Mkuu
PakaJimmy, maelezo unayoyatoa ni understandable sawa(na si kwamba watu hawayajui), tunachoongelea ni delay za kila siku, kutotolewa kwa taarifa mapema, majibu mabaya n.k wanaovionyesha.. haiingii akili mmeshafanya checking then mnaambiwa ndege hakuna!Kweli??..Sometimes mizigo inapotea na luggage tag uko nayo, tena ukiwa wa kwanza katika sehemu ya kusubiria mizigo!!
Kuna siku tulikuwa tunaondoka hapa JKN Airport na PW ya jioni, check in ilikuwa saa kumi na moja(na mtu unawahi kwa ajili ya foleni ya jioni ile) lakini hatukuwa na usafiri hadi kesho yake asb.(Taarifa ilikuja kutolewa saa mbili na nusu usiku)..imagine, kuna Binti alikuwa anakaa Kimara na alikuwa yuko na mtoto wake, hawana mahali pa kwenda, na kuna mzee aliletwa tu pale na anasema mwanae anakaa huko Tegeta, sasa situations kama hizi ndizo zinazoudhi!
Unapokata ticket unaacha njia ya mawasiliano, what is the use of that?..na kama wakishindwa kutoa huduma ya usafiri kwa wakati kwanini wanashindwa kuwahudumia wateja wao(kuwajibika kwa usumbufu)? Hizo expenses nyingine alipe nani? Usalama wa wateja uko wapi?
Wakati fulani mikutanoni/kazini mtu unachelewa almost kila wakati kwa sababu tu ya delay!Na ukiwaambia
Haijalishi kama wana ndege mpya au lah! wala idadi kubwa ya ndege au wahudumu...Hata kama wakiwa na ndege kidogo(chache) lakini huduma nzuri hakuna atakayelalamika! Watu wanasema/tunasema haya kwa kuwa inaudhi na kuna expectation fulani unayoitarajia katika kupata huduma iwapo ni haki yako.
We understand kuna wakati wa services(maintanance services), lakini iwapo kuna Technical matter taarifa zitolewe mapema,