Pride Comes Before the Fall: CHADEMA inabidi wajipange upya

Njia sahihi ni kuyasema yapi hayana msingi. Ukinionyesha na kunithibitishia wapi nimekosea, sitasita kujirekebisha. Ni kwa sababu najua uwanja haupo sawa ndio maana nimesema nilichosema.
Ni kweli watanganyika wa leo sio wa jana. Pamoja na kuonyesha wazi muamko wao kuhusu Katiba na mfumo wa uchaguzi, walikaa kimya muda wote Slaa alipokuwa ndani. Hatuwaoni wakipinga kukamatwa kwa Lissu. Hii ni tofauti kabisa na amsha amsha iliyofanywa na CDM wakati wa kesi ya Mbowe. Wengi walioongoza amsha amsha ile leo wanaitwa wasaliti.
Nasubiri kwa hamu kila kitu kuwekwa wazi. Nikionekana kuwa nimekosea, nitakula matapishi yangu bila kusita.

Amandla...
 
NO REFORM NO ELECTION umeamua kuongea kinyume
 
Kwa kuwa umeniita mjinga, bc tuishie hapo hapo.
 

Not quite, and here's why.

To say CCM “played CHADEMA like a fiddle” is to grossly underestimate the strategic depth and long-term resilience of CHADEMA as a movement — and overstate CCM’s ability to indefinitely control political outcomes through manipulation and repression.

Yes, politics is chess, not checkers. But let’s not confuse short-term tactics with strategic victory. If CCM anticipated Lissu’s boldness and thought that jailing or silencing him would neutralize CHADEMA, they fundamentally misunderstood the moment. Lissu’s voice isn’t just loud — it resonates. His fearlessness isn’t a liability; it’s a catalyst. And history has shown us time and again: attempts to silence truth-tellers often amplify their cause.

Freeman Mbowe’s equanimity is indeed a virtue — but leadership isn’t a monolith. CHADEMA doesn’t have to choose between calm and fire, moderation and confrontation. It can, and should, harness both. The brilliance of a revolutionary movement lies in its ability to deploy different tools at different times — the steady hand of Mbowe and the sharp spear of Lissu are complementary, not contradictory.

If anything, what we're witnessing isn’t CHADEMA being outplayed. It's the regime revealing its fear — fear of democratic accountability, of mass mobilization, of a Tanzania that refuses to remain silent. The real game of chess is just beginning.
 

Kwa hiyo unasema nini haswa, Fundi?

Kwamba CCM ni wajanja kiasi cha kuigeuza CHADEMA kuwa genge la vipofu wanaochezeshwa bila kujua? Hiyo ni tafsiri nyepesi mno ya hali halisi — na pengine ni upuuzi wa kisiasa uliopambwa kwa mbwembwe za kijanja.

Kama CCM walidhani kuwa kumpa Lissu nafasi ya uenyekiti ni mtego wa kujitakia, basi walikosea kwa kiwango cha kihistoria. Kujitokeza kwa Lissu si ajali ya kisiasa — ni matokeo ya kiu ya Watanzania ya kuona uongozi usioogopa kusema ukweli hata mbele ya msumeno wa dola. Na kama walitarajia atazungumza kwa sauti — basi walikuwa sahihi. Lakini wakidhani hiyo sauti itaweza kuzimwa kwa vipingamizi vya kisheria vya kutungwa-tungwa, basi wamesahau somo la historia: haki hucheleweshwa, lakini haizimwi.

Na kuhusu Freeman Mbowe kuwa na utulivu zaidi — hiyo si hoja ya udhaifu wa Lissu, bali ni uthibitisho wa nguvu ya CHADEMA kama taasisi yenye sura nyingi. Hili si kanisa lenye kasisi mmoja; ni vuguvugu la watu walioamka, lenye akili, hasira, na matumaini. Mbowe ni busara. Lissu ni kishindo. Na Tanzania inahitaji vyote viwili.

Kwa hiyo kama huu ni mchezo wa chess, basi ni vyema CCM waelewe kwamba pia wanaocheza nao wamejifunza mchezo huo. Na safari hii, si rahisi kuvunja meza.
 
