PPRA pamoja kuweka mfumo sahihi, kagueni michakato ya manunuzi inayofanywa na Procurement Unity. Bado urasimu unaendelea

Embe Bichi

Member
Feb 1, 2024
87
206
Habari za asubuhi wanajamvi. Naomba nielekeze malalamiko yangu moja kwa taasisi husika hapo.

Kwanza nitangulize pongezi kwenu kwa maboresho ya mfumo wa manunuzi kutoka Tanep`s na kwenda Nest. Mwaka jana wakati mnaendesha semina kuhusu huu mpya mojawapo wa vitu mlivyotuahidi ni kuwa mfumo huu unaenda urasim wote uliokuwa unafanyika hivyo wazabuni wangepata zabuni kama taratibu na vigezo vinavyohitaji.

Pia naomba niwakumbushe kuwa kila zabuni moja tunayojaza na kuwasilisha kwenye mfumo tunakatwa 30,000 au 100,000.00 kama ni zabuni ya kualikwa. Tunatambua kuwa baada ya kuomba jukumu linalofuata ni evaluation na taratibu zingine.

Ninaomba niulize swali kidogo ambalo limenifanya niandike huuu
Hivi inawezekanaje umetangaza zabuni, umealika watu zaidi 10, wameshiriki kuomba hiyo baada ya ufunguzi matokeo yanaonekana, baada ya wiki moja hiyo zabuni inarudiwa kutangazwa tena pasipo hata notification kwa wale waombaji wa mwanzoni kuarifiwa kuwa wameshindwa kwa sababu ya kigezo fulani.

Hiyo zabuni inaporudiwa kutangazwa mojawapo ya wale wazabuni walioomba mwanzoni wanaalikwa tena {hapa nitumie neno kuwa waliokosa vigezo na kusababisha zabuni kurudiwa}. Cha kushangaza hakuna mabadiliko au ammendment yoyote ambayo imefanyika kwenye BOQ ni ile ile ya mwanzoni, hata qualification information zinahitajika zilezile za mwanzoni lakini cha ajabu mojawapo ya wale wazabuni wa mwanzo ambaye kwenye zabuni ya mwanzo almost alikuwa highest bidder anarudia ile zabuni na kushusha bei kwenye zabuni ya pili almost 10% kutoka kwenye bei ya mwanzoni na baada ya wiki mbili mnatoa notification ya kumpa huyo mtu zabuni.

Ombi langu ni moja, kama mnakuwa na interest na mtu, ni vyema mkamulika pekeake kwa zabuni hiyo kwa sababu mfumo unaruhusu maana una kipengele kualika mzabuni mmoja (single source), haiwezekani kama mtu alikosa vigezo kwa zabuni ya kwa kwanza baada kurudia zabuni hiyo hiyo na vigezo vile vile anashinda. Kumbukeni na sisi tusiokuwa kuwa na connection tuna wapambe wa chini chini (underdog) wanaotupatia information sahihi kwa yale wanayofanya PMU.

PPRA pamoja kuweka mfumo sahihi lakini pia kagueni michakato ya maunuzi inayofanywa na Procurement Unity bado urasimu unaendelea na kusababisha sisi tusiokuwa na connection tukose zabuni tulizokuwa tunasitahili kwa kupokwa na kupewa wengine wakati huo tukiwa tumekatwa hela maana zabuni hatujazi.

N.B: Nilichokiandika hapa nina ushahidi nacho maana ni mojawapo ya watendewa, nimeuriwa niliamshe ila kila nikiangalia nikifanya hivyo ndugu yule (PMU) anaenda kupoteza kibarua chake.

Tunatumia hela nyingi kwenye zabuni hizi, tupeni haki yetu pale tunapokuwa tumestahili. Unachokipata kwa Mshana hata Embe Bichi pia anaweza kukupa pia.

Ahsante ngoja niende kuaga mwili wa Rais wangu mstaafu.
 
Pole sana tajiri....inawezekana the lowest bidder bado akawa ame exceed budget ya taasisi husika na kupelekea kutangazwa upya. Na kama ilikuwa ni invitation ya watu kumi, wanaweza waka extend idadi ya wazabuni kuwa wengi zaidi kwenye re-advert ili kupata ushindani mkubwa zaidi.
 
Mkuu kwenye bajeti hapo sio, wazabuni walikuwa 8, pia tuna taarifa kutoka vyanzo vya ndani kuwa wazabuni wote tulikuwa chini ya Engineer estimate, tatizo ni kwamba yule waliekuwa wanamhitaji alikuwa yuko mbali sana, na wote waliokuwa chini yake walikuwa wanakizi vigezo hivyo ikawa hamna namna zaidi ya kurudia zabuni na kumwambia ashushe bei.
 
Uzuri intention to award ikitoka, huwa ina toa room kwa washiriki kulalamika. Its better ukafuata hizo hatua. Japo kitendo cha kusema pia unataarifa za ndani kinaweza kukutia hatiani kwamba unajihusisha na rushwa.

Nenda nao taratibu na kwa akili.
 
Shukran mkuu
 
Back
Top Bottom