GE2010 Post-Mortem: Kwa Nini Dr. Slaa Na CHADEMA Wameshindwa

- Chadema wanastahili heshima sana kutoka kwetu wananchi wa Tanzania, kwa kuweza ku-compete katika mazingara magumu sana ndugu zangu, msisikie jamani haya mambo sio mchezo huko ground zero, maana unashindana na walioko kwenye power for the last 50 years, usitegemee kwamba watakuachia kirahisi rahisi. Kwa hilo Chadema wanastahili sana pongezi, na hasa ni vizazi vijavyo ndio watakuja kufaidi kazi nzito zilinazofanywa na Chadema sasa.

- HOWEVER: Chadema, kwa maoni yangu tatizo kubwa ni la ni la personalities zaidi kuliko chama inapokuja kwenye collectivity political image. Ninaamini wananchi wengi wamempigia kura Dr. Slaa as DR. Slaa wanayemsikia bungeni, kuna wakati Chadema ilikuwa Zitto, ninasema hivi inaeleweka kwamba Chadema ni wachanga, lakini wafike mahali walifanyie kazi hilo la chama kuwa mbele kuliko majina ya viongozi, na wajitahidi sana kuweka sura ya taifa katika uongozi wao wa juu. Ingawa kwa sasa inaeleweka kwamba they had to start somehwere!

- Chadema wapunguze hasira katika siasa za kampeni, ni sawa sana kuwa na hasira bungeni, lakini kuileta ile hasira kwa wananchi inaweza ikawatisha wananchi waliozoea amani, wakaona afadhali zimwi wanallolijua zaidi kuliko sera za hasira, wananchi wengi sana waliohojiwa kuhusu huu uchaguzi wamesema hayo tena sana kwamba waliogopa sana kutokea vita, kwa hiyo wakpigia CCM.

- Matatizo mengine karibu yote ya Chadema ni ya uchanga zaidi kuliko uongozi kwa hiyo tunaweza kuwasamehe, I mean kuna masuala ya hela haya yanaeleweka sana kwamba hawana hela za kutosha, kwa hiyo bado hawawezi kufikia kila sehemu ya taifa na ninaamini kwamba viongozi wao wengi walioshinda wametumia rasilimali zao binafsi kufanikisha kampeni zao, otherwise ninaamini kwamba Chadema wako on the right track, I mean kushindana na political machine ya 50 years, jamani sio mchezo ndio maana ninasema tena kwamba Chadema wanahitaji pongezi kubwa sana, maana kwa mara ya kwanza wameonyesha kwamba CCM sio invisible tena kama ilivyokuwa zamani na sasa inapenyezeka!

- Look at this: Kwa mara ya kwanza katika historia ya hili taifa, nimeona kiongozi wa kampeni ya CCM akilalamikia media, kwa mara ya kwanza CCM wamekataa mdahalao, kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili Usalama Wa Taifa wamelazimika kujitokeza in public na kujibu tujuma za siasa za mgombea wa Chadema never before this has happened in our history, tumejionea viongozi wa CCM wakijitokeza kujibu malalamiko ya Chadema na Dr. Slaa never before hii imetokea, kwa nini wamefanya yote haya ni kwa sababu hawakutegemea yaliyojiri wameingia kwenye hizi kampeni na idea ya politics as usual, kwa hiyo kwa maoni yangu uchanga na mazingara bado ni tatizo kubwa sana la Chadema, lakini all in all wako kwenye the right track na they did the best under mazingara ya siasa tuliyonayo!

William.
 
Superman... unamaana gani "wameshindwa"? maana ukiniuliza mimi nitakuambia walioshindwa ni CCM kulinganisha na matokeo ya 2005. Kwa kila kipimo.. hakuna mahali ambapo CCM imeongeza viti au kura. Lakini naweza kukuonesha mahali ambapo Chadema imeongeza viti na kura (ndio kushinda kwenyewe). Ama ushindi ni kuwa Rais tu ndio tunaweza kuuhesabu kuwa ni ushindi?

