Mfumo wa E-Mrejesho hautoi majibu kwa malalamiko ya watu

Konny Joseph

Member
Aug 28, 2016
81
133
Pamoja na kwamba serikali imeamua kuanzisha mfumo unaowawezesha wananchi kupeleka malalamiko, maoni, taarifa ama mapendekezo kwa taasisi mbalimbali za serikali ili kuweza kuzitatua, ila mfumo huo kwa upande wangu sijaona kama unafanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Binafsi nilishawahi kuandika malalamiko mara tatu kwenda kwenye taasisi mbalimbali za serikali, lakini mpaka sasa, hakuna hata lalamiko moja lililojibiwa, zaidi tu ni kuambiwa kuwa lalamiko langu limepokelewa na kupelekwa katika taasisi husuka, ila hakuna majibu yeyote niliyopata kuhusu utatuzi wa malalamiko yangu.

Hii inaonyesha wazi kwamba mfumo huu bado haujaweza kukidhi mahitaji ya watanzania, aidha kwa wahusika wenye dhamana ya kusimamia mfumo kutokuwajibika kuwasilisha taarifa kwenye sehemu husika au wahusika wanaolalamikiwa kutokubali kuwajibika kulingana na malalamiko yanayowahusu.

Labda kama kuna mtu mwenye uzoefu zaidi juu ya hili anisaidie uzoefu zaidi juu ya huu mfumo.
 
Back
Top Bottom