Prime ministers Sumaye miaka 12 vs Lowassa miaka 2 nani mzoefu?

Prime ministers Sumaye miaka 12 vs Lowassa miaka 2 nani mzoefu?

wananchi msiumize vichwa vyenu... Binafsi naweza kusema sumaye anazosifa za kushika nafasi kuu. Akiwa w/mkuu miaka miwili ya mwisho ya mzee rukhsa na baadae kuendelea na mzee mkapa tumeweza kuona juhudi zake na mapungufu yake kiasi lkn amethubutu chini ya uongozi wa mkapa kuifanya nchi kuheshimika kwa wananchi na nje ya nchi kwa kudhibiti mifumuko ya bei ambayo mpaka leo hii ambacho siwezi kusahau ni nauli ya daladala aliipokea kutoka kwa mzee mwinyi ikiwa ni sh 150/= na tukamaliza nayo katika utawala wake mpaka alipo mkabidhi kanali jakaya ambaye binafsi nasema ameliyumbisha taifa kupitia kwa msaidizi wake mr lowassa aka msanii nimuite hivyo.
Kinacho shangaza mr lowassa amekuwa na juhudi nyingi za kujifanya anauchungu wa nchi hii wakati si kweli.
Nisiseme mengi juu ya huyu mr lowassa kwani anajulikana ndani ya miaka mi2 tu ameharibu na kufikia kutimuliwa hii ni kutokana na kukosa uadilifu katika madaraka aliyokabidhiwa.
Hivyo basi nahitimisha kusema kwamba wananchi tusihadaike na mh. Huyu msanii maana hana jipya.
Kama tunataka kweli maendeleo basi bw. Sumaye anaweza kutokana na historia yake na pia la muhimu zaidi ni yuko fiti kiafya na anajiamini hana kashfa, na mtu wa watu maana nilishawahi kukutana nae duka moja mitaa ya samora sikuweza kuamini waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu kupita wote walio pita awe hana ulinzi wa kutisha kama anavofanya bwana msanii maana nae nilikutana nae mitaa yake ya obay akiwa na jopo la ulinzi nilishangaa mbona sumaye waziri mstaafu hana ulinzi kama huu?? Wakati huyu msanii kakaa miaka 2 tu mjengoni na kutimuliwa alafu ulinzi mkubwa loh??? Haya ni majanga
kiukweli kama wananchi tunataka maendeleo ya nchi hii basi nafasi iwe wazi kwa bw sumaye maana rekodi yake inajulikana. Tusifate ushabiki na njaa ya vijipesa mnavyohongwa makanisani na misikitini na sasa hivi kaingia mashuleni ili awakamate wazazi.
Kazi kwenu wananchi.
 
hivi huyu lowassa si ndo nyerere alimkataa.sasa watanzania tunasemaje tunamuenzi mwl.kwa kuendelea kukumbatia fisadi kama hili.Mi nadhan ni wakati wa kupata mtu sahihi.sina shaka na uadilifu wa muheshimiwa sumaye.binafsi namkubali sana..lowassa hana utu hata kidogo yan yuko radhi kutoa mabillion kunnua urais,swali la kujiuliza ni vipi atazirudisha?!!!
 
Frederick Tluway Sumaye (amezaliwa 29 Mei 1950) alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 27 Novemba 1995 mpaka 28 Desemba 2005.
 
Hapo hakuna lowasa wala sumai wote hawafai huyo sumai si ndo aliuza nchi na mshikaji wake mkapa mikataba mibovu.EPA.eti wakaleta nn ile ya Tanesco Net group solution.wakauza NBC kwa bei ya.kutupa akajikopesha hels za nssf na ndugu yake mkulo.wengi hamtakubali lakini jembe la ukweli na linalo jiamini nimmoja tu samuel sitta .angalia alivoongoza bunge mpaka mafisadi wakamtilia zengwe.angalia ansvoongoza wizara ya EA hawa jamaa walitaka chukua ardhi yetu lakini wamekoma mpaka wamechukia na kuamua kujitenga.jk alionambali kumpa hiyo wizara.
 
hivi huyu lowassa si ndo nyerere alimkataa.sasa watanzania tunasemaje tunamuenzi mwl.kwa kuendelea kukumbatia fisadi kama hili.Mi nadhan ni wakati wa kupata mtu sahihi.sina shaka na uadilifu wa muheshimiwa sumaye.binafsi namkubali sana..lowassa hana utu hata kidogo yan yuko radhi kutoa mabillion kunnua urais,swali la kujiuliza ni vipi atazirudisha?!!!
nafarijika kwamba wapo watu waelewa kama wewee na umethubutu kueleza ukweli halisia.. LOWASA HAFAI LABDA KWA ASIYE MJUA
 
