chokambayaa
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 543
- 69
Dovutwa alisema kwa kawaida posho ya kujikimu inalipwa kwa mtumishi anapokwenda nje ya kituo chake cha kazi na kwamba kitendo cha kuwalipa posho wabunge wanapokuwa mjini Dodoma ni cha ubadhirifu.
Alisema Dodoma ndiyo kituo cha kazi za wabunge na kwa hiyo hakuna sababu ya kuwalipa posho ya kujikimu.
Alisema anakusudia kutafuta usahihi wa jambo hilo kabla ya kuamua kuchukua hatua za kisheria."Hoja yangu ni viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza taasisi na idara za umma, kuhusika katika hujuma za ubadhirifu na ufisadi huo, maana wakati mwingine inakuwa vigumu kuhoji kutokana na kuwa tuhuma zenyewe zinafanyika baada ya kubarikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni," alisisitiza.
Hapo keshachukua hela zakeHapa kwenye kifungu cha posho za vikao lazima kukomalia, wanachofanya ni wajibu na wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi zao, iweje tena walipwe posho za vikao wakati ni majukumu ya kazi yao. Wizi huu haukubaliki kamwe.
Yaani kwa mtazamo wangu 90% ya waheshimiwa wanapigania kuingia bungeni
Kwa minajili ya kujipatia/kuboresha maisha yao binafsi, hawana nia ya dhati kulikomboa taifa letu na umasikini uliokithiri
Mfano leo sheria ikipitishwa kupunguza posho/maslahi ya waheshimiwa hao (m. 12 per month) thubutuuu!!!!!!!!!! Hutaona tena ubunge ukifukuziwa kwa kutumia nguvu nyingi kama sasa
Wana wa janvini, hili mwalionaje?
Are there for its own curiosity or for the nation interests??eep:
Ukishajua itakusaidia nini mdogo wangu? Unataka kuwakaba mnadani? Tulia kula nguru yako na mchunga.
Slaa mwenyewe alijifanya kupigia kelele mshahara wa wabunge upunguzwe, alipo pata ukatibu mkuu akawalazimisha CHAKushindwa wamlipe kama mbunge, na kwanza kupinga hii hoja yako atakuwa Slaa. Na anae bishia hili basi huyo ni mwenda wazimu kabisa, abishe tu ili tumjue sasa
kama sikosei per diem ni Tsh 200,000/= na mshahara ni Tsh 8,500,000/= kama nimekosea figure naomba mnirekebishe.