Post SMS za vichekesho na utani hapa

(Joni) dogo wa darasa la kwanza kafika shule akaanza kulalamika kwa mwalimu wake wa darasa kwamba la kwanza si saizi yake na anataka arushwe hadi darasa la tatu kwa maana anaamini ana akili kumzidi hata dada yake ambaye yuko darasa la tatu. Ticha wa darasa kuona dogo kazidi kupiga kelele na kusumbua akamchukua akaenda naye kwa mwalimu mkuu. Ticha wa darasa: Huyu mtoto hata simuelewi, darasani anapiga kelele kwamba anataka apelekwe na darasa la tatu kwamba la kwanza si saizi ya akili zake.

Ticha mkuu akapigwa: Ngoja nimuulize maswali ya la tatu akishindwa arudi darasani na akae atulie vinginevyo acheze na bakora. We mtoto, tatu mara tatu ngapi?
Joni: Tisa mwalimu.
Ticha mkuu: Tisa mara 4?
Joni: 36
Basi ticha mkuu akamkandamiza dogo maswali kibao ya darasa la tatu dogo akawa anapatia.
Ticha mkuu: mwalimu mi naona kijana yuko sawa, hebu mpeleke tu darasa la tatu, fanyeni utaratibu wa kumuingiza kwenye atendensi ya darasa la tatu.
Ticha wa darasa: sawa mwalimu ila ngoja nimuulize maswali zaidi. Joni ni kitu gani ambacho ng'ombe anavyo vinne na mimi ninavyo viwili?
Joni: Miguu
Ticha: Kitu gani unacho ndani ya kaptula yako ya shule ambacho mimi sina? (Ticha mkuu akashtuka kuhusu hilo swali)
Joni: Mifuko
Ticha: Kitu gani mbwa anakifanya halafu binadamu anakikanyaga?
Joni: Kujisaidia haja kubwa njiani. (ticha mkuu mdomo ukawa uko wazi anashangaa)
Ticha: Kitu gani ukikiingiza ndani kinakuwa kigumu na cha rangi kama nyekundu au pink lakini kikitoka kinakuwa kilaini na kinanata nata? (Ticha mkuu jicho likamtoka lakini kabla hajamzuia dogo kujibu dogo akatoa jibu)
Joni: Big G.
Ticha: Kitu gani mwanaume anakifanya akiwa amesimama, mwanamke akiwa amekaa na mbwa akiwa kasimama kwa miguu mitatu?
Joni: Kujisaidia haja ndogo.

Ticha mkuu akaanza kutetemeka.

Ticha: Neno gani linaanza na herufi K na linaishia na herufi A ambalo huleta raha sana watu wakilitamka?

Joni: KULA

Ticha mkuu akavuta pumzi ndefu halafu akazishusha akasema: Mwalimu naona mpeleke Joni darasa la tano. Maswali yote sita ya mwisho mimi mwenyewe nimekosea majibu yake.
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom