President daughter

President daughter

endrizzy

Senior Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
186
Reaction score
137
MTUNZI: ERICK NZIKU
STORY: PRESIDENT DAUGHTER
SEHEMU YA KWANZA


Naitwa James david Massawe ni mzaliwa wa Same, Kilimanjaro,i live with my both parrents na nna wadogo wawili john na jenny. Maisha katika familia yangu ni magumu sana ndo maana inanibidi nifanye kazi huku nasoma katika chuo cha ualimu Moshi, na kuuza mboga mgoga katika Soko kuu la same na stori inaanzia hapa.

Siku moja nilikuwa natoka kwenye biashara yangu mida ya usiku nilikuwa nimechoka sana ukizingatia ilikuwa jumamosi so sikwenda shule nilikuwa sokoni toka asubui, wakati nikiwa natembea ghafla nashaa gari limesimama mbele yangu na watu wenye suti nyeusi wakiwa wamenyoa vipara wakashuka na kunichukua kinguvu na kunipeleka nisipokujua,,, Kufumbua macho nilikuwa katika bonge moja la jumba mbele yangu akiwa amesimama Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania Saido mjuni, kwa kweli nilipigwa na butwaa pasi kujua nini kinaendelea.

Mwema: kijana umeletwa hapa kwa dhumuni moja tu, tumekuwa tukikufuatilia toka mda mrefu tunajua kuwa ni wewe ndiye uliye hack system yetu mara mbili so tunakupa nafasi ya kujiunga na sisi ili siri zetu zisivuje kama hutaki hatuna jinsi bali ni kukuua tu,
ME; Naogopa sana kifo katika misha yangu so sikuwa option zaidi ya kusema ndio.

Mjuni: mission yako ya kwanza itakuwa kwenda Usa utafute mahali mtoto wa Raisi alipo umlete Tanzania akiwa Salama bin Salmin maana hali ni mbaya sana tumepata onyo kwamba kuna watu wa vyama vya upinzani wakishirikiana na Marekani wanataka kumuua.tumekuandalia usafiri na passport yako iko tayari nenda nyumbani kesho njoo mapema kwaa jili ya Safari yako. Na kumbuka usimwambie mtu yoyote hata familia yako kuhusu mission hii kama unaipenda familia yako.Kumbuka hii ni mission kubwa mabayo kila askari anaitaka lakini nimekuchagua na kukuamini wewe.

ME: Ndio, sitomuambia mtu. Wakanirudisha hadi nyumbani niwakuta familia yangu wote wakiwa katika mlo wa usiku bila kusita na mimi nikajongea moyoni nilikuwa na uzuni sana sababu ilikuwa siku ya mwisho mimi na familia yangu tunakaa pamoja...nikaenda zangu kulala kichwani nikifikiria safari ya kesho... Yap..safari imewiva nipo kwa mkuu akinipa maelekezo mengine Mwema: jina anaitwa Aisha Mahmood anakaa west Corolado asije akajua wewe ni askari sababu apendi kuchungwa na hapendi watu wajue ye ni mtoto wa Raisi , una uhakika utaweza kazi?

Me: nina uhakika ntaweza mkuu
Nilifika Usa kesho yake na kuanza kazi yangu ya kumsaka mtoto wa Raisi, Kitu ambacho Mkuu wa jeshi la Tanzalia alikuwa afahamu kuwa mimi nilikuwa ni mfuasi wa chama cha upinzani CHADEME na nilipopata nafasi ile moja kwa moja niliwataarifu viongozi wangu nao wakaniambia niende kwa dhumuni moja tu la kumuua mtoto wa raisi....

Ilikuwa kazi ngumu sana kwangu sababu nilitakiwa nimlete Tanzalia at the same time nimuue, katika tembea tembea zangu akatokea jamaa mbele yangu na kunipora begi wakati nataka nimkimbize akatokea msichana mmoja alimpiga yule jamaa kwa pigo ambalo sijawai kuliona duniani nilishangaa sana...
msichana: here is your bag,

Me: Thank you,what is your name miss? Msichana: Aisha...and you? Me:James......Mara simu yangu ikaita kuangalia ni mkuu akitaka kujua kama nimefika nikwambia nimefika na kuniambia ananitumia picha sasa hivi nisubilie kidogo tu.......

Aisha: ah kumbe unaongea kiswahili unatokea tanzalia nini?
ME: ndio mzaliwa wa moshi na nimekulia huku huko Simu yangu tena ikalia kuangalia ni meseji ya picha kuangalia ile picha i couldnt believe my eyes coz msichana aliyesimama mbele yangu ndiye alikuwa mtoto wa Raisi.......................






