Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,829
Rais Samia akiwa nchini Oman, ameshiriki kongamano lililojumuisha wafanyabiashara wa Oman na Tanzania leo Julai 13, 2022.
Rais Samia amesema tangu achukue madaraka Serikali yake inaongoza pekee na biashara zinafanywa na sekta Binafsi. Rais Samia amesisitiza na kusema amemaanisha aliposema hakuna biashara zaidi kwa Serikali.
Rais Samia kasema wao kama Serikali wanatengeneza mazingira bora kwa sekta binafsi iwe wa ndani au nje kukua na kufanya biashara Tanzania.
Kwenye utawala wa awamu ya tano Tanzania ilishuhudia ufufuaji wa mashirika na kufanyiwa uwekezaji mkubwa ili kufanya biashara sambamba na sekta binafsi kama TTCL, ATCL na TBA.