Post-Mortem: Kwa Nini Dr. Slaa Na CHADEMA Wameshindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Post-Mortem: Kwa Nini Dr. Slaa Na CHADEMA Wameshindwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Superman, Nov 6, 2010.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Wana JF;

  Katika Uchaguzi Mkuu 2010 Dr. Slaa na CHADEMA wametoa changamoto na upinzani mkali tofauti sana na miaka ya nyuma. Uchaguzi mwaka huu ulikuwa na msisimko mkubwa sana huku kukiwa na propaganda nyingi sana ambazo hazijawahi kusikika.

  Kuna baadhi waliamini kabisa kuwa Dr.Slaa na CHADEMA wangeshinda katika Uchaguzi Mkuu 2010.

  Kwa maoni yangu baadhi ya sababu zilizoifanya CHADEMA na Dr. Slaa washindwe ni pamoja na:

  1. Kutokuwa na Mtandao mkubwa wa chama na wanachama na hivyo kukosa kuwafikia wapiga kura wa uhakika.
  2. Maandalizi duni ya ki-organaizesheni katika kampeni
  3. Ukosefu wa rasilimali za kutosha katika kampeni hasa fedha

  Je kwa maoni na utafiti wako ni sababu gani zingine zilizofanya Dr.Slaa na CHADEMA wasishinde Uchaguzi Mkuu 2010?
   
 2. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wizi pia umechangia kwa kiasi kikubwa.
  Hofu ya vita ambayo CCM iliwajaza wananchi hasa wa vijijini
  Uelewa mdogo kwa wapiga kura. Na mtaji mkubwa wa wananchi wasiojua haki zao na kuwaona wapinzani kama ni maadui
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Asante Nicky,

  Mpaka sasa tuna sababu hizi:

  1. Kutokuwa na Mtandao mkubwa wa chama na wanachama na hivyo kukosa kuwafikia wapiga kura wa uhakika.
  2. Maandalizi duni ya ki-organaizesheni katika kampeni
  3. Ukosefu wa rasilimali za kutosha katika kampeni hasa fedha
  4. Tuhuma za wizi wa kua umechangia kushindwa kwao
  5. Hofu ya vita ambayo CCM iliwajaza wananchi hasa wa vijijini na kuogopa kuwapigia kura
  6. Uelewa mdogo kwa wapiga kura juu ya mageuzi.
  7. Ukosefu wa Elimu ya Uraia kuwafikia wengi na hivyo kusababisha wananchi kutokujua haki zao na kuwaona wapinzani kama ni maadui

  Je kuna sababu zingine?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Superman... unamaana gani "wameshindwa"? maana ukiniuliza mimi nitakuambia walioshindwa ni CCM kulinganisha na matokeo ya 2005. Kwa kila kipimo.. hakuna mahali ambapo CCM imeongeza viti au kura. Lakini naweza kukuonesha mahali ambapo Chadema imeongeza viti na kura (ndio kushinda kwenyewe). Ama ushindi ni kuwa Rais tu ndio tunaweza kuuhesabu kuwa ni ushindi?
   
 5. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Nicky, ni kwa vipi sababu hizo zimechangia Dr. Slaa na CHADEMA kushindwa? Haiko wazi bado.
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  hii hofu sio vijijini tu hata mjini, rafiki yangu mmoja dar aliombwa na bibi mmoja amsaidie kutia tick sehemu ya mgombea anaemtaka, bibi alikuwa anamwonyesha kwenye picha ya kikwete, jamaa yangu akamuuliza kwa nini unamchagua huyu na sio huyu hapa ( akimwonyesha Slaa), yule bibi akasema "sina miguu ya kukimbilia baba vita ikitokea", so ni kweli wananchi wametishwa na wakatishika
   
 7. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  NEC na Usalama wa Taifa ndio sababu pekee ya DK Slaa kushindwa.
   