Tuliwahi kukataa mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu kujitwalia nafasi ya watanzania wote kutusemea fulani ndiye anayefaa kuwa kiongozi na si fulani...hata kama sababu mnazo,ni mtizamo wenu!
Tunataka kiongozi ambaye atatuambia wazi,kwanini anataka kutuongoza,na hiyo miaka/miezi aliyopata fursa ya kuwa kiongozi wa watu ni jambo gani amelifanya ambalo leo tukimpa nafasi ya juu zaidi atalifanya kwa upana zaidi!
12 na 2 ni namba tu! Tunataka zaidi ya hapo!
 
Hapo hakuna lowasa wala sumai wote hawafai huyo sumai si ndo aliuza nchi na mshikaji wake mkapa mikataba mibovu.EPA.eti wakaleta nn ile ya Tanesco Net group solution.wakauza NBC kwa bei ya.kutupa akajikopesha hels za nssf na ndugu yake mkulo.wengi hamtakubali lakini jembe la ukweli na linalo jiamini nimmoja tu samuel sitta .angalia alivoongoza bunge mpaka mafisadi wakamtilia zengwe.angalia ansvoongoza wizara ya EA hawa jamaa walitaka chukua ardhi yetu lakini wamekoma mpaka wamechukia na kuamua kujitenga.jk alionambali kumpa hiyo wizara.
ni sawa maelezo yako na nilitangulia kusema kila mtu anamapungufu yake lkn ukweli unabaki palepale katika kipindi cha mkapa kazi zilifanyika sio kipindi hiki ambapo tulitaka mpaka kuletewa mvua ya mawingu kitaalamu haya si ni majanga??
BADO NAMUAMINIA SUMAYE SANA TU
 
tuliwahi kukataa mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu kujitwalia nafasi ya watanzania wote kutusemea fulani ndiye anayefaa kuwa kiongozi na si fulani...hata kama sababu mnazo,ni mtizamo wenu!
Tunataka kiongozi ambaye atatuambia wazi,kwanini anataka kutuongoza,na hiyo miaka/miezi aliyopata fursa ya kuwa kiongozi wa watu ni jambo gani amelifanya ambalo leo tukimpa nafasi ya juu zaidi atalifanya kwa upana zaidi!
12 na 2 ni namba tu! Tunataka zaidi ya hapo!

yes!! Ni mtazamo wangu tu bw mkubwa... Ila mwenye kutambua hili ataelewa nini umuhimu wa watu hawa wa2 tunaowazungumzia hapa jamvini.. Wapo wengi tu kina mzee sita, membe, hata magufuli pia yumo nae hivyo kazi ni kwako broo
 
Hata hivyo, alipoulizwa kama amejipanga kugombea urais mwaka 2015, Sumaye alisita kujibu kwa muda mrefu, lakini baadaye akajibu:

"Nasema hivi, kama ni kugombea nina haki zote, kama ni uwezo ninao, kama ni imani ya Watanzania kwa sehemu kubwa ninayo. Kilichobaki ni uamuzi tu wa mimi kutamka. Kwa hiyo sijatamka msije mkasema nagombea urais. Nasema tu na mimi katika Watanzania wanaofikiriwa na mimi nasikia nimo. Kwani ninyi hamnifikirii? Sasa itakapofika huko mbele, si tutaamua wakati huo?"
 
Huyu Lowasa mbona hana heshima ? Hivi kwanini hamheshimu aliyemzidi miaka 10 kiutendaji ? Pamoja na kwamba ccm yote haifai , lakini LOWASA hatakiwi kabisa ! huyu ni fisadi mkubwa aliyethibitishwa bila shaka yoyote na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania , nani amesahau hili ?
 
tuliwahi kukataa mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu kujitwalia nafasi ya watanzania wote kutusemea fulani ndiye anayefaa kuwa kiongozi na si fulani...hata kama sababu mnazo,ni mtizamo wenu!
Tunataka kiongozi ambaye atatuambia wazi,kwanini anataka kutuongoza,na hiyo miaka/miezi aliyopata fursa ya kuwa kiongozi wa watu ni jambo gani amelifanya ambalo leo tukimpa nafasi ya juu zaidi atalifanya kwa upana zaidi!
12 na 2 ni namba tu! Tunataka zaidi ya hapo!

ni kweli sana lakini nafasi hiyo kumpa lowasa ni sawa na kuonja sumu .
 
