Precision Air hongereni lakini mnakera..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision Air hongereni lakini mnakera..!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kwetunikwetu, Sep 30, 2009.

 1. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Last Sunday nilikuwa natoka Tabora kuja Dar kwa usafiri wa ndege ya Precision Air.

  Kero ya kwanza (ambayo ni ya muda mrefu) niliipata pale kwenye security check ambapo jamaa (Tanzania Airport Authority) hawana modern equipment bali unafungua masanduku jamaa wanapekua. Kibaya zaidi kuna mdada nikaona kang'ang'ania sanduku langu sijui alikuwa anatafuta chupi......pumbavu zake!

  Kero ya pili ni pale baada ya kupanda ndege, mara wakamwita abiria mmoja na kumjulisha kuwa galoni lake la asali lilikuwa inavuja kwenye mizigo hivyo waishushe au atafute mfuko wa nailoni aifunge vizuri. Abiria akawaambia poa waishushe tu, kama mfuko atoe wapi, kwenye ndege kuna duka?

  Kero ya tatu ni pale ngoma ilipochelewa kuondoka na baadae wakaanza kushusha mizigo.....rubani akatutangazia eti temperature imepanda ghafla toka 25 centigrade to 31 centrigrade hivyo taking off ingeleta shida mzigo mkubwa. Hivi huwa wanajaza mizigo mpaka maximum capacity? Assume ndio ndege ingekuwa inataka kutua na mzigo mkubwa, si tungechimba mchanga hapo?
   
 2. w

  wasp JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kero ya Precision Air katika swala hili ni nini? Kwanza, Security check ni kazi ya TAA na sio Precision Air. Kama TAA pale Tabora hawana vifaa vya kisasa vya kuscan hand luggage za abiria wakulaumiwa ni Wizara inayohusika na sio Precision Air. Pili, je wewe ulitaka ndege pamoja na mizigo ya watu wengi ichafuliwe na asali kutoka kwenye galoni la abiria mzembe? Ebu fikiria ndege yenu ingelivamiwa na nyuki ambao wanafuata asali uoni usalama wa abiria ungelikuwa hatarini? Tatu, kuhusu kushushwa mizigo iliyozidi. Wewe ukumbuki yalio wapata Mheshimiwa marehemu Akukweti na wenzake pale Mbeya wakati ndege iliposhindwa kupaa angani kutokana na uzito mkubwa wa mizigo? Ndugu yangu hacha kutoa lawama zisizo na msingi.
   
 3. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Napenda nielezee kidogo kero yako ya tatu. Upakiaji wa abiria kwenye ndege una vigezo vingi hususan urefu wa kiwanja, capacity ya ndege, urefu wa kiwanja toka usawa wa bahari (sea level) na hali ya joto (Temperature).

  Mara nyingi watu wanafika uwanjani wanaambiwa ndege imejaa lakini ukiingia ndani unakuta kuna viti kama 5 hivi viko wazi. Unajiuliza kulikoni?

  Kawaida viwanja vilivyo karibu na bahari (sio ziwa) kama Dar Es Salaam, Mombasa n.k vinafanya ndege iwe na uwezo mkubwa wa kubeba abiria na mizigo kuliko viwanja vilivyo juu ( toka usawa wa bahari) kama Nairobi, Jorburg, ADDIs Ababa n.k. Kwa mafano ndege aina ya B737-200 ina uwezo mdogo kuchukua abiria kutoka (take off weight) Jorburg kuliko Dar ES Salaam. Dar Es Salaam ndege hiyo hiyo ina uwezo wa kuchukua abiria 116 (fullcapacity) na mizigo yao lakini kutoka Jorburg maximum passengers ni 80 tu! Kwa sababu Jorburg iko juu sana toka usawa wa bahari kuliko DAR

  Pili viwanja vilivyo kwenye ukanda wa joto vina uwezo mdogo (payload penalty) wa kubeba abiria na mizigo kuliko viwanja kwenye ukanda wa baridi. Ndio maana kiwanja cha Dubai (hata kama kiko kwenye bahari) kina payload penalty wakati wa joto. Kwa hiyo utakuta safari nyingi za ndege kutua na kutoka (landing and take off) kwa Dubai zinafanyika usiku wakati hali ya joto imeshuka kidogo.

