Press ya Halima imeongeza maswali mengi kuliko majibu. Amezungumza vitu vingi lakini "theme" ya press yake haieleweki

Kuzungumzia haya mambo unayosema ni kama kuaribu ushahidi na kuongeza matatizo ndani ya chama.

Haya ni mambo ya kuzungumzia kwenye kikao cha kesi sio kwa wana blog au TBC
 
Sijasoma nikamaliza lakini natangaza rasmi kuwa chadema wamefanya ujinga mkubwa na utawagharimu.

Sikubaliani na walichofanya CCM, lakini sikubaliani zaidi walichoamua kukifanya chadema.Walikuwa na muda wa kufanya maamuzi ya busara.
Rule of law should be a cornerstone of our nation! Even the persons that have the power to be above the law by instruments, should observe the existence of such instruments as the law itself !

Wenye mamlaka wasitumie mapungufu ya kisheria yanayotoa mianya ya ubabe kuwa wababe. Huo ni ushamba uliopitiliza.
 
Nadhani watu wengi hawajamuelewa Mdee;

Kuna mambo hajataka kuweka Public kwa sasa.

Anasubiri muda muafaka ufike.

Na muda huo ni mpaka hiyo process ya vikao vya ndani ikifeli ataruka hewani.

Kamheshimu Sana Mwenyekiti wake na katoa nafasi ya kupokelewa tena.
 
Na, Malisa GJ

Press ya Halima imeongeza maswali mengi kuliko majibu. Amezungumza vitu vingi lakini "theme" ya press yake haieleweki. Hata yeye ukimuuliza "theme" ya Press yako ilikua nini hawezi kusema.

Ukiachana sura zao zenye mashaka na majuto, leo vyombo vyote vya habari vya serikali na mamluki wake vimeshiriki press hiyo. Kuanzia TBC, DailyNews, Uhuru hadi Tanzanite ya Musiba. Hivi hadi hapo hamjajua nani wapo nyuma yao? Uliwahi kuona TBC au Tanzanite kwenye press ya Mbowe?

Hata hivyo watu walitegemea aeleze ni nani aliyepeleka majina NEC? Kwanini walikiuka maagizo ya kamati kuu? Yalikua maelekezo ya nani? Kwanini walienda kujiapisha? Na kwanini alisema uongo kuwa Mwenyekiti alimpa baraka?

Lakini Halima kakwepa maswali hayo katika namna ya kupanic. Amesema hawezi kujibu nani alipeleka majina wala kwanini walienda kuapa kwa sababu eti watakata rufaa baraza kuu. Kwahiyo majibu watayatoa huko baraza kuu na sio kwenye press. Sasa kama wamekata rufaa baraza kuu hii press wamefanya ya nini? Non sense.

Pamoja na kuongea kwa kujichanganya sana, kuna mahali amesema kuna watu walitaka kupeleka majina NEC lakini wao hawakuwemo. Tafsiri yake ni kwamba Halima aliamua kufanya uhuni ili kulishinda kundi jingine liliotaka kufanya uhuni. Yani aliwacounter attack wahuni wenzie.

Yani amemaanisha kwamba pamoja na msimamo wa Chadema kutopeleka wabunge viti maalumu, kuna wahuni walitaka kupeleka majina kwa siri. Alipochungulia hiyo orodha akaona hayupo, akaamua kutengeneza orodha yake fasta na kuwahi NEC. Hii ndio tafsiri ya maelezo yake.

Kwa maelezo haya Halima ametusaidia kujua kwamba yeye ndiye aliyepeleka majina NEC pamoja na kwamba amekataa kujibu swali hilo. Lakini pia ametusaidia kujua jinsi alivyo msaliti. Kama aligundua kuna watu wameandaa majina wanataka kuyapeleka NEC na yeye hayupo, kwanini hakutoa taarifa kwa uongozi wa chama?

Kwanini hakuomba kamati kuu kuwachukulia hatua hao wahuni waliotaka kusaliti? Ina maana angekuta jina lake lipo kwenye hiyo orodha angekausha? Hii ndio press ya mtu anayejisifu kukaa Chadema miaka 16? What a shame?