Superman... unamaana gani "wameshindwa"(HAWAKUPATA RIDHAA YA WALIO WENGI) ? maana ukiniuliza mimi nitakuambia walioshindwa ni CCM (WAMESHINDA KWA 61.17%) kulinganisha na matokeo ya 2005 ( YAWEKE BAYANA) . Kwa kila kipimo ( KAMA VIPI ?) .. hakuna mahali ambapo CCM imeongeza viti (WANA WABUNGE 186) au kura (WANAZO NYINGI NDIO MAANA WAMESHINDA ) . Lakini naweza kukuonesha mahali ambapo Chadema (CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO) imeongeza viti na kura ( HAZIKUTOSHA LAKINI KUCHUKUA DOLA) (ndio kushinda kwenyewe)(TUME HAIKUWATANGAZA KWA MUJIBU WA SHERIA) . Ama ushindi ni kuwa Rais tu (NA WABUNGE PIA) ndio tunaweza kuuhesabu kuwa ni ushindi? (USHINDI ULIOTANGAZWA NA TUME KWA MUJIBU WA SHERIA)
 
- Chadema wanastahili heshima sana kutoka kwetu wananchi wa Tanzania, kwa kuweza ku-compete katika mazingara magumu sana ndugu zangu, msisikie jamani haya mambo sio mchezo huko ground zero, maana unashindana na walioko kwenye power for the last 50 years, usitegemee kwamba watakuachia kirahisi rahisi. Kwa hilo Chadema wanastahili sana pongezi, na hasa ni vizazi vijavyo ndio watakuja kufaidi kazi nzito zilinazofanywa na Chadema sasa.

- HOWEVER: Chadema, kwa maoni yangu tatizo kubwa ni la ni la personalities zaidi kuliko chama inapokuja kwenye collectivity political image. Ninaamini wananchi wengi wamempigia kura Dr. Slaa as DR. Slaa wanayemsikia bungeni, kuna wakati Chadema ilikuwa Zitto, ninasema hivi inaeleweka kwamba Chadema ni wachanga, lakini wafike mahali walifanyie kazi hilo la chama kuwa mbele kuliko majina ya viongozi, na wajitahidi sana kuweka sura ya taifa katika uongozi wao wa juu. Ingawa kwa sasa inaeleweka kwamba they had to start somehwere!

- Chadema wapunguze hasira katika siasa za kampeni, ni sawa sana kuwa na hasira bungeni, lakini kuileta ile hasira kwa wananchi inaweza ikawatisha wananchi waliozoea amani, wakaona afadhali zimwi wanallolijua zaidi kuliko sera za hasira, wananchi wengi sana waliohojiwa kuhusu huu uchaguzi wamesema hayo tena sana kwamba waliogopa sana kutokea vita, kwa hiyo wakpigia CCM.

- Matatizo mengine karibu yote ya Chadema ni ya uchanga zaidi kuliko uongozi kwa hiyo tunaweza kuwasamehe, I mean kuna masuala ya hela haya yanaeleweka sana kwamba hawana hela za kutosha, kwa hiyo bado hawawezi kufikia kila sehemu ya taifa na ninaamini kwamba viongozi wao wengi walioshinda wametumia rasilimali zao binafsi kufanikisha kampeni zao, otherwise ninaamini kwamba Chadema wako on the right track, I mean kushindana na political machine ya 50 years, jamani sio mchezo ndio maana ninasema tena kwamba Chadema wanahitaji pongezi kubwa sana, maana kwa mara ya kwanza wameonyesha kwamba CCM sio invisible tena kama ilivyokuwa zamani na sasa inapenyezeka!

- Look at this: Kwa mara ya kwanza katika historia ya hili taifa, nimeona kiongozi wa kampeni ya CCM akilalamikia media, kwa mara ya kwanza CCM wamekataa mdahalao, kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili Usalama Wa Taifa wamelazimika kujitokeza in public na kujibu tujuma za siasa za mgombea wa Chadema never before this has happened in our history, tumejionea viongozi wa CCM wakijitokeza kujibu malalamiko ya Chadema na Dr. Slaa never before hii imetokea, kwa nini wamefanya yote haya ni kwa sababu hawakutegemea yaliyojiri wameingia kwenye hizi kampeni na idea ya politics as usual, kwa hiyo kwa maoni yangu uchanga na mazingara bado ni tatizo kubwa sana la Chadema, lakini all in all wako kwenye the right track na they did the best under mazingara ya siasa tuliyonayo!

William.

Kwa kweli umesema ukweli ambao hata mie siupingi, ila wapo watu humu ni ma radical sana huu ukweli ulio usema hawataki kuusikia. Hebu badilikeni acheni siasa za chuki aisee.
 