Hujaskia juzi ACT wanasema kanuni haziko sawa, zina kasoro wataenda mahakamani kuzipinga lakini wamesaini, hivi maana ya kusaini si nikukubaliana na kilicho andikwa? Sasa kama ulikubali unaenda mahakamani kufanya nn?
Hiki ni kituko 😂
 
Kwa hiyo unasema nini haswa, Fundi?
Mbona nimesema mengi tu?
Kwamba CCM ni wajanja kiasi cha kuigeuza CHADEMA kuwa genge la vipofu wanaochezeshwa bila kujua? Hiyo ni tafsiri nyepesi mno ya hali halisi — na pengine ni upuuzi wa kisiasa uliopambwa kwa mbwembwe za kijanja.
Kila mmoja ana mtazamo wake. Hatuwezi kufanana wote. Mimi sikubaliani na wewe kuwa ni upuuzi.
Lissu sio wa kwanza kuzungumza kwa sauti. Mtikila alizungumza bila kuogopa pengine kuliko hata Lissu. Kwangu mimi shida ya watanzania ni kila siku kutegemea atakuja mtu wa kuwakwamua. Alikuweko Mrema, tukamfurahia Mtikila, tukamfurahia Maalim na wengine wenye uthubutu lakini hali iko pale pale. Sasa hivi tuna Lissu, na yeye asipoangalia ataachwa solemba na hao hao watanzania wenye kiu.
Na kama walitarajia atazungumza kwa sauti — basi walikuwa sahihi. Lakini wakidhani hiyo sauti itaweza kuzimwa kwa vipingamizi vya kisheria vya kutungwa-tungwa, basi wamesahau somo la historia: haki hucheleweshwa, lakini haizimwi.
Umesahau somo lingine la historia kuwa haki ikicheleweshwa sana ni kama imezimwa.
Nakubaliana na wewe kwenye hili. Muungano wa Mbowe na Lissu ulikuwa formidable. Shida ni kuwa Team Lissu inaona kuwa Mbowe hana nafasi ndani ya CDM na wamefanya kila mbinu kum undermine. Wao wanaona ni wao peke yao wenye mtazamo sahihi. Lissu amewekwa kwenye pedestal na hairuhusiwi kutofautiana nae. CDM inaelekea kuwa cult.
Kwa hiyo kama huu ni mchezo wa chess, basi ni vyema CCM waelewe kwamba pia wanaocheza nao wamejifunza mchezo huo. Na safari hii, si rahisi kuvunja meza.
Bahati mbaya CDM imewatenga waliojifunza huo mchezo na meza imeisha vunjika.

Amandla...
 

Twende kazi, taratibu:

Ni kweli, kila mtu ana mtazamo wake — lakini si kila mtazamo una uzito wa hoja au msingi wa kweli. Na ndiyo maana baadhi ya mawazo yakiachwa yakiwa hayajarekebishwa, hugeuka sumu ya fikra kwa wengine.

Unaposema CCM si wajanja wa kuigeuza CHADEMA kuwa "genge la vipofu", halafu papo hapo ukakiri kuwa “CHADEMA imewatenga waliokuwa wamejifunza mchezo wa chess na meza imevunjika” — hapo umethibitisha usichotaka kukiri: kwamba kuna mikono ya kisiasa inayohujumu CHADEMA, na hiyo ni hoja yangu ya msingi. Ukiondoa neno “wajanja,” bado hoja ni ile ile — kuna operesheni za makusudi za kuingilia, kugawa, na kudhoofisha upinzani. Sasa kama si CCM, ni nani?

Kuhusu Lissu kulinganishwa na Mtikila: Mtikila alikuwa mpambanaji, hilo halina mjadala. Lakini hoja yangu haikuwa kwamba Lissu ndiye wa kwanza kuzungumza kwa sauti, bali ni kwamba katika mazingira haya ya sasa, Lissu ndiye anayebeba uzito wa kiongozi wa kisasa asiyeogopa mamlaka. Kwa hiyo, kumlinganisha na waliotangulia si hoja ya kumdhoofisha — bali ya kuthibitisha kwamba historia inaendelea, na kila kizazi kina askari wake. Sasa, kama Watanzania wanachoka haraka na mashujaa wao — hiyo si kasoro ya mashujaa, ni tatizo la taifa lenye ndoto fupi.