Mtasema yote,..SUMAYE SI SIZE YA LOWASSA,.sumaye aendelee kubwabaja tu,.Mpaka sasa matokeo ni LOWASA 3 SUMAYE 0
 
nafarijika kwamba wapo watu waelewa kama wewee na umethubutu kueleza ukweli halisia.. Lowasa hafai labda kwa asiye mjua

pro sumaye at work sumaye hana jipya amebaki kulialia...2015 -2025 lowasa presdent
 
yes!! Ni mtazamo wangu tu bw mkubwa... Ila mwenye kutambua hili ataelewa nini umuhimu wa watu hawa wa2 tunaowazungumzia hapa jamvini.. Wapo wengi tu kina mzee sita, membe, hata magufuli pia yumo nae hivyo kazi ni kwako broo
Halafu nynnyi magamba mnchusha sana, yaani nchi hii mlivyoivuruga bado mnapigiana upatu magamba? Yaani hakuna watanzania wengine wenye uwezo wa kuongoza nchi hii zaidi ya magamba yaliyolaanika? Kama unampenda sana Sumaye na unaamini anafa, kwa nini anang'ana kukaa katika chama kinchowakumbatia mafisadi unaowataja kama Lowassa? Kawani CCM ni mama yake Sumaye au na yeye ni fisadi kama wenzake?
 
ni kweli sana lakini nafasi hiyo kumpa lowasa ni sawa na kuonja sumu .

Huu utamaduni wa kupendekeza na kupigiana chepuo ndio uliotufikisha tulipo...nidhanivyo kama ni sahihi hata hii dhana ya kwamba Rais akitoka bara basi msaidizi wake atoke visiwani haina maana kwa sasa! Muhimu ni kuwapa wananchi elimu ya uraia ya kutosha na mtu achaguliwe si kwa ajili ya kumfurahisha fulani so far haya ni maisha...kumchagua mtawala mbovu kwa kipindi cha miaka mitano ni sawasawa na kujipa 'poo' ya maisha kwa miaka mitano of which umeshajipotezea miaka mitano ya maana kimaisha!

Sina sababu ya kuhoji uhalali na kutokuwa halali kwa Mwalimu kuchukua nchi miaka yake ile...ni mwasisi! Nafikiri kwa sababu ambazo wanazijua wenyewe akamwachia kijiti mzee Mwinyi na kama haitoshi akampendekeza mzee Ben!

Kama ni mtu wa kucheza na sequency vyema utaona Nyerere Mkristu,Mwinyi Muisilamu,Ben Mkatoliki na baba Riz wa Msoga(whom amechukua kombe kwa namna yake mwenyewe).

Kwa zama tulizonazo hatuhitaji kumchagua mtu kwa ukristu/Uisilamu wake,hasha hatutamchagua mtu kwa kuwa historia inamsafisha kwa namna moja ama nyingine,hatutamchagua mtu kwa sababu ya kabila lake na haturtaacha kumchagua kwa sababu ya kabila as well!

Lowasa ni mchafu/msafi machoni mwa beholders,kuna wenye sababu ya kutambua usafi wake na wenye sababu ya kuhoji usafi wake,all in all si usafi wa Sumaye wala uchafu wa Lowasa utakaoweze kutukwamua tulipo kimaisha ila mtu commited anayejua kwanini watu wamempa ridhaa!
 
Hapo hakuna lowasa wala sumai wote hawafai huyo sumai si ndo aliuza nchi na mshikaji wake mkapa mikataba mibovu.EPA.eti wakaleta nn ile ya Tanesco Net group solution.wakauza NBC kwa bei ya.kutupa akajikopesha hels za nssf na ndugu yake mkulo.wengi hamtakubali lakini jembe la ukweli na linalo jiamini nimmoja tu samuel sitta .angalia alivoongoza bunge mpaka mafisadi wakamtilia zengwe.angalia ansvoongoza wizara ya EA hawa jamaa walitaka chukua ardhi yetu lakini wamekoma mpaka wamechukia na kuamua kujitenga.jk alionambali kumpa hiyo wizara.

Hapa kwa Sitta Kaka umenena.
 
nafarijika kwamba wapo watu waelewa kama wewee na umethubutu kueleza ukweli halisia.. LOWASA HAFAI LABDA KWA ASIYE MJUA

Mkuu mbona hata Lowassa wakati wake wa Uwaziri Mkuu hakufanya madudu. Unaweza ukalinganisha Uongozi wake wa Uwaziri Mkuu na Mh. Pinda??? Kama unazungumzia wizi basi unamtaja JK, Lowassa ni Kiongozi mzuri.
 
Back
Top Bottom