Wanajamii, kutowafikia watu wengi wanaopiga kura inasimama zaidi.
Watu wengi TZ wako vijijini, twende huko. Kijijini kwangu kule Songea wanasikia CHADEMA kwenye redio tu.
Tumeshaibiwa tayari sawa lakini tujipange tusiibiwe tena 2015 na tuende nchi nzima. Mimi nimeanza kwa kufungua tawi la CHADEMA kijijini kwangu na wanachama wa kwanza huko ni baba na mama yangu.
Wewe je? Unaendelea kuangalia kisiki ulichojikwaa au unatafuta jembe la kuking'oa usijikwae tena kesho?
 
Chadema hawakusimamisha wagombea ubunge kwenye majimbo zaidi ya 60+.
Wagombea ubunge wanachangia kwa sana kwenye kampeni za uraisi.

Pia madiwani wengi hawakuwekwa kugombea.
 
Unachosema mkuu ni sahihi. Wakati mwingine ni heri kuwa na mgombea ubunge hata kama ataonekana ana nguvu kuliko kutokuwa nae kabisa
 
Nisingetofautiana sana na William lakini nina ya kuongezea:
1) Hofu ya nini CHADEMA inasimamia: Pamoja na kuwa na ilani nzuri yenye mvuto, CHADEMA walipata shida sana kuielezea na kuwaaminisha wapiga kura ingetelezeka. Sio kwa kuwa hawakuwa na maelezo bali kwa sababu CCM kwa kutumia mtandao wake waliibeza kwa hisia kali na kuichafua. Mifano ni mingi! Hii ilihusu hasa mapendekezo ya sera kuhusiana na ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu, elimu bure na sera za majimbo. Hata wasomi pale UDSM walisikika wakikituhuma kwa nguvu kabisa CHADEMA wanatafuata cheap popularity, na ni chama cha wachagga! Ndio walisema Slaa ni Mchagga na mwanzoni sikuona hii kama issue kubwa lakini kuna hisia kwamba Mchagga akichukua uongozi wa taifa basi taifa litakuwa limeisha au vile, lakin kweli kuna hofu! Na hawa wasomi (niwaite uchwara) wanakazia hoja yao kwamba haitowezekana kamwe mtu wa kabila la kichagga au kihaya akawa Raisi. Angalizo hapa ni SIASA TAKA ZA UKABILA na hofu iliyopandikizwa na wale ambao ni wapinzani wa Chadema.

2) Sio bahati mbaya kwamba CUF na CCM ilipata kukubalika zaidi maeneo ya Pwani, miji katika reli ya kati na kule kusini kwa mchomba(lindi na Mtwara). SIASA TAKA ZA UDINI zilitawala. CHADEMA walishindwa kabisa kusafisha madongo yalitupwa kwake kwamba mgombea wake ni Mdini na alikuwa ametumwa na Dini yake kugombea.

Ili Chadema wafanikie kuna kila sababu ya kutafuta jinsi ya kufuta hizi hisia ndani ya wapiga kura, pengine ni kuelekeza operesheni kama Sangara maeneo haya zaidi. Hilo la ukabila linazidi kupotea kwa kadiri CHADEMA wanalyozidi kupata wabunge na viongozi kutoka sehemu mbalimbali nchini. Kazi ya kupigana na CCM yenye mizizi na fedha nyingi, uchoyo wa madaraka na isiyo na haya kudanganya haikuwa rahisi hata kidogo. Ukifikiri ingekuwa rahisi kwa mpiga kura kuamini ahadi za CHADEMA kuliko kumwamini Kikwete na ahadi za Viwanja vya ndege, bandari, kujenga mto wa maji, reli nk. Lakini mashine ya propoganda za CCM ni kubwa!
 
Wana JF;

Katika Uchaguzi Mkuu 2010 Dr. Slaa na CHADEMA wametoa changamoto na upinzani mkali tofauti sana na miaka ya nyuma. Uchaguzi mwaka huu ulikuwa na msisimko mkubwa sana huku kukiwa na propaganda nyingi sana ambazo hazijawahi kusikika.

Kuna baadhi waliamini kabisa kuwa Dr.Slaa na CHADEMA wangeshinda katika Uchaguzi Mkuu 2010.

Kwa maoni yangu baadhi ya sababu zilizoifanya CHADEMA na Dr. Slaa washindwe ni pamoja na:

1. Kutokuwa na Mtandao mkubwa wa chama na wanachama na hivyo kukosa kuwafikia wapiga kura wa uhakika.
2. Maandalizi duni ya ki-organaizesheni katika kampeni
3. Ukosefu wa rasilimali za kutosha katika kampeni hasa fedha

Je kwa maoni na utafiti wako ni sababu gani zingine zilizofanya Dr.Slaa na CHADEMA wasishinde Uchaguzi Mkuu 2010?

Je unajua na unakubali msimamo wa akina Dr. Slaa kuwa wameshinda uchaguzi huu ila wameporwa ushindi wao? Unakubaliana nao?
 
Wana JF;

Katika Uchaguzi Mkuu 2010 Dr. Slaa na CHADEMA wametoa changamoto na upinzani mkali tofauti sana na miaka ya nyuma. Uchaguzi mwaka huu ulikuwa na msisimko mkubwa sana huku kukiwa na propaganda nyingi sana ambazo hazijawahi kusikika.

Kuna baadhi waliamini kabisa kuwa Dr.Slaa na CHADEMA wangeshinda katika Uchaguzi Mkuu 2010.

Kwa maoni yangu baadhi ya sababu zilizoifanya CHADEMA na Dr. Slaa washindwe ni pamoja na:

1. Kutokuwa na Mtandao mkubwa wa chama na wanachama na hivyo kukosa kuwafikia wapiga kura wa uhakika.
2. Maandalizi duni ya ki-organaizesheni katika kampeni
3. Ukosefu wa rasilimali za kutosha katika kampeni hasa fedha

Je kwa maoni na utafiti wako ni sababu gani zingine zilizofanya Dr.Slaa na CHADEMA wasishinde Uchaguzi Mkuu 2010?

Naomba nitoe maoni yangu kuhusu Dr.Slaa na CHADEMA kutokushinda Uchaguzi Mkuu 2010 kama ifuatavyo :-

1. Watanzania wamekuwa mtaji wa CCM kwa kufanywa wasiwe na ufahamu wa haki zao pamoja na nchi wanayoitaka (Ujinga!! mtaji wa CCM)

2. Watanzania wamekuwa mtaji wa CCM kwa kufanywa masikini (Ufisadi ni mtaji wa CCM) kwa kutogawana villivyo rasilimali za taifa. Kwa hiyo rushwa inafanikisha ushindi wa ziada wa CCM. Vyombo vya dola vinafaidika na ufisadi haviko tayari kukubali mabadiliko. Vinalinda Ufisadi.;

3. Nakubaliana na wewe kuhusu rasilimali za kufanyia uchaguzi. Lakini la msingi pesa za seirikali zimetumika na CCM. Serikali hii ni watanzania wote.

MWISHO MIMI BINAFSI NAONA UCHAGUZI UMEBAKWA TUSUBIRI SHUBIRI
 
Nisingetofautiana sana na William lakini nina ya kuongezea:
1) Hofu ya nini CHADEMA inasimamia: Pamoja na kuwa na ilani nzuri yenye mvuto, CHADEMA walipata shida sana kuielezea na kuwaaminisha wapiga kura ingetelezeka. Sio kwa kuwa hawakuwa na maelezo bali kwa sababu CCM kwa kutumia mtandao wake waliibeza kwa hisia kali na kuichafua. Mifano ni mingi! Hii ilihusu hasa mapendekezo ya sera kuhusiana na ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu, elimu bure na sera za majimbo. Hata wasomi pale UDSM walisikika wakikituhuma kwa nguvu kabisa CHADEMA wanatafuata cheap popularity, na ni chama cha wachagga! Ndio walisema Slaa ni Mchagga na mwanzoni sikuona hii kama issue kubwa lakini kuna hisia kwamba Mchagga akichukua uongozi wa taifa basi taifa litakuwa limeisha au vile, lakin kweli kuna hofu! Na hawa wasomi (niwaite uchwara) wanakazia hoja yao kwamba haitowezekana kamwe mtu wa kabila la kichagga au kihaya akawa Raisi. Angalizo hapa ni SIASA TAKA ZA UKABILA na hofu iliyopandikizwa na wale ambao ni wapinzani wa Chadema.

