Press ya Halima imeongeza maswali mengi kuliko majibu. Amezungumza vitu vingi lakini "theme" ya press yake haieleweki

Kutetea demokrasi na katiba ya Nchi ni namna moja ya kutafuta ugali kwani haya majizi na mafisadi hayataweza tena kuiba chaguzi ili kung’ang’ania madaraka.
Mlishindwa uchaguzi kwa halali na sasa mnaweweseka tu kwa machungu ya kuambulia mbunge mmoja. Tumewachokaaaa
 
Hakuna lolote CHADEMA ni ile ile isiyo na kichwa wala miguu, wakati mwenyekiti wenu anabadili gia angani mwaka 2015 mlimchukulia hatua gani ? Ni machungu tu ya kushindwa uchaguzi ndio kinamsumbua huyo DJ wenu. Na ndio mnajimaliza wenyewe maana hili ndio anguko la CHADEMA maana dhambi yake inailemea na wala haitainuka tena.
 
Huo unasema andiko bora ? We vipi Mbona huyo mwenyekiti wenu alipobadili gia angani mwaka 2015 hakusema chochote ? Hii ni andiko la kipuuzi kuliko maandiko yote kwa sasa.
Andiko bora kabisa with full and complete analysis.Wee Jamaa mzazi wako hakupoteza ada.
 
Hiyo miaka ya 2010 na 2015 walienda kwa sababu mbowe alishinda uchaguzi

Kwa kuwa 2020 Mbowe ameshindwa hakuna wote kwenda bungeni .View attachment 1639208
Kuhusu "udikteta" wa Mbowe kwenye maamuzi ya chama kila mmoja anafahamu. Wewe utusaidie kujua Mdee na timu yake waliwezaje kufika na kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya mwenye chama?
 
Nadhani watu wengi hawajamuelewa Mdee;

Kuna mambo hajataka kuweka Public kwa sasa.

Anasubiri muda muafaka ufike.

Na muda huo ni mpaka hiyo process ya vikao vya ndani ikifeli ataruka hewani.

Kamheshimu Sana Mwenyekiti wake na katoa nafasi ya kupokelewa tena.
Ile siku bwana mdogo Ndugai anamuapisha Polepole lakini anaongelea mambo ya Chadema na kusema kuna "unyanyasaji wa kijinsia" akiwatumia akina Halima Mdee kama Mfano. Halima anafanya press yake na kusema Chadema hakuna mfumo dume kama inavyoelezwa, maana wao wamekuwa viongozi huko. Ndugai anajionaje?
 
Hiyo miaka ya 2010 na 2015 walienda kwa sababu mbowe alishinda uchaguzi

Kwa kuwa 2020 Mbowe ameshindwa hakuna wote kwenda bungeni .View attachment 1639208
Kwa hiyo kama vipindi hivyo walienda ni yeye ndiye anayepaswa kuamua kwamba na safari hii pia waende.

Huyu mwanamke wasimlee yeye pamoja na wenzake waende kwa hao mabwana zao wanaowadanganya mbona na wenyewe wana chama chao si wawachukue tu mbona huko nyuma wamekuwa wakiwanunua wabunge na madiwani wa upinzani, wawachukue na hawa bure waende nao ccm.
 
Na, Malisa GJ

Press ya Halima imeongeza maswali mengi kuliko majibu. Amezungumza vitu vingi lakini "theme" ya press yake haieleweki. Hata yeye ukimuuliza "theme" ya Press yako ilikua nini hawezi kusema.

Ukiachana sura zao zenye mashaka na majuto, leo vyombo vyote vya habari vya serikali na mamluki wake vimeshiriki press hiyo. Kuanzia TBC, DailyNews, Uhuru hadi Tanzanite ya Musiba. Hivi hadi hapo hamjajua nani wapo nyuma yao? Uliwahi kuona TBC au Tanzanite kwenye press ya Mbowe?

Hata hivyo watu walitegemea aeleze ni nani aliyepeleka majina NEC? Kwanini walikiuka maagizo ya kamati kuu? Yalikua maelekezo ya nani? Kwanini walienda kujiapisha? Na kwanini alisema uongo kuwa Mwenyekiti alimpa baraka?

Lakini Halima kakwepa maswali hayo katika namna ya kupanic. Amesema hawezi kujibu nani alipeleka majina wala kwanini walienda kuapa kwa sababu eti watakata rufaa baraza kuu. Kwahiyo majibu watayatoa huko baraza kuu na sio kwenye press. Sasa kama wamekata rufaa baraza kuu hii press wamefanya ya nini? Non sense.

