Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

JAMANI HUKU BONGO NI USIKU SAA HIZI NAWAHI MSONDO NGOMA KUONA WANANCHI WAKIONYESHA TALENTS ZAO ZA SANAA, HA! HA! HA! USIKU MWEMA WENGINE SIWEZI KUWAJIBU MAANA HOJA ZENU HAZINA MASHIKO KABISAA, WENGINE MNAKUWA KAMA WATOTO WA CHEKECHEA BANA, HA1 HA! HA!
William.

Wakati wewe unaweza kwenda msondo ngoma kwa starehe, unawaambia watu wenye shida Wanakuwa kama watoto na wana argument za chekechea.

Halafu unacheka in capital letters, without saying " in a light touch", ni kukebehi na kudharau mamilioni ya watanzania wenye njaa, watanzania Wanaokufa na malaria, wakina mama wanaolala chini mawodini, wanaojifungua wakiwa wamesimama, watanzania wanaoshindwa kusomesha watoto wao vyuo vikuu kwa fedha za serikali, watoto wanaosoma kwenye vumbi shule za msingi, waalimu wasiolipwa, waganga wanaozalisha bila gloves, wakulima wanaokopwa mazao yao, wananchi wasio na maji salama, wazee wa Jumuiya ya afrika mashariki wanaodai haki zao.

Usidhani kuwa wote waliotajwa hapo juu na wengineo wote hawapendi kwenda msondo ngoma, hawana uwezo William.
 
KAMA WABUNGE WANAMAISHA MAGUMU, VIPI KUHUSU WANAOISHI DODOMA INAMAANA WAONGEZEWE MISHAHARA NAO.............ALAF PILI HAO WABUNGE WANAPENDA WENYEWE KUKAA GUEST HOUSES NA HOTELS COZ NYUMBA 300 ZIMEJENGWA PALE ENEO LA KISASA NJE KIDOGO YA MJI WALIPEWA KIPAUMBELE WAKAKATAA KWA KIGEZO NYUMBA ZIPO MBALI NA MJI, PILI HATA KAMA WATAISHI KWENYE NYUMBA ZAKULALA WAGENI BASI MBONA ZIPO ZA 25,000 MPAKA 40,000 NA ZINA HADHI NZURI SANA..............TATIZO LA WABUNGE WETU HUWA WAKIENDA DODOMA WANAPENDA SANA STAREHE NA PIA WAKIENDA WANABEBA FAMILIA NZIMA AS IF WANAHAMIA HUKO WAKATI PALE SANA SANA NENDA NA MKEO TU INATOSHA:faint:
 
- Wabunge ni tofauti sana na hao wengine, WAO NI WATUNGA SHERIA! sasa mwenye kutaka sheria mbovu kwa wananchi akiwapa rushwa na kutupitishia sheria mbovu kwa taifa utasema ni sawa na wengine serikalini?

William.
William hoja yako kwenye post kuu ni sawa, lakini hili la kusema wabunge ni tofauti na wengine kwakuwa wao wanatunga sheria hapa naomba nitofautiane na wewe. tatizo lililopo ktk jamii yetu kwa sasa ni la jamii nzima. ni kweli nchi nyingine wabunge wamepewa kipaumbele, lakini si kipaumbele kilicho waumiza wananchi wengine- hapana. hali ya maisha ya dodoma ni hali ya watu wote, wote haichagui. kumbuka kuwalipa wabunge hata millioni 1 kwa siku ni kuongeza tatizo na si kutatua tatizo kwa sababu zifuatazo
1. hao wanaowafuata kuomba misaada wataongezeka hata kuzidi nyongeza ya pesa
2. dodoma itakuwa na maisha magumu zaidi kwani bei ya kila kitu itapimwa kwa kipato cha mbunge
3. watumishi wa kawaida wa umma watashindwa kushiriki ktk kufanikisha vikao vya bunge kwani posho zao nazo ni hiyo elfu sitini na tano kwa siku

njia pekee ni kujenga na kukuza uchumi haya matatizo yatapungua. kumbuka hizo gharama za maisha dodoma ndo tunaita mfumuko wa bei- ni kosa kubwa kukabili mfumuko wa bei kwa kuongeza mshahara.

ushauri kwa wabunge:
waache kukopa ovyo, wengi baada ya ubunge wanakopa mno, bila hata kujua mzigo wa kuhudumia mkopo. tumeona hata walimu wa shule za msingi kwakuwa wao ni wa chini , hawana namna ya kuomba nyongeza ya posho, wanaishia kukimbia vituo vya kazi kwaaajili ya mikopo/madeni
ushauri kwa mabenki;
wazingatie sheria za mikopo, wasikopeshe bila kuzingatia kipato cha mbunge kwa mwezi
 
