Press realese: Basata yafungia miss tourism

GRANDPUBA

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
572
1,000
Ni hatua nzuri kwa sababu zilizoelezwa, nawapongeza, lakini sanaa katika nchi hii siyo urembo tu, Baraza la Sanaa Tanzania sasa ligeukie suala la zima la uaandaji na utoaji wa tuzo za music hapa nchini, mpaka sasa kibali kimetolewa kwa Kampuni ya bia ya Kilimanjaro tu, why only Kilimanjaro? Kuna taarifa kwamba kuna kampuni zenye uwezo zimejitokeza kuomba kibali cha kuandaa tuzo hizi lakini hazijapewa kibali. Na hakuna sababu za kimantiki zilizotolewa na Basata za kutoruhusu kampuni hizo kuandaa hizo tuzo. Ninavyoona tunahitaji kampuni zaidi moja katika utoaji wa tuzo hizi kama ilivyo katika nchi nyingine ambazo "music industry" yao inaendelea kukua kama hapa kwetu. Angalau tupate uzoefu mwingine wa namna "categories" za wanaowania tuzo hizo zitakavyopangwa na waandaaji wengine, badala ya category moja unamweka Hadija Kopa, LadyJay Dee sijui na Vanessa Mdee, maana yake hapa unataka tumpigie kura mwimbaji bora wa kike kupitia mitindo mitatu tofauti, taarabu, afro-pop sijui bongoflava na Rn'B. Mimi huwa inanichanganya.
 

Attachments

  • MISS-UTALII.jpg
    File size
    165.6 KB
    Views
    223

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom