Precision Air mmezidi

Precision Air mmezidi

Ndege zote zinazonunuliwa na PW ni mpya- brand new!
Amini usiamini PW wana routes nyingi na hakuna ndege inayokuwa on ground kusubiria itakayopata hitilafu.
Kila ndege mpya inayokuja inapangiwa route yake, na si rahisi kuvunja route ya kwenye ratiba.
Hii ndiyo shida ya kuwa na ukame wa mashirika ya ndege nchini, lau yangekuwepo PW wangekodi ingine ikapiga route husika.
Nawasifu sana PW so far kwa kuwa National Carrier, na wanaiepusha nchi na aibu ya mwaka.
Labda niwaulize wote mnaolaumu na kubeza kazi iliyotukuka ya PW kuwa ni kipi bora, kurusha ndege yenye snag, au kuipeleka kwanza hangar ikarekebishwe hata kama matengenezo yatakula masaa 6? Naomba jibu.

Mnazifahamu vizuri ajali za ndege, na jinsi zisivyo na Mswalie Mtume katika kuchinja abiria, halafu leo mnambeza rubani anayetoa taarifa kuwa ndege ina snag! kwa watu waliostaarabika walitakiwa watoe compliment kwa PW kwa kuzingatia kanuni za Usalama wa ndege na wasafiri.

Nawapongeza sana PW kwa umakini wenu, ndiyo maana hadi leo hamjakumbwa na fatal au catastrophi accident. Huu ni uzingatiaji wa juu sana wa kanuni za usalama.

Ki-aviation inasemekana kuwa 85% ya ajali za ndege husababishwa kutozingatia kanuni za usalama. Masuala kama mchafuko wa hali ya hewa na mis-communication yanachangia percent ndogo iliyobakia.

Ndege katika hali ya kawaida ina uwezo wa juu sana wa kujiepushia ajali yenyewe inapokuwa angani. Ndege inaweza kudevelop tatizo kubwa ikiwa angani, lakini ikatumia spare-capacity yake kukata mawingu hadi mwisho wa route yake, then ikishatua haitatoa go-ahead kwa rubani kuiondoa tena hadi irekebishwe.

Sasa system za safety zenye akili namna hiyo tunazibeza, tunataka nini?

Ile kawaida yetu ya kushinda tunalaumu tusiiingize kwenye masuala ya technical, na hasa maeneo nyeti kama usafiri wa anga.

Angani hakuna parking au stendi meen.

Ahsante Mkuu!!
 
huwa najiuliza kwanini kila siku wao tu ndio mabingwa wa kucancel flight zao?
Je tuamini kuwa ni shibe?

Ila hawa jamaa kama ni ndege wanazo nyingi sasa inakuwaje wana cancel flight kwa muda mrefu sana hivyo wakati kila siku twasikia wameagiza ndege mpya kutoka France

Je tuamini kuwa hizo ndege wanazouziwa huwa ni mbovu maana haiwezekani juzi wameintro ndgee mpya leo ndege wanacancel.

Pia watanzania mnajiunga kwa kumsupport Fastjet ili huyu mtu aweke heshima

tatizo sio ndege mama, tatizo huwa ni abiria. kama abiria wa hiyo flight ni wachache huwa wanatoa visingizio vya hapa na pale baadae wanawachanganya abiria wa ndege labda mbili au tatu mnaondoka pamoja. hakuna cha tatizo wala nini, mimi yalishawah nikuta haya na kuchunguza ndo nikafahamu jamaa walikuwa wanatuvutia muda tujae watuchanganye kwa flight moja watu wa flight 3 tofauti i mean timing zilikuwa tofauti tukajikuta tuko kwa ndege moja.
 