 8. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  MKJJ, tunaweza kuanzisha thread nyingine ya kwa nini CCM safari hii Rais amepata kura kidogo kuliko 2005 au kwa nini wamepoteza majimbo mengi safari hii ukilinganisha na 2010.

  katika thread hii ni kuangalia kwa nini CHADEMA hawakushinda na kuwafanya waunde serikali. Japo wameshinda kwa kuongeza majimbo na kura za Urais kuliko 2005 lakini bado hawajaweza kuunda Serikali. Tunapenda tuweke wazi sababu zote.
   
 9. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  ABABU ILIYO KUBWA KABISA YA CHADEMA kushindwa ni kwasababu ya hujuma na njama za CCM . Njama na hujuma hizo ni pamoja na:
  1. NEC KUCHAKACHUA MATOKEO KWA KUIPENDELEA CCM.
  2. KUWATIA HOFU WAPIGA KURA KWA KUTUMIA JESHI.
  3. CCM KUCHELEWESHA KUBANDIKA MAJINA YA WAPIGA KURA KWENYE VITUO.
  4. CCM KUTUMIA USALAMA WA TAIFA KUIBA KURA.
  5. CCM KUTUMIA VIHIYO WA IT KWENYE KUHESABU KURA.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Ya kwanza nakubaliana na wewe. KWamba CHADEMA campaign was under staffed. Haikuwa na watu wengi wa kuweza kufika kila eneo la Tanzania kwa kipindi kifupi. Na CCM walijua hilo kuwa wao hata wakiwa na mwezi mmoja wa kampeni tayari ni head start.

  Yapili si kweli. Ukiangalia kwa udani unaweza kuona CHADEMA imepata mafanikio makubwa sana kuliko uchaguzi uliopita. Angalia idadi ya ongezeko la wabunge wake bungeni ikilinganishwa na 2005. Sababu moja ni ni kuwa kuliwa na smart organisation ya wasomi na watendaji.

  Tatizo kubwa la Chadema ni kuwa it is too honest and too clean. CCM wenzao wametumia njia zote ili kupata ushindi. Kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki, ukiangalia kwa makini utaona kuwa CCM imepata kura nyingi kwa wanyonge(hohehahe na wasio na elimu) mtu akinunuliwa tu T-shirt, akipewa kofia au kitenge anachagua CCM. Hiyo kwa upande fulani ni kama kurubuni watu hawa wale wanyonge. Lakini CHADEMA haikufanya hivyo.

  Lakini mkuu angalia kwanza takwimu za waliojiandikisha na waliopiga kura, kwanini ziko tofauti sana? ni bahati mbaya au watu wakutaka kupiga kura????, jaribu pia kuangalia pia uchakachuaji. Angalia pia role ya CUF, kampeni chafu za kukitaja CHADEMA kama chama cha kikristo. Ukiangalia hayo unaweza kujua ni kwanini CHADEMA haikupata ushindi. Otherwise naweza kusema CHADEMA hawajafanya vibaya, lakini they could do much better.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Basi swali lako hapa haliko sahihi - kwani halina qualification. Umeuliza kwanini wameshindwa? Kushindwa maana yake ni kutofanikiwa, kutofikia malengo n.k Kwa mfano, kwenye Halmashauri lengo ni kupata madiwani wengi na kuunda serikali ya Manispaa hapo - mwaka 2005 Chadema nadhani ilikuwa na Halmashauri nne tu inazoongoza (Tarime, Karatu, na Kigoma Mjini, Kigoma Kaskazini kama sikosei) Mwaka huu wameshika miji karibu yote mikubwa - kwanini huku kuwe ni kushindwa?

  Kwa upande wa Wabunge Chadema ina wabunge wengi zaidi ikiwaangusha baadhi ya wabunge maarufu na hivyo kuongeza idadi ya wabunge wake kutoka sita wa kuchaguliwa kufikia 24 - Kwa maneno mengine wamefanikiwa kuwashawishi wananchi wengi zaidi kukuwakubali - kwanini huko kuwa ni "kushindwa"?