Na hoja kuwa haki ikicheleweshwa sana ni sawa na kuzimwa — ni kweli, lakini tukikubali hoja hiyo kama hitimisho, basi ni sawa na kusema “acha tupoteze matumaini kabisa.” Hapana. Historia pia imetufundisha kwamba haki ya kweli huwa ngumu sana kupatikana — lakini huja tu, kwa wanaokataa kukata tamaa. Ndiyo maana wapo bado wanaopambana.

Kuhusu suala la Mbowe na Lissu: hakuna aliyesema Lissu hawezi kukosolewa. Isipokuwa, kuna tofauti kati ya kosoa kwa nia ya kujenga, na undermining kwa lengo la kumchafua kisiasa. Ukosoaji wa hoja ni sehemu ya afya ya demokrasia. Lakini tukifikia hatua ya kuchafua jina la mtu kwa kutumia propaganda za ndani — tumeacha siasa, tumeingia kwenye fitna. CHADEMA si cult — lakini wanaojaribu kuipaka tope la cultism ni wale wanaotaka ionekane dhaifu ili wapate nafasi ya kuua matumaini.

Na mwisho, hoja yako kuwa meza ya chess imeshavunjika — hiyo ni tamko la kukata tamaa. Lakini historia ya siasa ni kama mto: unaweza kupinda, unaweza kufurika, lakini hauwezi kusimama. Waliovunja meza, wasidhani wameua mchezo. Waliopindua kete, wasidhani wanamiliki ubao.

CHADEMA ni taasisi — si jina la mtu. Na kizazi cha mabadiliko kipo kazini, hata kama kelele za hofu zinapigwa kutoka pembeni.
 

Yupo jela sasa na mama kapita bila kupingwa unaumia bado?
 
Ila ushindi wa Lissu bado unakutesa sana sana ndugu.
 
Umemuita mjinga bila sababu; na hiyo ndio CDM ya sasa. Uwezo wa kujenga hoja umepungua sana. Miaka ya zamani vijana wa CDM walitisha hapa jukwaani kwa michango yao constructive..

Ukiona kijana anaongea Utanganyika jua kuna tatizo hapo; na for the benefit ya Nchi ni nadra kushinda uchaguzi wowote. Hata kama nchi ilikosea lakini sisi wabara ni watanzania zaidi kuliko watanganyika. Hiyo ni tunu yetu, hata mataifa ya ulaya yamekosea mambo mengi lakini yanajitahidi kumantain hayo waliyoyakosea hadi leo. Ni tunu zao. Imagine UK hadi leo wana utawala wa kifalme na hawana mpango wa kuuacha, sisi miaka sitini tu tunaongea utanganyika. Mbaya sana hii. Kwa mtu aliyezaliwa 1980 anaijua hata hiyo Tanganyika?

Ukirudi kwenye mada; mtoa hoja yuko sahihi, ni rahisi zaidi kudeal na CDM ya leo kuliko ya zamani. Imagine baada ya TAL kuwekwa ndani, kiongozi gani mwingine kwa sasa anaweza akaitisha mkutano nje ya jimbo lake na akaatract mass kubwa ukimtoa Makamu kwa Cheo chake? (Angalia hata mwitikio wa mkutano wa Heche jana mbarali na kyela) Yaani pambalu aende Arusha alafu apate watu? Sosopi aende Maswa apate watu?? lakini CDM ya sasa inawaona wastaafu ni wasaliti... wakati CCM ina hazina kubwa. Huwezi kushinda uchaguzi kama hauna akili za kisiasa....
 