nilikuwa natoka mwanza tarehe 25 Nov,2012 jumapili kwa ndege ya ya saa mbili na nusu usiku, nimefika airport saa moja kasoro nakutana na msururu wa abiria tukiuliza mbona hatu check in wakadai eti machine za kuprint boarding pass zimefail so they do it manually, tukaendelea kusubiri weee, tahamaki saa mbili na nusu hii hapa bado tupo , kwenye foleni hakuna anaeingia, PW hawatoi maelezo yoyote , ikabidi tuulize, muda wa flight kuondoka umefika na bado tupo hapa what is happening mbona hatuma maelezo, ndio jamaa anasema ohh sijui Boing ilipata hitilafu since mchana, so mchana ikaja ATR ambapo haikuweza kuchukua abiria wote, wengine walibakizwa imebidi waende wa mchana kwanza na ndege ya saa mbili na nusu usiku halafu sisi wa tusubiri ndege nyingine saa tano usiku, na kweli tuliondoka saa tano usiku mwanza.

The same problem imenitokea jumapili ya tarehe 9 Dec, 2012, ilikuwa niondoke na ndege ya saa saba na nusu mchana from mwanza to dar nimefika airport saa sita kasoro, PW wanatuambia Boing imeshindwa kuja mwanza so since asubuhi inakuja ATR ambayo haina capasity ya kubeba abiria wote , kwa hiyo waliachwa asubuhi ndio watakaondoka mchana na sisi wa mchana tukaambiwa tuache tiketi, turudi saa kumi nambili jioni , ili tuondoke na ndege ya saa mbili na nusu usiku , of which tuliondoka saa tatu na dak kumi usiku, tumefika dar saa nne na nusu usiku, nilikuwa na visamaki wangu wameharibika, na abiria walikuwa waondoke na ndege ya saa mbili na nusu usiku wakaaambiwa wataondoka saa saba usiku!
sasa najiuliza PW mna matatizo gani ?? mbona hizi delays zimekuwa nyingi mnooo, halafu hamna customer care, abiria hadi anafika airport ndio anaambiwa ndege yake itadelay,? kwa nini mnachukua abiria kupita uwezo wenu?
 
Una afadhali wewe umeambiwa ndege mbovu.
Mie niliambiwa ndege imejaa, ilhali nina return ticket tangu naondoka Dar jana yake. Nilikuwa najisikia kupigana pale KIA, thanks to mchelewaji mmoja, nikapewa nafasi yake

KIA ndi zao wanauza ticket mara mbili.halafu wale waudumu wanadhalau sana hawana kauli nzuri kwa wateja has yule dem mwembamba
 
Mkuu thnx kwanza,

Ni mara chache sana kutokua airport 1.30hrs kabla ya safari za ndani na 2hrs kwa za nje. Mfano Leo tu nimefika airport saa 12.05 na flight yangu ilitakiwa iwe 1.10 asubuhi, hapo kwa Mimi nilijiona Kama nimechelewa, na ndio maana nilikua nikirush!! Na checkin counter ilikua na foleni, dada mmoja akicheck lkn ghafra akastop kucheck na kusema kunaitirafu kwenye hiyo ndege! Kwa precision yamenikuta mengi, mzigo kusauhuliwa, kuharishwa kwa flight na wakati mwingine unaambiwa ndege imejaa wkt wa kucheckin

Kama alikua ana check in halafu akasema ndege ina matatizo,hao waongo lazima ilikua over booked.wana michezo michafu sana mie siwapendi precision
 
KIA ndi zao wanauza ticket mara mbili.halafu wale waudumu wanadhalau sana hawana kauli nzuri kwa wateja has yule dem mwembamba

