Kila kona ya nchi. Huyu ni MBINAFSI. Wakati wake alijenga Sekondari ngapi? University ngapi. KUBWA la kumkumbuka ni KUUZA NYUMBA ZA SERIKALI na KUUZA viwanda. Mshaurini Anyamaze. Anatia AIBU. HATA Watu wa Kwao walimnyima U NEC. Hafai
 
Huyu Lowasa mbona hana heshima ? Hivi kwanini hamheshimu aliyemzidi miaka 10 kiutendaji ? Pamoja na kwamba ccm yote haifai , lakini LOWASA hatakiwi kabisa ! huyu ni fisadi mkubwa aliyethibitishwa bila shaka yoyote na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania , nani amesahau hili ?

Hivi Lema ana heshima kweli kumwita Zitto kiongozi wake ndani ya chama ni msaliti na mnafiki??
 
SUMAYE ANATAKA NNI SASA. MIAKA 10 ya U-PM. Alifanya nini. Mbona alijitajirisha sana. Alimtumia shemeji yake Bw. KEENJA kutumia makusanyo ya Kodi za JIJ LA DSM na kumjengea majumba huko KibaHa na
kwingine. Amenunua mashamba MAKUBWA Kila kona ya nchi. Huyu ni MBINAFSI. Wakati wake alijenga Sekondari ngapi? University ngapi. KUBWA la kumkumbuka ni KUUZA NYUMBA ZA SERIKALI na KUUZA viwanda. Mshaurini Anyamaze. Anatia AIBU. HATA Watu wa Kwao walimnyima U NEC. Hafai

Ahsante Sana.
 
Sumaye akiwa rais mm nakuwa shoga

Utakuwa unampango wako. Ushoga wako na uraisi wa Sumaye vinahusiaje? Wewe utakuwa tayari ni Cameroon member sema tu unahitaji mgeni rasimi kufungua shughuli hiyo.
 
Unamfagilia huyu tuliyekuwa tukimuita zero? for sure wonders will never end!
 
wananchi msiumize vichwa vyenu... Binafsi naweza kusema sumaye anazosifa za kushika nafasi kuu. Akiwa w/mkuu miaka miwili ya mwisho ya mzee rukhsa na baadae kuendelea na mzee mkapa tumeweza kuona juhudi zake na mapungufu yake kiasi lkn amethubutu chini ya uongozi wa mkapa kuifanya nchi kuheshimika kwa wananchi na nje ya nchi kwa kudhibiti mifumuko ya bei ambayo mpaka leo hii ambacho siwezi kusahau ni nauli ya daladala aliipokea kutoka kwa mzee mwinyi ikiwa ni sh 150/= na tukamaliza nayo katika utawala wake mpaka alipo mkabidhi kanali jakaya ambaye binafsi nasema ameliyumbisha taifa kupitia kwa msaidizi wake mr lowassa aka msanii nimuite hivyo.
Kinacho shangaza mr lowassa amekuwa na juhudi nyingi za kujifanya anauchungu wa nchi hii wakati si kweli.
Nisiseme mengi juu ya huyu mr lowassa kwani anajulikana ndani ya miaka mi2 tu ameharibu na kufikia kutimuliwa hii ni kutokana na kukosa uadilifu katika madaraka aliyokabidhiwa.
Hivyo basi nahitimisha kusema kwamba wananchi tusihadaike na mh. Huyu msanii maana hana jipya.
Kama tunataka kweli maendeleo basi bw. Sumaye anaweza kutokana na historia yake na pia la muhimu zaidi ni yuko fiti kiafya na anajiamini hana kashfa, na mtu wa watu maana nilishawahi kukutana nae duka moja mitaa ya samora sikuweza kuamini waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu kupita wote walio pita awe hana ulinzi wa kutisha kama anavofanya bwana msanii maana nae nilikutana nae mitaa yake ya obay akiwa na jopo la ulinzi nilishangaa mbona sumaye waziri mstaafu hana ulinzi kama huu?? Wakati huyu msanii kakaa miaka 2 tu mjengoni na kutimuliwa alafu ulinzi mkubwa loh??? Haya ni majanga
kiukweli kama wananchi tunataka maendeleo ya nchi hii basi nafasi iwe wazi kwa bw sumaye maana rekodi yake inajulikana. Tusifate ushabiki na njaa ya vijipesa mnavyohongwa makanisani na misikitini na sasa hivi kaingia mashuleni ili awakamate wazazi.
Kazi kwenu wananchi.
Mkuu hapa umeniacha kabisaaa! tuseme hii ni kampeini au umetumwa na sumaye au ni wewe mwenyewe unajipigia debe mapema?! mbona kama umeingia chaka la simba huku ulikopitia?! Mh ngoja niwaachie wahusika waje hapa uone mtiti wake!
 
Back
Top Bottom