Pamoja na kuongea kwa kujichanganya sana, kuna mahali amesema kuna watu walitaka kupeleka majina NEC lakini wao hawakuwemo. Tafsiri yake ni kwamba Halima aliamua kufanya uhuni ili kulishinda kundi jingine liliotaka kufanya uhuni. Yani aliwacounter attack wahuni wenzie.

Yani amemaanisha kwamba pamoja na msimamo wa CHADEMA kutopeleka wabunge Viti Maalum, kuna wahuni walitaka kupeleka majina kwa siri. Alipochungulia hiyo orodha akaona hayupo, akaamua kutengeneza orodha yake fasta na kuwahi NEC. Hii ndio tafsiri ya maelezo yake.

Kwa maelezo haya Halima ametusaidia kujua kwamba yeye ndiye aliyepeleka majina NEC pamoja na kwamba amekataa kujibu swali hilo. Lakini pia ametusaidia kujua jinsi alivyo msaliti. Kama aligundua kuna watu wameandaa majina wanataka kuyapeleka NEC na yeye hayupo, kwanini hakutoa taarifa kwa uongozi wa chama?

Kwanini hakuomba kamati kuu kuwachukulia hatua hao wahuni waliotaka kusaliti? Ina maana angekuta jina lake lipo kwenye hiyo orodha angekausha? Hii ndio press ya mtu anayejisifu kukaa CHADEMA miaka 16? What a shame?

Halima anadai wao bado ni wanachama wa CHADEMA. Ni aibu mtu aliyesoma sheria na kukaa CHADEMA miaka 16 lakini hajui katiba ya chama chake. Asome ibara ya 6.5.1(d) atajua yeye na wenzake SI WANACHAMA WA CHADEMA tena kuanzia siku Kamati kuu ilipofanya maamuzi, unless washinde rufaa baraza kuu.

Anasema watakata rufaa baraza kuu warudishiwe uanachama wao, lakini wakati huohuo anasema wao bado ni wanachama wa CHADEMA. Sasa kama bado ni wanachama, huo uanachama wanaotaka warudishiwe na baraza kuu ni upi? Confusion.

Halima akumbuke CHADEMA haina uanachama wa hiyari. Uanachama wa chama chochote cha siasa ni wa masharti. Miongoni mwa masharti ni kuheshimu katiba, kanuni na itikadi ya chama. Sasa Halima na wenzie wamevunja Katiba, wameshindwa kuheshimu maamuzi ya vikao, wamefanya usaliti na bado wanajiita wanachama wa CHADEMA?

Huwezi kukataa kwenda kanisani, umkimbie Padri, ukatae kumtambua Papa, ukatae kushiriki ibada za jumuiya halafu ujiite mkatoliki. Labda Roma Mkatoliki lakini sio Ukatoliki kwa maana ya kanisa takatifu la mitume.

Halima ameulizwa kuhusu Nusrat kuachiwa usiku na kesho yake akaapishwa, akasema aulizwe DPP. Hivi Halima anatuonaje? DPP alijuaje Nusrat ataapishwa November 24 akamwachia November 23? Kwanini hakumwachia November 10? Kwanini asubiri hadi siku moja kabla ya kuapishwa ndipo amwachie? Lazima kuna mawasiliano yalikua yakiendelea kati ya Halima na DPP. Hilo halina ubishi. Asidhani watanzania wote ni wajinga kama yeye.

Halafu anataka kuonesha CHADEMA wamekasirika Nusrat kuachiwa. Si kweli. Hakuna watu waliokua wanataka Nusrat aachiwe kama wafuasi wa CHADEMA. Ni wafuasi hao walikesha mitandaoni kulaani Nusrat na wenzake kushikiliwa kwa uonevu. Ni haohao walikusanya "vijisenti" vyao hadi vikatosha nauli kwenda kumsalimia Nusrat gerezani Singida na baadae Dodoma.

Ni haohao waliojichanga pesa za mawakili wa kuwatetea Nusrat na wenzake. Hivi leo wanawezaje kuchukia Nusrat kuachiwa? Halima aache kupotosha. Watu wanachotaka kujua ni kwanini Nusrat aachiwe usiku wa Novemba 23 then Novemba 24 aapishwe? Hii "considence" sio ya kawaida. Halima anatakiwa kujibu imewezekanaje, sio kusema tumuulize DPP.