  Mbunge ana majukumu ya Bunge na siyo kila mbunge lazima awe sehemu ya kuunda serikali. Huitaji kuunda serkali ili upime kufanikiwa kwa ubunge. Lakini mimi naamini swali sahihi lingekuwa "kwanini hawakufanya vizuri zaidi ya walivyofanya sasa"? Wouldn't you agree? Kwa sababu kusema wameshindwa ni kuashiria kuwa hawakuwa na mafanikio yoyote kitu ambacho naamini si kweli.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Nov 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Hivi kikweli kweli CHADEMA wameshindwa au CCM wamechakachua matokeo na kuyafanya yawaonyeshe wao ndio washindi? Enthusiasm iliyokuwepo kwa Slaa hailingani kabisa na matokeo. Hayo ndiyo maoni yangu...
   
 13. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema haikuwa na walinzi wa kura za Uraisi kama ilivyokuwa kwa wabunge.
  Tumeshuhudia vijana wakilinda kura kwa ushujaa dhidi ya mbinu mbalimbali za kijizi katika majimbo karibu yote iliposhinda.
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Dude you are damn right. I believe that there was a serious job in doctoring election results, no wonder why NEC was twitching it's hand in releasing results, there is a huge body of evidence pointing to that direction. Any person with working brains could easily see that, but unfortunately those who make decisions in this country have decided that the will of the people can not prevail. We just have to move on, but one door has just been opened.
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  katika sababu zako hizo tatu, mimi sizikubali hata moja,
  mimi kwa mtazamo wangu, katiaka miaka yote ya vyama vya Upinzani ni mwaka huu pekee ndio chama cha upinzani kilionesha kufanya kampeni iliyokuwa well organized, na ilikuwa so focused na ilikuwa ina malengo maalumu,
  Wapiga kura wengi wa Tanzania wako Mwanza, Dar, Mbeya,Shinyanga,Arusha, KLM na wanafuatiwa na Kagera na KIgoma na Chadema walilijua hilo na wakaweka nguvu zao huko muda mrefu ref-operation Sangara (Japo ilikuwa nchi nzima lakini kwewnye mikoa hiyo ndio ilikuwa zaidi),
  sasa ukiangalia wapiga kura wa Lindi, mtwara hata wakiwa mara tatu hawawezi kuwafikia watu wa Shinyanga pekeyake, sasa uwezo ka kichama lazima uwe na target na malengo,
  ni ukweli usiopingika Japo Chadema hakupata kura nying maeneo ya kusini, lakini walikuwa na kura za kutosha kuchukua madaraka, kwa sababu walikuwa na kura nyingi kutoka kwa maeneo yenye majority
  hebu chukua mfano wa Mwanza-Nyamagana, Chadema kachukua viti 12 vya udiwani, Masha kapitwa kwa kura nyingi na Wenje, alafu JK kampita Slaa kwa kura, hivi inakuingia akilini hiyo?
  Chadema walijipanga kwa resources zao ndogo walizo nazo na walishinda huu uchaguzi
   
 16. jcb

  jcb JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 6, 2010
  Messages: 281
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ELIMU YAKUTOSHA KWA WAPIGA KURA. Mfano: Nilikuwa na vijana wa kitaa waliotoka kupiga kura wakielezea walicho fanya kwenye chumba cha kura kama kuchora vibaya picha za wagombea wengine wasio wapenda kwakufikiri ujumbe wao kwa wasio wapenda utafika na palepale chaguo lao likitimia kumbe sivyo wanaishia kuharibu kura.
  Hivyo tuna hitaji elimu ya jinsi yakupiga kura itolewe kunusuru kuharibu kura
   
 17. doup

  doup JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  mikakati ielekezwe vijijini zaidi watu wajue umuhimu wa kulinda kura zao vituoni, na kupata mawakala wa ukweli wasio mapandikizi; hapo kitaeleweka

  Sababu kuu ni Hujuma=Wizi wa kura; NEC kuwa chombo pandikizi/chakachuzi cha CCM;

  Naamini nikakati kwa 90% ilifanikiwa.
   
