Posho na Mishahara ya wabunge...

chokambayaa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
543
69
Yaani kwa mtazamo wangu 90% ya waheshimiwa wanapigania kuingia bungeni kwa minajili ya kujipatia/kuboresha maisha yao binafsi, hawana nia ya dhati kulikomboa taifa letu na umasikini uliokithiri

Mfano leo sheria ikipitishwa kupunguza posho/maslahi ya waheshimiwa hao (m. 12 per month) thubutuuu!!!!!!!!!! Hutaona tena ubunge ukifukuziwa kwa kutumia nguvu nyingi kama sasa.

Wana wa janvini, hili mwalionaje?

Are there for its own curiosity or for the nation interests??

:peep:
 
Poleni na kazi wana JF.
Mimi nahitaji kujua wabunge wanalipwa kiasi gani kwa siku? sitting allowance na per dm.
Je ni kweli wanastahili hicho kiasi?
 
Ukishajua itakusaidia nini mdogo wangu? Unataka kuwakaba mnadani? Tulia kula nguru yako na mchunga.
 
kama sikosei per diem ni Tsh 200,000/= na mshahara ni Tsh 8,500,000/= kama nimekosea figure naomba mnirekebishe.
 
Dovutwa ajiandaa kupinga posho za wabunge

Thursday, 03 March 2011
Joyce Mmasi


MWENYEKITI wa Chama cha UPDP, Faham Dovutwa, anajiandaa kupinga alichokiita ubadhirifu na ufisadi wa kitaasisi, unaofanywa na Bunge kwa kulipa posho za kujikimu kwa wabunge wanapokuwa katika vikao vyao mjini Dodoma.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Dovutwa alisema utaratibu wa kuwalipa posho za kujikimu wabunge wanapokuwa mjini Dodoma, ni makosa na ubadhirifu wa fedha za walipa kodi.Alisema wabunge hawastahili kulipwa fedha hizo kwa sababu wanalipwa mishara yao kwa kazi hiyo.

"Wabunge wanalipwa mishahara ya kila mwezi kama watumishi wa eneo lolote na miongoni mwa kazi zao ni wanazifanyia mjini Dodoma, sasa inashangaza wanapolipwa posho za siku huku wakiwa wanalipwa mishahara yao," alisema Dovutwa.

Dovutwa alisema kwa kawaida posho ya kujikimu inalipwa kwa mtumishi anapokwenda nje ya kituo chake cha kazi na kwamba kitendo cha kuwalipa posho wabunge wanapokuwa mjini Dodoma ni cha ubadhirifu.

Alisema Dodoma ndiyo kituo cha kazi za wabunge na kwa hiyo hakuna sababu ya kuwalipa posho ya kujikimu.

Alisema anakusudia kutafuta usahihi wa jambo hilo kabla ya kuamua kuchukua hatua za kisheria."Hoja yangu ni viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza taasisi na idara za umma, kuhusika katika hujuma za ubadhirifu na ufisadi huo, maana wakati mwingine inakuwa vigumu kuhoji kutokana na kuwa tuhuma zenyewe zinafanyika baada ya kubarikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni," alisisitiza.

 
Dovutwa alisema kwa kawaida posho ya kujikimu inalipwa kwa mtumishi anapokwenda nje ya kituo chake cha kazi na kwamba kitendo cha kuwalipa posho wabunge wanapokuwa mjini Dodoma ni cha ubadhirifu.

Alisema Dodoma ndiyo kituo cha kazi za wabunge na kwa hiyo hakuna sababu ya kuwalipa posho ya kujikimu.

Alisema anakusudia kutafuta usahihi wa jambo hilo kabla ya kuamua kuchukua hatua za kisheria."Hoja yangu ni viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza taasisi na idara za umma, kuhusika katika hujuma za ubadhirifu na ufisadi huo, maana wakati mwingine inakuwa vigumu kuhoji kutokana na kuwa tuhuma zenyewe zinafanyika baada ya kubarikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni," alisisitiza.