Halima anasisitiza kuwa wao bado ni wabunge kupitia CHADEMA. Huku ni kukitukana chama na kujaribu kuonesha kiburi chao hadharani. Kwa lugha ya vijana "wamekivimbia" chama. Yani mmetufukuza lakini tutaendelea kujitambulisha kwa chama chenu, na hamna la kutufanya. Hiki ndicho Halima na wenzake walichofanya leo.

CHADEMA imeshasema HAIJAPELEKA wabunge wa viti maalumu na HAITAPELEKA. Kama Halima na wenzake wanataka kuendelea kuwa wabunge watafute chama kingine cha kujitambulisha nacho lakini si CHADEMA. Period!

Kwa kifupi press ya Halima ameandaliwa na waliomtuma wamemweleza nini cha kusema. Ameambiwa aendelee kusisitiza kuwa wao ni wabunge kupitia CHADEMA ili kuweka uhalali wa kambi ya upinzani bungeni, jambo ambalo litaisaidia serikali isipoteze matrilioni ya wafadhili.

Ndio maana amekwepa hoja zote za msingi badala yake akaishia kusisitiza wao ni wabunge kupitia CHADEMA. Hilo ndilo kubwa aliloambiwa aje kusema. Serikali inataka kusikia wakisema wao ni wabunge kupitia CHADEMA ili kulinda pesa za wafadhili.

Halima akikubali kwamba wamefukuzwa CHADEMA it means watakosa uhalali wa kuunda kambi ya upinzani Bungeni na hivyo serikali itakosa matrilioni ya wafadhili. Kwahiyo Halima ametumwa aseme wao ni wabunge wa CHADEMA na ataendelea kusisitiza hivyo hadi Bunge litakapoisha 2025.

Haya ndio malipo ya Halima kwa CHADEMA. Chama ambacho kimemlea tangu akiwa binti mdogo pale UDSM. Akawa anachukuliwa chuoni na kupelekwa kwenye mikutano ya siasa ili kumjengea uwezo wa public speaking.

Alipomaliza chuo hakutembea na bahasha kutafuta ajira, akapewa ubunge viti maalumu akiwa binti mdogo wa miaka 24 tu. Baada ya kufaidi matunda kwa miaka 15 leo kaamua kuisaidia serikali kulinda pesa za wafadhili kwa kukihujumu chama kilichomlea. Historia ni mwalimu mzuri, ipo siku itamhukumu.
Yaani huyo Halima fukuzeni kabisa keshakengeuka huyo sio yule wa zamani!
 
Hakuna utata pale kila kitu kipo wazi, Halima na wenzake sio wanachama wa CHADEMA na Katiba iko wazi hadi sasa sio Wabunge.

Kilichobaki wanajifariji tu Mfano ni Sofia Simba wa CCM in 2017.

Pamoja na kwamba miaka yote walikuwa wanaenda bungeni japo hawakukubali matokea, lakini utaratibu wa kwenda ulikuwa na baraka za Chama.

Halima na Wanzake waseme nani aliwateua, na je wanawake wengine ndani ya CHADEMA hawana haki ya Kuwakilisha kwenye hizo seat 19.

Kuruhusu uhuni ule ni Kukiaribu chama..let them go, if CCM wanawataka basi Waende huko.
Naunga mkono hoja
 
Siasa ndivyo zilivyo...




Cc: mahondaw

Kweli ni siasa lakini katika hili Halima kashirikiana na wahuni fulani kugushi nyaraka kitu ambacho ni jinai inayonajisi katiba ya inchi pia katiba ya CDM,

Wengine tulitegemea atakuja na wenzie waombe msamaha kumbe kaja na brabra zilezile za kulishwa maneno na hao waliomnunua ya kusema kuwa wao bado ni wanachama wa CDM wakati chama kimeshamfukuza, inajulikana kuwa watalindwa mpaka 2025 na hiyo sio shida kwani CDM wanalijua kwanini itakuwa hivyo na kamwe hawatarudishiwa uanachama wakiwa wabunge wakujichagua wenyewe na hiyo ndio itakuwa mwisho wao wa safari ya kisiasa labda waende CCM
 
Ukiona jirani analia sana kwenye msiba kuliko ndugu wa mfiwa ujue kuna jambo.
 
Back
Top Bottom