President Samia: No more Business to the Government, Private sector will do the Business

Rais Samia akiwa nchini Oman, ameshiriki kongamano lililojumuisha wafanyabiashara wa Oman na Tanzania leo Julai 13, 2022.

Rais Samia amesema tangu achukue madaraka Serikali yake inaongoza pekee na biashara zinafanywa na sekta Binafsi. Rais Samia amesisitiza na kusema amemaanisha aliposema hakuna biashara zaidi kwa Serikali.

Rais Samia kasema wao kama Serikali wanatengeneza mazingira bora kwa sekta binafsi iwe wa ndani au nje kukua na kufanya biashara Tanzania.

Kwenye utawala wa awamu ya tano Tanzania ilishuhudia ufufuaji wa mashirika na kufanyiwa uwekezaji mkubwa ili kufanya biashara sambamba na sekta binafsi kama TTCL, ATCL na TBA.

Rais ana hoja. Lakini hapa bongo kweli kuna private sekta yenye uwezo wa kugharamia miradi mikubwa ya kiuchumi au tuendelee na mfumo wa PPP. Wachumi wataweza kutoa ufafanua katika hili.
 
Katika nchi zenye uchumi unaokua, serikali hazifanyi biashara! Biashara ni hodhi ya private sector, hawa ndio wenye ujasiri na umahiri wa kubeba risk na mikikimikiki ya kufanya biashara! Kazi ya serikali ni regulation; mind you: sio over-regulation au micro-management! Utaratibu wa serikali kufanya biashara ulikuwa ni usanii wa magufuli kujifanya anamuenzi baba wa taifa ili kuturudisha kwenye mfumo Command economy ya kijamaa na kisoshalisti wakati kumbe hiyo ilikuwa ni pazia tu la kufanya ufisadi na uovu wa kutisha dhidi ya raslimali za taifa na maisha ya wananchi!
Good riddance magufuli!
Kwani haiwezekani serikali ikawa na makampuni yake kwenye baadhi ya sekta sambamba na makampuni binafsi ili iwe rahisi kwao kufanya regulation kwani itakuwa inajua kinachoendelea.
 
Tuanze na ATCL,TTCL,STAMICO,TANESCO na mashirika mengine ya umma yanayofanya biashara yavunjwe mara moja.

Serikali inapaswa kuwa msimamizi na kuruhusu uwepo wa sera rafiki kwa private sector ili kuruhusu ushindani...na kuleta unafuu wa biashara nchini.

#MaendeleoHayanaChama
TANESCO haifanyi biashara inatoa huduma ndiyo maana bei ya umeme unayolipa ni ndogo kuliko bei halisi
 
Back
Top Bottom