Ppf inaitaji msaada na marekebisho;;hatari kujiunga nayo


P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
Kama mnaweza ni vyema mkajiunga na mashirika mengine
hili ppf kwa kweli limeanza kuchoka watu wameanza kudai pesa
yao kama walikuwa awatoi.....pesa zinakuja daiwa baada ya mwaka
je hapo kuna umhimu wa kujiunga nayo??
Hili shirika linaitaji kurekebishwa watu wamenza kufanya kazi kwa mazoea kwa urafiki na mwisho kuanza kuaribu maisha ya watu
nalaani kwa garama zote mambo machafu yanayfanywa na ppf
akuna sehemu utasikia mdau amekaa zidi ya miezi 3 akaachwa kimya
huu ni uhuni kuanzia bodi mpaka menejiment yake....kama mnaweza kuhama ameni mara moja kwanza mfumo wake wa kulipa pesa ni mchafu kabisa tofauti na nsff na wengine wapya wazuri
unaenda sehemu kudai hela yako kwa shida baada ya hapo wakwambie sheria fulani imetumika upati hela yako yoote jamani huu si ujambazi
embu tuamke kama mnaweza kuhamia nssf na wengineo nawatangazien jamani tuwakimbie hawa tuwaachie wenyewe na matapeli wao watakaoweza kuishi nao wanavyotaka bila kutuharibia fyucha za watoto zetu....kumekuwa na matatizo ya makampuni mengi yakiwalalamikia kwa kuacha waajiri wakitumbua pesa za wafanyakazi bila kupeleka sehemu husika...na hili yawezekaana ikawa ni ama urafiki wa wakurugenzi husika ama watu kutotambua umuhimu wa wajibu wao

nawakilisha
 
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
39,863
Likes
8,686
Points
280
P

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
39,863 8,686 280
NHIF kuwachukulia hatua waajirina Mwandishi Wetu
BAADHI ya waajiri nchini wamelaumiwa kwa kuwakata wafanyakazi wao michango ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) bila kuwasilisha makato hayo kwenye mfuko huo.

Taarifa ya NHIF iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, ilisema waajiri hao wanajumuisha halmashauri za miji, taasisi na mashirika ya umma pamoja na wakala wa serikali walioko Dar es salaam na mikoani.

Mkuu wa Elimu ya Umma wa Mfuko huo, Rehani Athumani, alisema mfuko wake utawachukulia hatua za kisheria waajiri hao kwa sababu ya kutowasilisha michango; ni kukiuka sheria Na. 8 ya mwaka 1999 iliyoanzisha mfuko huo.

Rehani aliongeza kuwa wakati waajiri hao wanakaa na michango hiyo, kwa upande mwingine wafanyakazi wao wanaendelea kupata matibabu na familia zao jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa mfuko.

Alisema miongoni mwa hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa na NHIF ni pamoja na kuwasilisha orodha ya waajiri hao kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Mbali na hiyo, mfuko utawafungulia mashtaka waajiri wote sugu ambao juhudi za kuwashawishi wawasilishe michango kwa njia za kiungwana zinaonekana kugonga mwamba.

Hadi kufikia Februari mwaka huu, mfuko huo ulikuwa na wafaidika milioni 3.1 ambapo wanufaika milioni 1.9 ni wale wanaohudumiwa kupitia huduma za NHIF wakati milioni 1.2 walihudumiwa na Mfuko wa Afya ya Jamii inayoendeshwa kupitia halmashauri 99 za wilaya nchini.
 

Forum statistics

Threads 1,236,034
Members 474,926
Posts 29,244,266