Ninasikia wewe umeishi NY miaka kadhaa na pia hakuna mtu aliyekuwa ankutegemea umtunze kule Bongo. Ushauri kama unapenda kuwa mwanasiasa wa kuwaletea maendeleo Watanzania au hata watu wa mkoa wa Dodoma - jipe assignment ya kutembelea vijiji na miji kwa kipindi cha miezi sita - tembelea mashule zungumza na walimu na wazazi, lala katika nyumba zao; tembelea mabwana na mabibi shamba, madaktari na vituo vya afya na wafanyakazi wengine; ongea na wakulima na wafugaji na wavuvi, nk. Baada ya kipindi hicho rejea hapa JF utetee wabunge kudai nyongeza ya posho! Kwa kungalia posho ya Tsh 200,000 au 400,000 kwa jicho la ki-New York au kiteule (wateule wa Tz ikiwa ni pamoja na mafisadi) itaonekana ni pesa ya kununulia kikombe ya chai! Lakini kwa kuiangalia kwa jicho la kitanzania (kwa watanzania halisi walalahoi) hiyo ni pesa ya ku-survive kwa zaidi ya nusu mwaka kama sio mwaka. :shock:
 
Nlichojiunza katika mjadala huu ni kwamba Kama ni kweli kuwa mbunge analipwa 80,000/= kwa kila siku (DSA) kila anapokuwa Dodoma aingie bungeni au la, 70,000/= kila anapohudhuria kikao kila siku, 50,000 za mafuta kila siku pamoja na mafuta ya kila mwezi lita 1,000(hata wakati wa bunge) hoja yako William juu ya ukali wa maisha Dodoma na hadhi ya mbunge iko wapi?. Mbona utakuwa unapotosha jamii ya watanzania?
 
nimesikitishwa na post ya malecela.
magamba yamemuathiri kijana, hana jipya.
--kijana endelea kuishi kwa father alishaweka mambo sawa.
ishu hapa ni mfumuko wa bei uliopelekea kupanda kwa gharama za maisha.
ccm shughulikieni suala la mfumuko, shilingi imeshuka, posho ikipanda ni directly proportional to kuongezeka kwa hizo bei za vyumba maana wafanyabiashara are there ku enjoy
 
- Wabunge ni tofauti sana na hao wengine, WAO NI WATUNGA SHERIA! sasa mwenye kutaka sheria mbovu kwa wananchi akiwapa rushwa na kutupitishia sheria mbovu kwa taifa utasema ni sawa na wengine serikalini?

William.

Kwahiyo kutunga sheria na delicate sana kuliko kutibu mgonjwa? kujenga miundombinu? kufundisha? nk nk? acha kujiandalia mazingira ya 2015
 
Nlichojiunza katika mjadala huu ni kwamba Kama ni kweli kuwa mbunge analipwa 80,000/= kwa kila siku (DSA) kila anapokuwa Dodoma aingie bungeni au la, 70,000/= kila anapohudhuria kikao kila siku, 50,000 za mafuta kila siku pamoja na mafuta ya kila mwezi lita 1,000(hata wakati wa bunge) hoja yako William juu ya ukali wa maisha Dodoma na hadhi ya mbunge iko wapi?. Mbona utakuwa unapotosha jamii ya watanzania?

Aswaa hayo ndiyo malipo yake. Zaidi kuna posho ya jimbo milioni 2, kuna mfuko wa jimbo (kiasi kinatofautiana, mbunge wangu anapata milioni 45), achilia mbali posho za safari mbali2 za wabunge. Malecela hawezi kuacha kutetea mapato yaliyomsomesha hadi hapo alipo
 
- Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.

- Serikali itafute suluhisho la hili tatizo kwa sababu ni tatizo, tunaawaacha wabunge in an open field ya kupokea rushwa, nimeona Wabunge wengine wakiishi sehemu ambazo ni very dangerous kwa kiongozi wa taifa tunayemtegemea kuishi, halafu unakuta magazeti yakifurahia mbunge apigwa mapanga, mbunge aibiwa, I mean as taifa we have to do something, nchi nyingi Duniani, infact hata Zambia tu Serikali imewajengea Special Hostel wabunge wake kwenye maeneo ya viwanja vya bunge kupunguza hili tatizo la posho, I mean kwa hali niliyoiona hili tatizo halikwepeki ni lazima lizungumzike.

- Nilichojifunza kule Dodoma ni kwamba wengi wa Wabunge waliokuwa wanapinga posho ni wale wenye uwezo mkubwa sana kipesa kwamba hata hawahitaji hiyo posho ya sh. 70,000 kwa siku maana kwao ni peanuts na ni wachache sana, ninasema hii hoja ijadiliwe tena, tunawaweka wabunge wengi pagumu sana kimaishana hata kutuongoza.

William John Samwel Malecela @DSM City!

Hizi ni fikra za mtu mlafi ambaye hapaswi kuaminiwa kupewa aina yoyote ya uongozi!

Kila mtu anajua unashadadia hizi posho ziwe kubwa because you are eyeing that mbunge position at some stage, kwa hiyo unapiga "tingatinga" sasa hivi ili kusawazisha mambo ili pindipo ukishaingia mjengoni mambo yawe rosy and sweet for you, huh? Yes, we know it - you aint fooling nobody!

By the way, unahitaji kuwa polished for yet another 10 years (i.e year 2022 and beyond) before you start dreaming of taking those high political posts. Lakini by then unatakiwa uwe tayari umejivua gamba na kuvaa kitu kingine (gwanda most probably kwani hopefully utakuwa umekuwa a lot less greedy baada ya kuwa polished).
 