2) Sio bahati mbaya kwamba CUF na CCM ilipata kukubalika zaidi maeneo ya Pwani, miji katika reli ya kati na kule kusini kwa mchomba(lindi na Mtwara). SIASA TAKA ZA UDINI zilitawala. CHADEMA walishindwa kabisa kusafisha madongo yalitupwa kwake kwamba mgombea wake ni Mdini na alikuwa ametumwa na Dini yake kugombea.

Ili Chadema wafanikie kuna kila sababu ya kutafuta jinsi ya kufuta hizi hisia ndani ya wapiga kura, pengine ni kuelekeza operesheni kama Sangara maeneo haya zaidi. Hilo la ukabila linazidi kupotea kwa kadiri CHADEMA wanalyozidi kupata wabunge na viongozi kutoka sehemu mbalimbali nchini. Kazi ya kupigana na CCM yenye mizizi na fedha nyingi, uchoyo wa madaraka na isiyo na haya kudanganya haikuwa rahisi hata kidogo. Ukifikiri ingekuwa rahisi kwa mpiga kura kuamini ahadi za CHADEMA kuliko kumwamini Kikwete na ahadi za Viwanja vya ndege, bandari, kujenga mto wa maji, reli nk. Lakini mashine ya propoganda za CCM ni kubwa!

Sahihisho Dr. Slaa siyo mchaga. Hoja yako ijenge upya. Nakubaliana na wewe kuhusu SIASA TAKA ZA UDINI na UKABILA zilizofanyika zaidi kwenye vikao vya ndani na vitanda kwa vitanda
 
Chadema walizani kulinda kura ni mawakala wazuri peke yake kumbe umati unahitajika kuzingira ofisi za halmashauri na kuimba nyimbo za ukombozi ili returning officer watangaze matokeo halali.

Siwezi kuwalaumu chadema kwa kutokuwa na watu wa kutosha kuzingira ofisi za halmashauri kwa kuwa hiki ni kitu kipya kabisa.

Nilitegemea chadema wangepata wabunge angalau 60, na around 45% presidential votes kwa ajili mikoa yenye watu wengi chadema ilikuwa inapendwa sana. Sikutegemea kikwete kumpisha slaa hata kwa damu. Kumbe nili underestimate ccm, walikuwa wameamua kukaa in power at any cost na kuiba hata kitu kisichostaili kuibwa

2015 kila mmbunge ahakikishe kuwa ana watu wa kutosha wa kuzingira ofisi za halmashauri
 
Kwa maoni yangu baadhi ya sababu zilizoifanya CHADEMA na Dr. Slaa washindwe ni pamoja na:

1. Kutokuwa na Mtandao mkubwa wa chama na wanachama na hivyo kukosa kuwafikia wapiga kura wa uhakika.
2. Maandalizi duni ya ki-organaizesheni katika kampeni
3. Ukosefu wa rasilimali za kutosha katika kampeni hasa fedha

Je kwa maoni na utafiti wako ni sababu gani zingine zilizofanya Dr.Slaa na CHADEMA wasishinde Uchaguzi Mkuu 2010?

Labda tuweke katika makundi mawili: Internal (within Chadema) na External. Hizo sababu ulizotaja ni internal sana. External ni Katiba isiyovipa vyama vya upinzani uhuru wa kufanya shughuli zao (ikijumuisha na kupata fedha za kutosha), tume ya uchaguzi yenye upendeleo, ma matumizi ya vyombo vya serikali kusaidia chama tawala. Sasa hizi external factors ndio zimesabadisha hizo internal limitations kwa hiyo ndio za kulaumu na kurekebisha. Kwa maneno mengine ni kwamba external factors zisingekuwepo na internal factors zisingekuwepo vile vile. La pili mkuu sikupenda matumizi ya neno "post-mortem" naona ni kali sana na ni na kukatisha tamaa. Ukweli ni kwamba upinzani haujashidwa kivivyo. Hatua kubwa sana imepigwa kwa mabadiliko. Labda ungetumia neno lingine
 
-
- Look at this: Kwa mara ya kwanza katika historia ya hili taifa, nimeona kiongozi wa kampeni ya CCM akilalamikia media, kwa mara ya kwanza CCM wamekataa mdahalao, kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili Usalama Wa Taifa wamelazimika kujitokeza in public na kujibu tujuma za siasa za mgombea wa Chadema never before this has happened in our history, tumejionea viongozi wa CCM wakijitokeza kujibu malalamiko ya Chadema na Dr. Slaa never before hii imetokea, kwa nini wamefanya yote haya ni kwa sababu hawakutegemea yaliyojiri wameingia kwenye hizi kampeni na idea ya politics as usual, kwa hiyo kwa maoni yangu uchanga na mazingara bado ni tatizo kubwa sana la Chadema, lakini all in all wako kwenye the right track na they did the best under mazingara ya siasa tuliyonayo!