Halima anadai wao bado ni wanachama wa Chadema. Ni aibu mtu aliyesoma sheria na kukaa Chadema miaka 16 lakini hajui katiba ya chama chake. Asome ibara ya 6.5.1(d) atajua yeye na wenzake SI WANACHAMA WA CHADEMA tena kuanzia siku Kamati kuu ilipofanya maamuzi, unless washinde rufaa baraza kuu.

Anasema watakata rufaa baraza kuu warudishiwe uanachama wao, lakini wakati huohuo anasema wao bado ni wanachama wa Chadema. Sasa kama bado ni wanachama, huo uanachama wanaotaka warudishiwe na baraza kuu ni upi? Confusion.!

Halima akumbuke Chadema haina uanachama wa hiyari. Uanachama wa chama chochote cha siasa ni wa masharti. Miongoni mwa masharti ni kuheshimu katiba, kanuni na itikadi ya chama. Sasa Halima na wenzie wamevunja Katiba, wameshindwa kuheshimu maamuzi ya vikao, wamefanya usaliti na bado wanajiita wanachama wa Chadema?

Huwezi kukataa kwenda kanisani, umkimbie Padri, ukatae kumtambua Papa, ukatae kushiriki ibada za jumuiya halafu ujiite mkatoliki. Labda Roma Mkatoliki lakini sio Ukatoliki kwa maana ya kanisa takatifu la mitume.

Halima ameulizwa kuhusu Nusrat kuachiwa usiku na kesho yake akaapishwa, akasema aulizwe DPP. Hivi Halima anatuonaje? DPP alijuaje Nusrat ataapishwa November 24 akamwachia November 23? Kwanini hakumwachia November 10? Kwanini asubiri hadi siku moja kabla ya kuapishwa ndipo amwachie? Lazima kuna mawasiliano yalikua yakiendelea kati ya Halima na DPP. Hilo halina ubishi. Asidhani watanzania wote ni wajinga kama yeye.

Halafu anataka kuonesha Chadema wamekasirika Nusrat kuachiwa. Si kweli. Hakuna watu waliokua wanataka Nusrat aachiwe kama wafuasi wa Chadema. Ni wafuasi hao walikesha mitandaoni kulaani Nusrat na wenzake kushikiliwa kwa uonevu. Ni haohao walikusanya "vijisenti" vyao hadi vikatosha nauli kwenda kumsalimia Nusrat gerezani Singida na baadae Dodoma.

Ni haohao waliojichanga pesa za mawakili wa kuwatetea Nusrat na wenzake. Hivi leo wanawezaje kuchukia Nusrat kuachiwa? Halima aache kupotosha. Watu wanachotaka kujua ni kwanini Nusrat aachiwe usiku wa Novemba 23 then Novemba 24 aapishwe? Hii "considence" sio ya kawaida. Halima anatakiwa kujibu imewezekanaje, sio kusema tumuulize DPP.

Halima anasisitiza kuwa wao bado ni wabunge kupitia Chadema. Huku ni kukitukana chama na kujaribu kuonesha kiburi chao hadharani. Kwa lugha ya vijana "wamekivimbia" chama. Yani mmetufukuza lakini tutaendelea kujitambulisha kwa chama chenu, na hamna la kutufanya. Hiki ndicho Halima na wenzake walichofanya leo.

Chadema imeshasema HAIJAPELEKA wabunge wa viti maalumu na HAITAPELEKA. Kama Halima na wenzake wanataka kuendelea kuwa wabunge watafute chama kingine cha kujitambulisha nacho lakini si Chadema. Period.!

Kwa kifupi press ya Halima ameandaliwa na waliomtuma wamemweleza nini cha kusema. Ameambiwa aendelee kusisitiza kuwa wao ni wabunge kupitia Chadema ili kuweka uhalali wa kambi ya upinzani bungeni, jambo ambalo litaisaidia serikali isipoteze matrilioni ya wafadhili.

Ndio maana amekwepa hoja zote za msingi badala yake akaishia kusisitiza wao ni wabunge kupitia Chadema. Hilo ndilo kubwa aliloambiwa aje kusema. Serikali inataka kusikia wakisema wao ni wabunge kupitia Chadema ili kulinda pesa za wafadhili.