 18. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  kiukweli ccm walikuwa wanatumia mno vitisho kwa wanachi hasa wa vijijini kuhusu upinzani, ndo maana watu wa vijijini waliowengi ukiongelea upinzani wanajua unaongelea vita, mi nafikiri kuna haja ya elimi kubwa ya uraia kwa watu hawa ambao akili zao zimedumaa kwa umaskini wao na ujinga ulioletwa na ccm
   
 19. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #19
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Msichanganye ushindi wa kura kidemokrasia na usimikwaji wa madaraka kibabe. Mpaka sasa hakuna ushahidi w kutosha kuonyesha kuwa Slaa kashindwa kwa kura hasa kutokana na rindi la uficho wa kuhesabu kura, tofauti za wazi baina ya namba ya kura zilizotangazwa na NEC na Zile za vituoni, na ukweli kuwa NEC haikutaka kusikiliza kabisa malalamiko ya CHADEMA huku ikitoa uzito wa ajabu kwenye malalamiko ya CCM kufikia kusaidia kubadilisha matokeo kama ilivyotokea KIBAHA, KIGOMA, TARIME, SEGEREA, MBOZI, Karatu, na nusura iwe hivyo pia kwa Ubungo na arusha mjini
   
 20. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kwa mawazo yangu, nadhani mbinu ya kutisha watu imetumiwa kwenye chaguzi nyingi, mfano US wakati wa Bush watu walitishwa kuhusu kuvamiwa na magaidi kama hawatamchagua Bush etc. Cha msingi ni chama kinachotuhumiwa kucounter attach, nadhani machinery ya Chadema kwenye kampeni kupangua hoja haikuwa kali sana. CCM walijitahidi na mpuuzi wao kampeni Manager.

  Nadhani pia Chadema kukosa VP (Mgombea mwenza) makini na mshambuliaji imechangia

  Lakini lingine kubwa ni kukosa resources. Kama mtakumbuka Obama alimu outspent McCain kwenye election ads kwa mara tatu or so, na ililipa. CCM wamewaoutspent Chadema zaidi mara kumi etc.Chadema walikosa uwezo huo, especially kurudi sehemu ambayo wagombea wengine walimwaga sumu kwenda kuclear air. Ona jinsi alivyovuna Mbeya na Mwanza, kwani alirudi kuclear air, JK alifanya hivyo lakini it was too late Mwanza, Mbeya Silaa alifunga kampeni, akavuna sana.

  CCM ilimtumia Mama Kikweche kusambaza fedha na kanga kwa kina mama. Chadema haikuwa na mkakati mzuri wa kuwapitia wapiga kura wakina mama- (simaanishi kuwapa rushwa noo), hata kwenye mikutano ya Slaa waliokuwa wanaonekana kwa wingi ni vijana na wana ume

  Lakini kubwa ni idadi ya waliopiga kura, nadhani hiyo asilimia 42 si kweli, na si ajabu kura za wapinzani zilienguliwa na ili kuoanisha mahesabu, wanasema turnout ilikuwa ndogo. This time kulikuwa na stake kubwa kwenye huu uchaguzi, watu wengi walihamasika, ccm base na chadema base walikuwa fired up, so independets voters, kuliko mwaka 2005. 1995 watu walikuwa fired up but wengi walikuwa hawajajiandikisha kwani ujio wa Mrema ulikuja late.

  Na la mwisho ni ile dhana potofu ambayo bado ipo kwenye akili za Watanzania kuwa mpinzani hawezi kushinda kiti cha uraisi. Kuna hilo jeraha alilotuachia Nyerere kuwa upinzani wa kweli utatoka ccm. That is very true, Slaa ni zao la CCM, alitoka CCM kwa kuwa alishindwa, Shibuda etc. Watanzania wenye kupenda vyama vya siasa wote walikuwa CCM, kabla ya mfumo wa vyama vingi, So tayari wameshameguka, sasa sijui Wtz wanangoja imeguke block kubwa ndio iishinde ccm.
   
Loading...