Huwezi kuoperate airbus kwa nauli ya 32k kwenda Mwanza!!!
I guess hiyo 32k ni offer ya ticket chache lets say 10% ya tickets for every flight, Marketing strategy
Tatizo tulilonalo Tanzania ni ukosefu wa waandishi wazuri wa mambo ya biashara. Ukisoma comments za watu wengi hapa ni wazi bado hawaelewi business model ya FastJet. Hii ni low-carrier/no-frills.
Kwa wale wanaolinganisha FastJet na Community air- sio sahihi kabisa. Anthony Diallo didn't do his homework properly kabla ya kuanza hiyo biashara and most crucially, hakuwa na experience kwenye aviation industry.
Founder wa FastJest - Sir Stelios- ni guru wa hizi low carrier. Yeye mwenyewe (Sir Stelios) ameenda shule - ya kueleweka. He is very good kwenye Finance na ana experience sana kwenye aviation industry. Tukumbuke huyu bwana ndiye alianzisha Easyjet. Sasa hivi Easyjest wana wanaenda zaidi ya nchi 30! Kwa mwaka mmoja tu EasyJet anasafirisha si chini ya 50 million passengers!
Pia Easyjet wako listed kwenye London Stock Exchange. Hana magumashi huyu bwana. FastJet itatumia business model hiyo hiyo ya EasyJet - no frills. Hakuna mambo ya juice -juice na vimikate au sijui vikorosho vya bure, kama unataka kula unalipa! Na pia ana very 'lean' administration. Wateja wanakuwa encouraged ku-book flight kupitia website au hata simu. Hii inapunguza gharama za uendeshaji - ambazo mwisho wa siku zinaishia kwa mteja!
Jambo jingine, FastJet kama ilivyo EasyJet, mteja anapata unafuu kwenye bei kama uta-book mapema. Kuna peak & off-peak prices. Mfano mtu anayesafiri saa 4 asubuhi anaweza kulipa zaidi kuliko anayesafiri saa 12 jioni, hata kama watasafiri siku hiyo hiyo. Uzuri ukifanya booking kupitia website yao unapata options nyingi (including bei/time dates). Pengine hii itatusaidia sisi Watanzania kuwa more organised - kupanga ratiba mapema badala ya kuishi kwa mtindo wa zima moto!
Kwa wale wanaosubiri FastJet wafe kifo cha Community air, waandike maamuvu. Kwanza tuone jinsi huyu Sir Stelios alivyoingia kwenye soko. Ameanza East Africa - specifically Tanzania - kwa kununua shares zote za 540. That means amenunua routes/customer base yote ya 540! (market entry). Badala ya kuweka base Nairobi - yeye kaja moja kwa moja Dar. why? Kwa sababu Bongo ndio kuna UKAME zaidi wa usafiri wa anga. Kenya wana Kenya Airways. Hapa bongo ni Prescion na mdundiko wake wa delays!
Kenya Airways waliposikia huyu FastJest inakuja (na wanajua fujo za Sir Stelios) walianza low-cost service - haraka. Leseni ya low-cost ilitoka kama miezi 2 hivi iliyopita. Hawakukaa chini na kuongea kama 'Tomaso', badala yake walianza kujiandaa kwa mazingira ya ushindani.
Jambo jingine, FastJet inaonekana ku-concentrate kwenye routes za kwenye natural resources. Mipango iliyopo ni kwamba, ataanza na Tanzania, Kenya & Ugana, lakini baadae ataongeza routes Angola, Ghana etc. Sijui Community air alikuwa na mipango gani?
How about Air Tanzania.
Sasa hivi Tanzania imeshaingia kwenye ukurasa wa nchi zenye gas, uranium na madini mengine. Big boys wako mjini. Serikali kuendelea kufanya biashara itatugharimu. Air Tanzania bado inaendeshwa na wanasiasa! Mkurugenzi anateuliwa na rais, tena bila interview yoyote! So far hakuna la maana linaloendelea na ujio wa wazee wa kazi kama FastJet unahitaji new thinking toka serikalini.
Kwa mtazamo wangu, Air Tanzania ivunjwe (kabisa), na kuundwa shirika jipya. Serikali iwe ni shareholder lakini wawepo wanahisa wengine. Mambo ya presidential appintee yaishe. Mkurugenzi/wakurugenzi wapatikane kupitia njia za ushindani. Tofauti na hapo, Dr Mwakyembe afunge office za ATCL, na aelekeze hela kuboresha viwanja vya ndege ili wazee wa kazi warushe ndege, na kama kuna change aboreshe usafiri wa Train.
And to the old bag - Precision air
Your time is up, review your business model -haraka. Bad mouthing is not a business model! Mtindo wa kuacha wateja airport wakipiga miayo siku nzima ukome. Even as we speak fungua websites za Precision na FastJet and you will see the difference! FastJet, naweza ku-book flight sasa hivi na nikapata jibu including muda wa kulipia. Lakini Precision website, hata kufunguka ni shida tupu!
Karibuni sana FastJet.