WJM,
Naona unajiandalia mazingira mazuri ili nawe utakapoingia huko ukute posho kama za akina Lionel Messi, Nadal, C. Ronaldo,...! Kulikuwa na mradi kujenga nyumba zaidi ya 300 kwa ajili ya wabunge wetu pale Dodoma. Muulize Kashilila au Spika umekwamia wapi.
Unawakuza na kuwatukuza mno WANASIASA bila sababu ya maana. Kila mara unataka kuona wanasiasa wanapewa hadhi na heshima tofauti na WATANZANIA wengine sijui kwa lipi la maana. Unajua fika kwamba hali tuliomo kiuchumi, huduma za jamii duni sana, imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa madudu wanayofanya. Wakati baadhi yetu tunapambana SIASA isiwe AJIRA wala UWEKEZAJI wewe unakazania wazidi kuneemeshwa zaidi!
 
- Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.

- Serikali itafute suluhisho la hili tatizo kwa sababu ni tatizo, tunaawaacha wabunge in an open field ya kupokea rushwa, nimeona Wabunge wengine wakiishi sehemu ambazo ni very dangerous kwa kiongozi wa taifa tunayemtegemea kuishi, halafu unakuta magazeti yakifurahia mbunge apigwa mapanga, mbunge aibiwa, I mean as taifa we have to do something, nchi nyingi Duniani, infact hata Zambia tu Serikali imewajengea Special Hostel wabunge wake kwenye maeneo ya viwanja vya bunge kupunguza hili tatizo la posho, I mean kwa hali niliyoiona hili tatizo halikwepeki ni lazima lizungumzike.

- Nilichojifunza kule Dodoma ni kwamba wengi wa Wabunge waliokuwa wanapinga posho ni wale wenye uwezo mkubwa sana kipesa kwamba hata hawahitaji hiyo posho ya sh. 70,000 kwa siku maana kwao ni peanuts na ni wachache sana, ninasema hii hoja ijadiliwe tena, tunawaweka wabunge wengi pagumu sana kimaishana hata kutuongoza.

William John Samwel Malecela @DSM City!

jamani kwani unataka waishi maisha ya namna gani?hivi unajua ya kuwa kuna wananchi ambao wamewapigia kura hao unaowatetea lakini mlo wao wa siku ni issue?kaka shukuru umekuta neema kwenu,kuna watu ambao wanafanya kazi kubwa kuliko zao kwa ujira mdogo sana,wao walikubali kutumikia taifa watumike kwa hali yoyote ile anaona hawezi apige chini kuna watz kibao wanaweza fanya kazi hizo hakuna mtu ambaye amelazimishwa,unaacha kuwaonea huruma watz wanaoishi ktk mazingira magumu unawaonea huruma watu ambao wako ktk neema
 
Wamemtuma awasemee, kwasababu wanaogopa kuianzisha tena mbele ya wananchi!
MIMI NAISHI DODOMA HIYO HOTEL ALIOITOLEA MFANO HAWAISHI KABISA HAPO! HOTEL ZA MITAANI BEI YAKE NI 40000 yaani hiyo ndo ya juu. ASIWADANGANYE HUYO!
 
Kwanza William katumwa, pili William kazaliwa, kalelewa na bado analelewa na gamba ndiyo maana yeye kwa fikra zake alizorithi from gamba anaona hoteli ya 65,000/= per day ni ya hadhi ya chini wakati hotel ya 20,000/= per day ni nzuri na yenye hadhi kabisa.

Au anataka kutuambia mtu ukishakuwa mbunge unakuwa exceptional kiasi kwamba unatakiwa ukae kwenye hotel ya gharama. Je, ili iweje?

Hizo gharama unazosema zimepanda ni kwa wabunge tu au gharama za maisha kwenye huo mji wa Dodoma ni za juu sana na wanaokwenda hapo Dodoma ni wabunge tu hakuna mwananchi mwingine anayeishi hapo?
 
Uroho/ulafi ndiyo vinawasumbua magamba. Uongozi mmefanya ni deal ya kutmikia matumbo yenu badala ya kutumikia wananchi na Taifa kwa ujumla.
Jitahidini mwisho wenu wa dunia ya matumbo ulafi ikn around ze kona
 
kama hali ni ngumu kimaisha kuwa mbunge si waache watafute kazi zingine...kwani ni lazima wawe wabunge...kwanini mtu alipwe 70000 kwa siku kwa kulala bungeni kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Kama ni posho basi wabunge wawe wanalipwa kwa jinsi wanavyochangia maada bungeni...wale wanaosimama na kuchangia hoja wawe wanalipwa zaidi na wale ambao kazi zao ni kulala tu bungeni hawafanyi kazi yoyote walipwe less..hii ita motivate wabunge wawe wanaongea na kutoa maoni yao kuhusu vilio na malalamiko ya wananchi wao hapo bungeni na sio kusinzia na kupiga umbea, tunawaonaga sana kwenye TV.
 
Back
Top Bottom