Twende kazi, taratibu:
Sawa kabisa.
Ni kweli, kila mtu ana mtazamo wake — lakini si kila mtazamo una uzito wa hoja au msingi wa kweli. Na ndiyo maana baadhi ya mawazo yakiachwa yakiwa hayajarekebishwa, hugeuka sumu ya fikra kwa wengine.
Sawa kabisa. Lakini atakayepima uzito huo wa hoja ni nani maana kila mmoja anajiona yuko sahihi? Badala ya kukazania kubadilisha mawazo ya mwenzako ni vyema zaidi kukubali kutofautiana kimawazo na kuheshimu haki ya kila mmoja kuwa na mawazo yake. Ni wajibu wa hao wengine kujifunza, na kutafakari kwa umakini kabla ya kuamua mtazamo upi ni sahihi kwake hata kama atatofautiana na wengine.
Huko ndiko kutafuta wachawi ninakozungumzia. Wanaohujumu CDM ni wao wenyewe ama kwa makusudi au kwa kutokufahamu. CCM haikuendesha kampeni ya kumgeuza Mbowe kuwa msaliti namba moja. Kama walihusika, walipita tu kwenye mlango uliofunguliwa na CDM. Haingii kichwani kuwa leo hii watu kama Mbowe, Ruge, Sigrada, Kiwanga, Mrema waitwe wasaliti na CDM. Wanaomwaga hiyo sumu ni CDM sio CCM.
Hapana. Hoja yako ya kwanza ilikuwa ni kumgeuza Lissu kuwa yule tuliyeahidiwa kuwa atakuja kutukomboa. Bahati mbaya yeye kama ilivyokuwa kwa waliomtangulia ameanza kuamini hivyo. Ametoka kuwa mtu aliyesema kuwa hataki machawa mpaka kuwa mtu ambae sura yake inapamba T-shirt za chama kama ilivyo kwa mpinzani wake.
Lakini unaposema kuwa unapambana lakini unaogopa gharama za mapambano hayo ni kukata tamaa. Mshindani wako anatakiwa ajue kuwa utapambana kwa gharama yeyote na muda wowote ili haki ipatikane atakuheshimu zaidi. Ndio maana kile ambacho mnaona kuwa ni weakness ya Mbowe ni strength yake. CCM wamemrushia kila kitu lakini bado amesimama. Wanajua hawa wa sasa wasipofanikiwa hivi karibuni watainua jamvi na kuwalaumu wananchi.
Na huko kukosoana kwa lengo la kuchafuana kuliasisiwa na nani? Kumuita dikteta uchwara ni kumueleza kuwa anatakiwa aruhusu mawazo mbadala ama sivyo hata kuwa tofauti na yule aliyemuita dikteta uchwara. Nasema kuwa ni cult kwa sababu ninayoona yanaendelea. Mguse Lissu uone matusi utakayoporomoshewa bila kujibiwa hoja yako. G55 na Sigrada ni mfano hai wa hili. Badala ya kujibiwa hoja zao wanaporomeshewa matusi. Hiyo kama sio cult ni nini?
Hapana. Kinachonipa tumaini ni kuwa wale ambao wana uzoefu wa kukijenga chama chao bado wapo. Hao wataikarabati hiyo meza au kununua nyingine na mchezo utaendelea.
CHADEMA ni taasisi — si jina la mtu. Na kizazi cha mabadiliko kipo kazini, hata kama kelele za hofu zinapigwa kutoka pembeni.
Kinachofanyika sasa ni kuigeuza kuwa jina la mtu. Na taasisi inajengwa. Kuiita taasisi hakumaanishi kuwa kweli ni taasisi.

Kizazi cha mabadiliko bado hakijafika. Mashujaa wa kwenye keyboard peke yao hawatafua dafu. Wanahitaji kuwakumbatia wenzao katika struggle, sio kuwa alienate.

Amandla...
 
Mimi ni jobless lakini niko happy kuona CHADEMA inafeli kisiasa kwa sababu, wako hush sana halafu ni waongo kupitiliza na ndio wanafanya watanzania wawe idiots.
 
Dhambi ya ubaguzi itawatafuna sana CHADEMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…