SEHEMU YA PILI
PRESIDENT DAUGHTER


Tanzalia hali sio nzuri homa ya uchaguzi imetawala, kampeni zilikuwa zikiendelea maeneo mbali mbali. raisi aliyemaliza muda wake MAHMOOD alikuwa akigombea tena kwa miaka mingine mitano.kila mtanzalia alikuwa na hamu ya kufahamu kitakachotokea lakini huku nyuma ya pazia kulikuwa na mchezo mchafu unafanyika,chama cha CP walikuwa wanafikiria ni jinsi gani ya kuiba kura ili waweze kurudi tena madarakani huku chademe wakiwaza jinsi ya kuanzisha vita katika hardhi ya Tanzalia.
Kuangalia picha James alipagawa baada ya kuona mtu aliyetumwa aje kumlinda na kumrudisha salama Tanzalia na upande mwingine kumuua ndie aliye msaidia na alikuwa amesimama mbele yake, Baada ya kutambulishana James alimuaga Aisha na kwa kuwa James Alikuwa mgeni alimuomba Aisha kesho Amuonyeshe jiji Aisha bila kinyongo akamkubalia.Wakaagana lakini James hakuondoka bali alikuwa anamfuatilia nyuma nyuma ili apajue anapoishi , Baada ya mwendo kidogo James alimuona Aisha akiingia kwenye nyumba yake anayoishi . alikaa hadi asubui akimlinda mtoto wa Raisi**Asubui kulivyoucha JAmes alishtushwa na mlio wa simu, alikuwa ni mwakilishi wa chama cha CHADEME kwa upande wa marekani akimwambia aende kuchukua vitu ambavyo atatumia kumuua mtoto wa Raisi bila kusita James alienda huko akapewa Bastola moja yenye silencer pia simu yenye secure line ili wawasiliane....ilikuwa kama saa sita mchana kule America naam ulikuwa ni muda wa ahadi ya James na Aisha, James alikuwa ameshafika mapema akawa akimsubili mtoto wa Raisi alikaa sana pasi na dalili ya kumuona mtoto wa raisi , alikuwa amechoka kusubili kwa hiyo akaona bora aondoke zake akiwa katika harakati za kuondoa anakutana uso kwa uso na Aisha akiwa amependeza akitabasamu kwa mbali moyo wa James ghafla ulirudi kwenye hali ya kawaida huzuni ilipotea na akaanza kutoa tabasamu lake la kuwa kamatia wasichana.
Aisha::samahani nimechelewa..
James:usijali...
Aisha: ok, tuendelee Na mambo mengine
James kichwani akiwa na mawazo ya jinsi ya kumuua mtoto wa raisi hana wasi wasi anatabasamu tu.Aisha alianza kazi ya kumutembeza Colorado na walizunguka sana, Aisha akamwambia James amsindikize kwake jamaa akaona hii ndo time ya kummaliza Aisha.Kumbuka james aliambiwa asipomuua Aisha wazazi wake na familia yake nzima itauliwa..wakiwa wamechoka wakawa wanaelekea nyumbani kwa AISHA njiani waliongea mengi sana wakipeana vichekesho vya hapa na pale.walipofika aisha alifungua mlango na wakaingia ndani walipoingia tu James akaomba kwenda chooni kufika chooni akaandaa Bastola yake tayari kwa kumaliza kazi ,akarudi akawa amekaa karibu na Aisha , Aisha alikuwa tayari ameshaanza kuvutiwa na james akiwa amelegeza macho na kumshika kifuani james akamwambia james I LOVE you..ilikuwa ni kama katoka usingizini james alishtuka na kusema WHat?Unanipenda? Kumbuka James katumwa amuue.........heheheheh kazi ipo. itaendelea next time.je, James atamuua Aisha????




SEHEMU YA TATU

PRESIDENT DAUGHTER.

Ilikuwa ni ndoto kwake hakuamini kama angeweza kupendwa na mtoto wa raisi alishtushwa na mwanga mwekundu kwenye paji la uso wa Aisha, bila kushangaa alimsukuma Aisha na kwenda nae chini, Aisha alishtushwa na mlio wa bunduki iliyomkosa kwa haraka James alianza kufuatilia kule risasi ilipotokea lakini hakuona mtu alibaki anashangaa asijue ni nani mwingine anayetaka kumuua mtoto wa raisi?

huku kwa mwakilishi wa chama cha CHADEME alipata order kutoka Tanzalia kuwa amuue yule Mtoto wa raisi lakini kesi yote apewe James.kwa iyo akamuajiri mtu aende akafanye kazi...