  Hivyo basi kilichotokea Tabora ni kwamba wapakiaji ndege (load controllers) walipakia ndege kutokana na temperature fulani lakini mwenye kauli ya mwisho katika mambo ya weight and balance ya ndege ni rubani mkuu (captain). Akiona kuna mabadiliko ya temperature analazimika kuagiza hatua fulani kuchukuliwa ikiwemo kushusha mizigo hata abiria ikibidi.
   
 4. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Unauliza kero gani, kama huoni nilichoandika si ukae kimya. Asiyejua security check ni kazi ya TAA ni nani, umesoma vizuri post yangu au unadandia juu juu tu.

  Yaliyobaki sina haja ya kujibu nisije nikafanana na wewe! Angalia post fafanuzi iliyotolewa na ByaseL sio unakurupuka tu ili kujaza maneno
   
 5. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Usiwatetee hao precision, Hawa jamaa wanatoa huduma lakini pia wanakero nyingi inabidi wazifanyie kazi la sivyo likija shirika jingine lenye ushindani watatoa macho abiria watakavyowakimbia. Mimi nilisafari na precision mwezi April kwenda Shinyanga, Tulifika airport saa 11 alfajiri na flight ya kuondoka saa moja, ilipofika muda walifanya usanii fulani na kucancel flight yetu na kutueleza kusubiri inafanyiwa matengenezo, tulisubiri mpaka saa nane tukaboard flight ya saa nane ya kwenda Mwanza na siyo Shinyanga tena, Mwanza na Shinyanga nauli ni tofauti hawakuturudishia diffrence ya nali. Baada ya kuingia ndani tukagundua kuwa ile flight ya asubuhi walicancel kwa kuwa haikuwa na abiria wengi wa kujaza seat zote hivyo kwa kutumia usanii wao wakatuchanganya na abiria wa mchana ili wamaximise profit. Angalia kero tuliyopata kuchelewa kufika tunakokwenda, kupelekwa destinationa tofauti ........
   
 6. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  biashara imani jamani
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Yote hayo sijaona tatizo la precission kama precission

  1)swala la cheki ni jukumu la taa na si precission

  2)kuhusu kuvuja asali ni haki ya sec kumwambia abiria...kumbuka kama si kujmjulisha mizigo ya watu wengine ingekuwa ina asali..hapo sijaona precission inapohusika

  3))swalal la mizigo nafikiri jukumu la kampuni ya handling ambayo owner si precission...2 jukumu la capt kushusha mizigo kma anaona iko above capacity ya ku takeoff yaani hairuhusiwi kutakeoff na max landing...so kwanza mshukuru mungu marubani wengoni ndio yanatokea ya juma akwikweti

  la nne ni wajibu wako kupanda ama kutopanda precission

  kila la kheri
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Yote hayo sijaona tatizo la precission kama precission

  1)swala la cheki ni jukumu la taa na si precission

  2)kuhusu kuvuja asali ni haki ya sec kumwambia abiria...kumbuka kama si kujmjulisha mizigo ya watu wengine ingekuwa ina asali..hapo sijaona precission inapohusika

  3))swalal la mizigo nafikiri jukumu la kampuni ya handling ambayo owner si precission...2 jukumu la capt kushusha mizigo kma anaona iko above capacity ya ku takeoff yaani hairuhusiwi kutakeoff na max landing...so kwanza mshukuru mungu marubani wengoni ndio yanatokea ya juma akwikweti

  la nne ni wajibu wako kupanda ama kutopanda precission

  kila la kheri
   
 9. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna kakero kengine bwana
  wanawapendelea sana wazungu mfano unakuta wanapewa bier mbilimbili wakati wengine wamepewa mojamoja,au wanatumia simu especially while taking off nk!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwe2nikwe2, hata kama ndege ikijazwa maximum load wakati wa kutua haiwez chimba mchanga km ulivouliza. Njiani huko hewani mafuta yanachomwa hivyo mzigo hupungua. Na hata kama haujapungua na kufikia kiasi kitakiwacho wakati wa ku-land, rubani atamwaga mafuta akiwa hewanh mfano baharini. Halaf kumbuka Temperature (joto) inaafect take off run. Huu ni umbal ndege ina roll na matairi in touch with ground mpaka iingie hewani(airbone). Kama take off run (ambayo hupatikana ktk graphs flan) ni kubwa kuliko runway(barabara itumiwayo
  Na ndege ku-land na ku-take off) length, captain hawez ruhusu kuondoka. The only solution ni kupunguza uzito wa ndege. Hii yote ni kwa usalama wa abiria, crew na malizao.
   
Loading...