William.

Nakubaliana na wewe kuhusu hili. Kutoingia Ikulu kusiwe ndio kama defeat. Upizani huu umeshatupeleka kwenye next level kwenye politics za TZ
 
Wana JF;

Katika Uchaguzi Mkuu 2010 Dr. Slaa na CHADEMA wametoa changamoto na upinzani mkali tofauti sana na miaka ya nyuma. Uchaguzi mwaka huu ulikuwa na msisimko mkubwa sana huku kukiwa na propaganda nyingi sana ambazo hazijawahi kusikika.

Kuna baadhi waliamini kabisa kuwa Dr.Slaa na CHADEMA wangeshinda katika Uchaguzi Mkuu 2010.

Kwa maoni yangu baadhi ya sababu zilizoifanya CHADEMA na Dr. Slaa washindwe ni pamoja na:

1. Kutokuwa na Mtandao mkubwa wa chama na wanachama na hivyo kukosa kuwafikia wapiga kura wa uhakika.
2. Maandalizi duni ya ki-organaizesheni katika kampeni
3. Ukosefu wa rasilimali za kutosha katika kampeni hasa fedha

Je kwa maoni na utafiti wako ni sababu gani zingine zilizofanya Dr.Slaa na CHADEMA wasishinde Uchaguzi Mkuu 2010?

Mwenye MACHO haambiwi tazama.
 
CCM ilimtumia Mama Kikwete kusambaza fedha na kanga kwa kina mama. Chadema haikuwa na mkakati mzuri wa kuwapitia wapiga kura wakina mama- (simaanishi kuwapa rushwa noo), hata kwenye mikutano ya Slaa waliokuwa wanaonekana kwa wingi ni vijana na wana ume

.

Mdau kuna fununu (ambazo sijathibitisha kwa sababu sina takwimu) kwamba kina mama wameangusha upinzani na wamekuwa mazito kukubali ujumbe wa mabadiliko ingawa wao ndio waathirika wakuu wa umasikini. Je, una takwimu uanzishe thread na kushirikisha wengine?
 
Kimtazamo wangu haya yametokea kwa sababu ya wizi wa ccm,vinginevyo Slaa kashinda.Manake pamoja na ubabe nwa wizi wote mliousikia ndio wamepata 61pc,ingekuwa fair unafikiri wangepata ngapi hao ccm.Pia swala la chadema kuwa na mtandao hadi vijijini lingeweza kukifanya chama kujulikana na kukubalika vizuri zaidi kiasi kwamba hata hao wachakachuaji wasingefanikiwa kwani kura zingekuwa nyingi mno,labda kutumia mbinu ya kivuitu.Pamoja na mapungufu ya kutokuwa na mtandao naamini Dr alijitahidi kufika sehemu nyingi na pia kusikika na kutambulika kila kona ya nchi na ndiyo iliyompa USHINDI tuliodhulumiwa.CHADEMA IMESHINDA!hayo mnayosema ni maboresho tu.
 
Superman... unamaana gani "wameshindwa"? maana ukiniuliza mimi nitakuambia walioshindwa ni CCM kulinganisha na matokeo ya 2005. Kwa kila kipimo.. hakuna mahali ambapo CCM imeongeza viti au kura. Lakini naweza kukuonesha mahali ambapo Chadema imeongeza viti na kura (ndio kushinda kwenyewe). Ama ushindi ni kuwa Rais tu ndio tunaweza kuuhesabu kuwa ni ushindi?
kwani chadema iliingia kwenye huu uchaguzi ikiwa na matarajio gani? imetimiza hayo matarajio? hapa wewe unataka kushinda kwenye technicalities? anzisha thread kuangalia 'ushindi' wa chadema kama unataka!!
 
Back
Top Bottom