Aisha alishikwa na kiwewe pasi kujua ni nani anayetaka kumuua anajua kuwa baba yake ana maadui wengi lakini si kufikia hatua ya kumuua.Aisha aka msichana wa kazi alikuwa na nyumba yake nyingine iliyokuwa karibu na bahari hivo akamwambia James waondoke wote kwani hali ishakuwa mbaya. Wakaondoka kwa kasi ya ajabu na gari ya aisha aina ya Hammer, walipofika wakaingia ndani haraka ili waweze kutafakari nini kimetokea kabla hawajaendelea Aisha anamwambia waende chini kwani nyumba yake ilijengwa na kuwekwa sehemu ya chini kwaajili ya kuhifadhi vitu vyake,walipofika chini huko James alipigwa na butwaa kukuta mtoto Aisha anamiliki silaha za aina mbali mbali

kabla hata hawajatoka chini wanashtushwa na mshindo mkubwa wa bomu Naam nyumba ya aisha ilikuwa ikiteketea kwa moto baada ya kupigwa bomu . Bahati yao walikuwa chini ya Ardhi la sivyo wangekwenda na maji , wanatumia escape rout kutoka kwenye ile nyumba na ile rout ilikuwa inaishia bahari wanafika baharini wakakutana na boti ya aisha wakapanda kuelekea Los Angels ili tuingie katika nchi nyingine ya mexico kwani hali ishakuwa mbaya.



kufika border tu tukashangaa kuona Askari wengi wamejaa wakifanya ukaguzi wa nguvu kwa anayeingia na kutoka tukajua tu kuwa wanatusubilia sisi watukamate, tukakaa pale kusubili usiku hali iwe sawa alafu tukavuke..Hapo hapo ikabidi Aisha awasiliane na baba yake (Raisi wa Tanzalia ) aweze kumsaidia Baba yake akamuaidi tuingie Mexico atatuma ndege ije kutuchukua.Nkawasiliana na mkuu wa polisi nae akanipa jibu lile lile..kumaliza kuongea tu nkapigiwa simu na viongozi wa CHADEME kutoka Tanzalia wakitaka kujua nimefikia wapi , lakini kabla sijajibu nkashtushwa na sauti ya mdogo Jane wangu ikiita kaka nsaidie wanataka kuniua. Dah ilikuwa ni kama kuniongezea mzigo mwingine wakati niliokuwa nao ni mzito siiuwezi, Kiongozi wa chademe akaendela akisema " umeskia hiyo sauti?

nadhani umeitambua sasa ukitaka kumuona mdogo wako fanya ulichotumwa na urudi Tanzalia la sivyo utakuta maiti pia hatutaishia kwa mdogo wako tutamaliza familia nzima.

Turudi nyuma kidogo.

Kabla sijaamua kusoma ualimu nilikuwa mwanajeshi kwani baada ya kumaliza form four na kupata division four sikuwa na zaidi ya kuingia Jeshini, Nilikuwa jeshi la anga, pia nilipata bahati ya kusoma kwa mwaka mmoja course ya mawasiliano(IT) tulipelekwa na jeshi nchini India.



Machozi yalikuwa yananilenga lenga lakini nikajikaza ili Aisha asijue kinachoendelea , nguvu za kumuua Aisha nilikuwa sina tena nilikuwa nimejazwa nguvu za kutaka kumsaidia mpaka afike Tanzalia lakini mdogo nampenda sana kuliko maisha yangu nikabaki sina choice zaidi ya kusubili na kuona kitakachotokea mbele..

tulikaa sana lile eneo pale kwani tulikuwa tumefika mapema sana, ilipofika saa moja jioni tukaanza michakato ya kuvuka ilie border kuelekea MEXICO...
 
Samahani kwa nia njema tu umeeleza historia yako kuwa unasoma chuo cha ualimu na kuuza mboga mboga mara unakamatwa na kuhusishwa na kazi kubwa ambayo mafunzo yake hujabainisha katika hadithi yako tafadhali niweke sawa hapo napata tabu kwenda uzuri na hadithi yako.
 
Mara kuhack system mara ualimu mara chademe mara kutumwa marekani.. story haina ushirikiano asee jipange umejifunzia wapi hacking.? hacker hawez kutumwa kwenye mission hacker anaassist tu kutrack watu.. huangalii hata movie..!!!!
 
Samahani kwa nia njema tu umeeleza historia yako kuwa unasoma chuo cha ualimu na kuuza mboga mboga mara unakamatwa na kuhusishwa na kazi kubwa ambayo mafunzo yake hujabainisha katika hadithi yako tafadhali niweke sawa hapo napata tabu kwenda uzuri na hadithi yako.
alafu ndo kwanza sehemu ya kwanza soma ya pili na tatu utajua then hutouliza maswali
 
Mara kuhack system mara ualimu mara chademe mara kutumwa marekani.. story haina ushirikiano asee jipange umejifunzia wapi hacking.? hacker hawez kutumwa kwenye mission hacker anaassist tu kutrack watu.. huangalii hata movie..!!!!
ikifika sehem ya pili utajua wap kajifunza pamoja na kusomea ualimu
 
Mara kuhack system mara ualimu mara chademe mara kutumwa marekani.. story haina ushirikiano asee jipange umejifunzia wapi hacking.? hacker hawez kutumwa kwenye mission hacker anaassist tu kutrack watu.. huangalii hata movie..!!!!
mission yake ilikuwa ni kumlocate na kumrudisha Tanzania
 
Back
Top Bottom