Pride Comes Before the Fall: CHADEMA inabidi wajipange upya

Hivyo vyama vingine vya upinzani mbona haviungani nje ya cdm ili vifanye hicho unachoamini? Au ni lazima cdm iungane navyo?
 
Kuwa mwanasiasa ni kukubali kiburuzwa, ukiwa hukubali kuburuzwa ww sio mwanasiasa bali ni mwanaharakati😂
 
Waliishaambiwa CCM ina mbinu 1000 za kushinda Uchaguzi Mkuu.
 

You miss the point.

Point yangu ni kuwa, CHADEMA haiwezi kurudi nyuma kwa kuisubiri TADEA ambayo haiko serious na misingi ya kuanzishwa kwao.

Hujaskia juzi CHAUMA wanasema wao wanaona Tume imewatendea haki, na wanaupongeza? Sasa unataka CHADEMA waongee nao nn?

Hujaskia juzi ACT wanasema kanuni haziko sawa, zina kasoro wataenda mahakamani kuzipinga lakini wamesaini, hivi maana ya kusaini si nikukubaliana na kilicho andikwa? Sasa kama ulikubali unaenda mahakamani kufanya nn?

Wanacho kifanya CHADEMA ni kitu sahihi na Wakati sahihi, Hata kama Mwisho wake itakua ni kukosa Uwakirishi kwenye serikali, kwani itakua Mara ya kwanza? Si juzi tu wameshiriki serikali za mitaa kwa ukamilifu wamepata nini?

Mnaingia kwenye uchaguzi huu butu ni kudance tune ya CCM, kwa kuionyesha Dunia wanafanya chaguzi za kidemocrasia mean while wanaiba kura, kufunga wapinzani.

Kwa sasa hivi, CHADEMA wamesema basi, Hapa kinacho subiriwa ni muitikio wa wapiga kura, Wakikubaliana na Hoja za CHADEMA kwa kutokushiriki uchaguzi basi automatically serikali itakayo chaguliwa itakua batili
 

Technically, mpaka sasa Chadema hawajajitoa kwenye uchaguzi. Ni zengwe la CCM kupitia tume kuhakikisha kuwa Maza anapita bila kupingwa kama walivyofanya ndani ya vikao yao.

Chadema watumie hii nafasi kwenda Mahakani kuipa kore publicity kampeni ya No Reforms No Election.
 
Hivyo vyama vingine vya upinzani mbona haviungani nje ya cdm ili vifanye hicho unachoamini? Au ni lazima cdm iungane navyo?

Waulize Mkuu.

Kwani ushawai sikia mgombea wa TADEA au CHAUMA akishikiriwa Rumande? Au kulalamika kuibiwa kura?

Hao wapo kama wapo, labda siku wasipewe ruzuku ndo wataanza kupiga kelele
 
Ni kweli hawajajitoa. Na inawezekana kuwa bado sheria inawapa nafasi ya kushiriki kwenye uchaguzi. Kama hiyo ni strategy yao basi watakuwa naive sana. Tangu lini sheria au Mahakama zetu zimewanyima CCM kitu wanachotaka? Wanasahau kuwa kuna wabunge 19 wa "Chadema " ambao wamehudumu term nzima ya 2020-2025 ingawa Chadema iliwafukuza kutoka kwenye chama? Baadhi yao sasa hivi wanafanya campaign za wazi kwa ajili ya CCM ingawa wanahesabiwa Bungeni kuwa ni wawakilishi wa Chadema.
Ukweli ni kuwa hawatapata reliefi yeyote Mahakamani kabla ya uchaguzi kufanyika.

Baada ya uchaguzi wanaweza kupewa haki ya kushiriki chaguzi zinazofuata.

Mapambano kuhusu Katiba mpya yataongozwa na ACT-WAZALENDO. Wasipokuwa makini CDM wanaweza kuwa watazamaji tu kama hawajirekebisha.

G-55 walitambua hili lakini walionekana kama wasaliti. Wajuaji walitia pamba masikioni.

Amandla...
 
Chadema hawataki kukubali kuwa wamekosea, wao kila muda wanajiona wapo sahihi na wanajiona maendeleo ya Tanzania hayawezekani bila wao.