Umeona eeh! Wamevimbiwa, ngoja wapewe haluli
 
hadithi za PW ni nyingi mno. mimi ni mteja wao mkubwa sana mpaka airhostesses wengi wananifahamu na katika route nyingi sana ila imefika kipindi nikiambiwa napewa tiketi ya PW naagiza nisafiri siku moja kabla hata kama mkutano unaanza mchana siku hiyo. Nimepitia machungu mengi. tahadhari, usipende kusafiri na ndege za asubuhi alfajiri za pw. ukikata tiketi usisahau kuuliza je kuna ndege nyinginesiku hiyo kwenda huko. ukiprwa jibu ndiyo angalia muda btn ndege hizo maana uwrzekano mkubwa ndege ya pili is more reliable. usipende kusafiri na ndege ya saa 4 usiku toka mwanza kuja dar maana piga ua kama ni weekend hiyo ndege itaondoka mwz saa 7 usiku. ukiondokea kia.usishangae unafika airport wanakuambia ndege imejaa. they always overbook flights hasa pale kia au ndio wanapeana kitu kidogo na watu waluichelewa ndege. unaweza ukajikuta unaondoka ns boeing inayotoka nairobi usiku. ukipata ya mchana badi mtapitia zanzibar.
PW inabidi ijitahidi kuwa ontime na hata hizo hitilafu inabidi waziangalie kwa karibu.
kuna siku tulikaa kwenye ndege pale JKNIA tukisubiri abiria toka west africa walioletwa na KQ waliokuwa wanaelekea KIA. yaani joto iliyokuwepo kwenye ndege so unbearable basi tueleze kwa nini hatuondoki wako kimya. basi hao wanaija walipoingia si wakaanza kututukana watanzania kuwa hatuna akili hapo pw waluwakatalia mwrnzao aliekata tiketi ya atcl kwenda arusha wakataka lazima apande pw. basi wakazuia ndege kuondoka makelele mtindo mmoja. baadaye akapanda ila matusi hayakuishia hapo. kumbuka tulikalishwa 2 hrs airport halafu tukakaa 1 hr kwenye ndege alafu mnaija anakuja kuwatukana aisee kidogo tushikane kwrnye ndege. wakafikiri matusi ya kiingereza wanajua wao tu.
nina story nyingi ila pw inabidi iboreshe huduma.
 
Treni imeanza kufanya kazi, dar mwanza third class ni 13,000/= tu..!!!
 
Mkuu Kirefu cha PW ni nn?
PW haina kirefu(ingawa unaweza kuhisi kuwa p=precision), lakini ni mfumo wa IATA wa utambuzi (identity) wa shirika la ndege kwa kutumia herufi mbili tu(two letter designator) kwa ndege yoyote inayofanya safari za kibiashara.
Herufi hizi zinatumika kwenye masuala ya routes, booking/reservations, ratiba, tiket na ishu zote zinazohusiana na biashara ya ndege za kampuni hiyo.
Kwa Precision utaona hata registration za ndege zao zote zinaanzia na PW..., lakini herufi ya tatu inabadilikabadilika kwa kila ndege(PWA, PWB,PWC,PWD,PWE etc)
 
haya mpwa umesomeka ilikuwa inanichanganya sana hii
 
hahaha Fast Jet is more worse.

Ndege gani iko full all the time. Ila nimegundua watanzania wanapenda vitu vya mteremko sana!! Very cheap!

cheap generalisation; barbs to you! sio kupenda "mteremko" kama unavyojaribu kurahisisha mambo bali ni kutafuta uwiano baina ya mahitaji na mgawanyo wa raslimali adimu!
 
cheap generalisation; barbs to you! sio kupenda "mteremko" kama unavyojaribu kurahisisha mambo bali ni kutafuta uwiano baina ya mahitaji na mgawanyo wa raslimali adimu!

Mimi siyo mtaalam wa mahesabu ila kwa hili its too much. Hii ni njia ni ya kuvutia watu wasio na uelewa. Ni mtazamo tu siyo lazima ukubali ninachosema.
 
hahaha Fast Jet is more worse.

Ndege gani iko full all the time. Ila nimegundua watanzania wanapenda vitu vya mteremko sana!! Very cheap!

Mi naona it is the opposite, watanzania wanapenda vitu ghali wakipata cheap wanavidharau!
 
Mkuu una uhakika hizo ndege ni mpya????Ulishapanda ndege zingine the same size ukaona tofauti??ndege za PW ni mpya zingekuwa zinaunguruma kama zinataka kupasuka???Mungu atulinde tuu coz usafiri wa anga tanzania bado sana...

Back
Top Bottom