Halima akikubali kwamba wamefukuzwa Chadema it means watakosa uhalali wa kuunda kambi ya upinzani bungeni na hivyo serikali itakosa matrilioni ya wafadhili. Kwahiyo Halima ametumwa aseme wao ni wabunge wa Chadema na ataendelea kusisitiza hivyo hadi bunge litakapoisha 2025.

Haya ndio malipo ya Halima kwa Chadema. Chama ambacho kimemlea tangu akiwa binti mdogo pale UDSM. Akawa anachukuliwa chuoni na kupelekwa kwenye mikutano ya siasa ili kumjengea uwezo wa public speaking.

Alipomaliza chuo hakutembea na bahasha kutafuta ajira, akapewa ubunge viti maalumu akiwa binti mdogo wa miaka 24 tu. Baada ya kufaidi matunda kwa miaka 15 leo kaamua kuisaidia serikali kulinda pesa za wafadhili kwa kukihujumu chama kilichomlea. Historia ni mwalimu mzuri, ipo siku itamhukumu.!
We naye Umeandika hisia zako nyiiingi, itisha tu press
 
Hao Hao Wanaondoka, Wanaondoka
Safari Imeiva Kwenda Ccm
Ngoma Ikilia Sana Mwishowe Hupasuka!!
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu


😁😂😀😅😃😃😁😂🤣😅😄😃😁😂😂🤣🤣😃😄😅
Sikio Halipiti Kichwa
Ziwa La Mama Ni Tamu Hata Liwe La Mbwa
Lingine Haliishi Hamu .
Unasema kweli
 
Wakuu naomba kujuzwa hivi anayeulizwa na hao wafadhiri kuwa je bungeni kwenu Kuna kambi ya upinzani ni spika wa bunge au Nec au chama husika cha upinzani? Mwenye kuelewa anijuze sababu Ndugai na serikali imeshupalia hili jambo isivyo kawaida inaonyesha Kuna mambo watayakosa isipokuwepo kambi rasmi ya upinzani, kwann mungufuli amng'ang'anie adui asiyempenda namna hii? Huu urafiki wa mashaka nahisi anataka awatumieawatumie tu
 


Pitia hili bandiko la NEC litakusaidia
Kama kwa ccm iliwezekana kumfurusha Sophia Simba kote kote, kigugumizi cha nini kwa Halima na wenzake?!
 
Tatizo la CHADEMA kila mmoja ana sharubu . Jambo likitokea kidogo tu kila mmoja anageuka
Msemaji wa chama. Hapo ndio mnatuyumbisha vichwa sisi wananchi 😓😓😓
 
Nadhani watu wengi hawajamuelewa Mdee;

Kuna mambo hajataka kuweka Public kwa sasa.

Anasubiri muda muafaka ufike.

Na muda huo ni mpaka hiyo process ya vikao vya ndani ikifeli ataruka hewani.

Kamheshimu Sana Mwenyekiti wake na katoa nafasi ya kupokelewa tena.
Apokelewe huko ccm maana bashir tayari ameshawaita wanawake wa shoka
 
Halima ameonyesha utovu mkubwa kwa viongozi na chadema kwa ujumla. anatafuta symphathy ambayo hawezi kuipata. hana majibu kwa maswali ya msingi aliyoulizwa. movie anayocheza ni ya kipumbavu kwa kuwa waliomfundisha wamemuahidi kumsaidia hiyo movie yake hata kwa kuvunja sheria. ngoja tuone mwisho wake.
 
Huyu Halima nadhan alifikia kiwango akaona kama yeye ana hisa flani kwenye chama ndio akashiriki huu ujinga lakini kumbe si chochote., nafurahi kwamba Chadema wako imara sana kwenye utawala kuliko chama chochote cha upinzani Tz.,

Na huko baraza kuu huyu halima akiwekwa mtu kati naamini atalia machozi., na sidhan kama ataruhusu hoja za yeye kufanya ujinga ziendelee kujadiliwa lazima atajuta sana.,

Tanzania lazima hivi vyama vya upinzani ifikie mahali kuwa na uongoz madhubuti kukomesha hii habari ya senior leaders kuwa very cheep.,
 
Back
Top Bottom