Wanachama wao wa hapa JF wameenda mbali ety Tz itawekwa kwenye vikwazo vya kiuchumi 😂 guys WTF is this
Tatizo masses wametekwa nyara na mawazo au maoni ya watu wachache bila kuona mtego huo.

Outcome sio nzuri ni kama wamejipandikiza kirusi cha kukimaliza chama kwa muda mfupi bila kujua madhara yake.KILL ME QUICK SYNDROME.
 
Hii “No Reforms, No Elections” campaign ingefanikiwa very easily kama ingebebwa na vyama vyote vya upinzani.
Haiwezekani vyama vyote vikawa na mtazamo sawa. Miaka mingi ingepotea kusubiri jambo kama hilo kutokea.
 
Kazi ipo safari hii.
 
Nilishanga sana bila aibu wanasema wale ni watu wa Mbowe !.

Lissu na genge lake hawaendi popote iwapo wataendelea na misimamo ya kipuuzi.
 
Kuna watu mnapenda kupindua pindua mambo mwonekane wachambuzi wakali kumbe hamnakitu. Yaani wewe huna tofauti na mchambuzi wa mpira ambaye anasubiri mechi imeisha ndio anaanza kuonyesha umahiri wa kuchambua mbinu za mpira kwa timu zilizocheza! Hizo mbinu za CCM za kumtaka Lisu kwa kumsifia Mbowe uliwapa wewe!?
 
Hili ndilo linalo wasumbua. Una criticise bila substance. Mimi nimekuwa nayazungumzia haya hata kabla ya uchaguzi wa CDM kufanyika. Ni mmoja wa waliopinga Mbowe kujiengua. Nilisema wazi na mapema kuwa mambo ya Wenje kutumika kumhonga Lissu yalikuwa ni usanii tu. Baada ya uchaguzi, tulishauri CDM waponye kwanza majeraha. Nimesema kampeni ya NO REFORM NO ELECTION inatakiwa kuboreshwa. Nimesema kilichotokea Njombe ni dalili ya vindictiveness iliyokuwepo ndani ya CHADEMA na kilipoteza opportunity ya kuponya majeraha. Nime unga mkono msimamo wa G-55. Badala ya kuni challenge kwenye haya unaleta mambo ya mpira!

Amandla...
 
Chadema hawataki kukubali kuwa wamekosea, wao kila muda wanajiona wapo sahihi na wanajiona maendeleo ya Tanzania hayawezekani bila wao.

Wanachama wao wa hapa JF wameenda mbali ety Tz itawekwa kwenye vikwazo vya kiuchumi 😂 guys WTF is this
Watu wajinga na waoga kama wewe ndio wanafanya Watanganyika kuonekana hatuna akili. Fikiria tume ngapi zimeundwa huko tulipo toka , kusudi ilikuwa ni kuweka mizania ya kisiasa sawa(Siasa shirikishi, ya Watanganyika wote kuwa na sauti katika maamuzi ya taifa lao.

Tume hizi za Jaji Kisanga, Jaji Nyalali, Jaji Bomani na mwisho Jaji Warioba. Coincidentally mapendejezo ya tume hizi yote yalifanana katika mambo mengi. kutaka kulikomboa taifa letu kisiasa.

Hiki ndicho CDM wanachodai. Mapendekezo ya hizi tume yafanyiwe kazi. Miaka 40 imepita sasa toka tume ya mwanzo ya Jaji Kisanga, hamna hata kimoja kilicho tekelezwa na chama tawala. Alafu unakuja hapa kulia heti CDM wanajiona wapo sawa!!!!! Tumia Akili yako vizuri.
 
Wakati CDM wanaendelea kutafuta mchawi CCM na ACT-WAZALENDO wanajipanga kwa uchaguzi ujao. Sitamlaumu Aida, Suzan na Ruge na wengine wakijiunga na ACT-WAZALENDO.

Amandla...
 
F. Mchundo, umeandika mengi yasio na msingi. Naona unajifurahisha tu. Uwanja wa Siasa haupo sawa na hili unalifahamu vizuri. Na Watanganyika wa leo sio wa jana. Muda ni Mwalimu mzuri, muda sio mrefu kila kitu kitakuwa wazi. Ukweli na Uongo utajitenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…