Posho za Wabunge: Marupurupu ya Slaa kupanda?

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96
Nafahamu CDM inampatia katibu mkuu W. Slaa maslahi sawa na ya mbunge. Hii ni kutokana na makubaliano yaliyopelekea Slaa kuachana na ubunge na kupeperusha bendera ya CDM kwenye kinyang'anyiro cha urais 2010.

Ikiwa sasa kuna harakati za wabunge kujiongezea posho/marupurupu, je hii nayo itaenda automatically kwa Slaa pia?
 
No wonder Slaa hatoi tamko lolote la maana juu ya hizi posho!
 
Nafahamu CDM inampatia katibu mkuu W. Slaa maslahi sawa na ya mbunge. Hii ni kutokana na makubaliano yaliyopelekea Slaa kuachana na ubunge na kupeperusha bendera ya CDM kwenye kinyang'anyiro cha urais 2010.

Ikiwa sasa kuna harakati za wabunge kujiongezea posho/marupurupu, je hii nayo itaenda automatically kwa Slaa pia?

unautakia nini "! Unakuhusu nini! Umekosa la kufanya?
 
chadema 'Investment comp.ltd'
Hatimaye kampuni ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema inayomilikiwa na Mzee Edwin Mtei ,Freeman Mbowe,Philemon Ndesamburo na Kabila la wachaga kutoka machame kimefanya uteuzi wa viongozi wake na kumteua Freeman Mbowe kuwa mkurugenzi Mtendaji............

source gazeti la sauti huru 01/02/2012
 
Nafahamu CDM inampatia katibu mkuu W. Slaa maslahi sawa na ya mbunge. Hii ni kutokana na makubaliano yaliyopelekea Slaa kuachana na ubunge na kupeperusha bendera ya CDM kwenye kinyang'anyiro cha urais 2010.

Ikiwa sasa kuna harakati za wabunge kujiongezea posho/marupurupu, je hii nayo itaenda automatically kwa Slaa pia?

Hii thread imekaa kishabiki zaidi ya thread zote nilizopata kuziona ...
Imebidi nicheke sana kwa kuwa ni jamba ambalo sikuwahi kufikiria.Kweli this is da homu of great thinkaz! haa haa haaa
 
huh,mna bifu nini na mchungaji wetu wa Assemble of god Tanzania Limited.?
Huyu mchungaji gani? Kilaza tu, kama wachungaji ndio mmavurumisha mitusi hivyo, mnaiba wake za watu ambao hawajatalikiwa, basi x-tianity should be abandoned!

Bumpkin Billionare,
Umetumia nguvu kubwa sana na workdone yako ni zero! Ni kama tu umesukuma ukuta...mbona umejibu vichache tu? Umeona mitusi ya mchungaji wako?
 
Slaa amvaa JK


na Tamali Vullu


amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoa tamko iwapo ameridhia wananchi waendelee kufa kwa kukosa huduma za afya kwa kukataa kuwaongezea posho madaktari huku akiidhinisha posho ya sh 330,000 kwa siku kwa wabunge.
Amesema Rais Kikwete amekuwa mgumu kuongeza posho kwa watu wanaotoa huduma muhimu kama madaktari na walimu, lakini amekuwa mwepesi kwa wanasiasa ambao hukaa kimya bungeni na wengine kuishi kupiga makofi.
Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima, kwa njia ya simu. Dk. Slaa alisema iwapo Rais Kikwete hatatoa tamko kuhusu suala hilo, CHADEMA itayatumia majukwaa kuwaeleza wananchi.
Alisema CHADEMA imekuwa ikilaumiwa kwa kuishtaki serikali kwa wananchi kila inaposhindwa kuwajibika lakini hivi sasa hawatakali wala kuogopa lawama hizo kwakuwa hazina msingi.
"Sasa imetosha. Rais Kikwete atoe tamko kama ameidhinisha wananchi waendelee kufa kwa kugoma kupandisha posho ya sh 10,000 kwa madaktari na kuwaongezea wabunge. Hivi anataka nchi iendelee hivi hadi lini?" alihoji.
Alisema kuwa madaktari wengi nchini wanafanya kazi katika mazingira magumu huku wakihatarisha maisha yao kutokana na kuwapo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa, lakini serikali haiwajali kwa kiwango inachowajali wanasiasa.
Alibainisha kuwa serikali inapaswa kulaumiwa kwa hali inayoendelea sasa nchini kwa wananchi kufa kutokana na kukosa huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini.
Aliongeza kuwa mgomo wa madaktari umeonyesha kuwa serikali imekosa umakini katika vipaumbele vyake na hivyo kuwafanya wananchi waishi maisha ya taabu kila kukicha.
"Rais Kikwete alipaswa kukaa chini na kuziongezea posho kada zote … sasa hakuna uwiano, jambo ambalo ni hatari kwa nchi. Mwaka 2007 niliwahi kusema bungeni kuwa kuna bomu litalipuka, Pinda (Waziri Mkuu, Mizengo Pinda) alikataa," alisema.
Juzi, Waziri Mkuu alikaririwa akisema kuwa Rais Kikwete ameidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka sh 70,000 hadi sh 200,000 kwa siku.
Kuidhinishwa kwa posho hiyo kunafanya sasa mbunge kupokea sh 330,000 kwa siku. Sh 200,000 ikiwa ni posho ya kikao, sh 80,000 posho ya kujikimu na sh 50,000 nauli.
Pinda alitoa taarifa hiyo katika kikao cha utangulizi cha wabunge ambako inaelezwa kuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), na mbunge wa Bumbuli, January Makamba (CCM) walipinga suala hilo.
Mjadala wa kupanda kwa posho hizo umeligawa taifa tangu kuibuliwa kwake huku baadhi ya makundi yakipinga ongezeko hilo.
Jana Spika wa Bunge, Anna Makinda, alisema posho hizo mpya zimeanza kulipwa kuanzia jana baada ya kupitishwa na ngazi zinazohusika.

 
We mtoa hoja ataongezewa times two ya 330000! C ndo what u want to hear or? Hutaki hama nchi mpendwa tena hamia kenya nikutafutie passport!!
 
naomba niweke kumbukumbu sawa kuwa dr slaa huyohuyo ndiye mtu wa kwanza kupgania juu ya posho kubwa za wabunge hata kabla hazjaongezwa.

Umenifunguwa masikio, sasa nnaelewa kwanini Zitto anapinga sana posho. Ni vita ya kisaikolojia ya nani zaidi!
 
Back
Top Bottom