PPAA yajipanga kuwanoa Wazabuni, Taasisi Nunuzi juu ya mfumo mpya wa kuwasilisha Rufaa Kieletroniki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,984
12,307
Ili kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imejipanga kutoa mafunzo ya mfumo mpya wa kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na Rufaa kwa njia ya kieletroniki (Complaint and Appeal Management) kwa wazabuni na taasisi nunuzi wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Pwani.

Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando amewasihi wazabuni na taasisi nunuzi wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Pwani kuhakikisha wanashiriki mafunzo hayo muhimu ili kuwajengea uwezo wa kujua jinsi kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kielektroniki pindi wanapoona hawakutendewa haki katika michakato ya ununuzi.

Sando ametoa wito huo leo tarehe 10 Mei 2024, alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha “Power Breakfast” cha Clouds Fm Jijini Dar es Salaam juu ya Moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) uliojengwa chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
WhatsApp Image 2024-05-10 at 17.16.43_226db67f.jpg

WhatsApp Image 2024-05-10 at 17.16.44_9b0af2ab.jpg

Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando akielezea moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika kipindi cha Power Breafast cha Clouds FM, Jijini Dar es Salaam.
“Kutokana na mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, ambayo inazitaka taasisi nunuzi na wazabuni kutumia (NeST), PPAA kwa kushirikiana na PPRA tumejenga moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki ili kukidhi matakwa ya sheria,” amesema Sando.
WhatsApp Image 2024-05-10 at 17.16.45_7d7189f3.jpg

Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando .
Sando ameongeza kuwa kuanzishwa kwa moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kielektroniki (Complaints and Appeals Management) katika Mfumo wa NeST, PPAA itaweza kufanya mapitio ya mchakato mzima wa zabuni inayolalamikiwa na kuiwezesha Mamlaka Rufani kupata uhalisia zaidi na kutoa uamuzi kwa wakati, haki na usawa.

Sando aliongeza kuwa, Sheria ya ununuzi wa umma imekuwa ikifanyiwa maboresho kila baada ya kipindi fulani kutokana na mahitaji pamoja na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia.
 
Back
Top Bottom