Hoja ya Dovutwa ina mashiko ila tatizo ni kuwa hata hizi mahakama ziko huru kiasi gani kujiamini na kutenda haki...................kama Bunge likishindwa kitakachofanyika ni kuhamishia posho hizo kwenye mshahara ili kukidhi haja za kisheria..............posho hukatwa kodi lakini mshahara haukiatwi kodi kwa hiyo hii ikawa ni neema nyingine kwa wabunge wetu ya kutolipa kodi.................au kulipa zaidi.........................kama posho ndizo zisizolipiwa kodi...................


Juzi juzi tu Anne makinda ametetea hoja ya kuwa posho hizo anajua hazitoshi lakini zisiwe chanzo cha kudai posho kemukemu kutoka taasisi nyingienzo za umma ambazo kamati za Bunge inazisimamia...................
 
KAMA Kambi ya Upinzani Bungeni ingepewa fursa ya kuwasilisha Makadirio na Matumizi ya Serikali katika mwaka wa fedha wa 2011/12, basi katika mapendekezo yake ingetaka posho zote za vikao kwa watumishi wote wa umma wakiwamo wabunge zifutwe. Hiyo imebainika katika maoni yake ya Bajeti ambayo yanayotarajiwa kusomwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo Juni 8 bungeni Dodoma. (..........)

Kambi hiyo imesema ingependekeza pia kupunguzwa kwa bei ya mafuta kwa asilimia 40 ikiwa ni harakati za kumpunguzia mzigo wa maisha mwananchi wa kawaida. Akiwasilisha vipaumbele vya bajeti hiyo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha na Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo upande wa Fedha, Christina Lissu, alisema lengo la kufuta posho za vikao ni kupunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima.

“Posho hizi kwa sasa ni nyingi na wakati mwingine wahusika hulipwa fedha nyingi kuliko hata mishahara yao. Sasa sisi tumeona kwa nini umlipe mtu fedha nyingine wakati akiwa kwenye vikao vya kazi, ambayo ni sehemu ya kazi na mshahara, haya ni matumizi mabaya ya fedha,” amesema Christina. (.......)

Alisema, pia itahakikisha inapanua wigo wa kodi kwa kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 20 ya Pato la Taifa. Kwa sasa Serikali inakusanya mapato kwa asilimia 16 ya pato hilo, kuongeza wigo kwa walipa kodi na kupunguza msamaha wa kodi hadi asilimia moja kutoka 4.5. Kwa upande wa kodi, bajeti hiyo imeonesha kuwa kampuni zote ambazo Serikali ina hisa zitatakiwa zijisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, ili kuiwezesha Serikali kuuza na kununua hisa na kuongeza mapato yake, ikiwa ni pamoja na kuweka sheria kali ya kuzuia ukwepaji kodi kwa mashirika makubwa.

Christina pia alitaja vipaumbele vingine vya bajeti hiyo kuwa ni pamoja na kipaumbele namba moja cha miundombinu, akisisitizia ujenzi wa barabara zote, kuboresha reli ya kati, bandari na kufufua Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATC). Aidha, alisema kipaumbele kingine ni umeme kupitia uzalishaji wa makaa ya mawe ambao utazalisha megawati 1,500 kutoka migodi ya Mchuchuma, Ngaka na Kiwira na gesi itakayozalisha megawati 300 kutoka Mtwara, Dar es Salaam hadi Mwanza, ikiwa ni njia ya kupunguza utegemezi wa vyanzo vya maji.

Vipaumbele vingine ni kuwezesha ukuaji wa sekta za uzalishaji na hasa ukuaji wa uchumi vijijini, maendeleo ya rasilimaliwatu kwa kuwekeza kwenye elimu na afya, ambapo kwa upande wa elimu, kodi ya uendelezaji ujuzi theluthi yake itabaki kwenye Bodi ya Mikopo badala ya kwenda Hazina.

Alivitaja vipaumbele vingine kuwa ni kuimarisha utawala bora kwa kuanzisha ofisi ya kushughulikia mafisadi wakubwa ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kuimarisha usimamizi wa mashirika ya umma.

Habari Leo
 
Hapa kwenye kifungu cha posho za vikao lazima kukomalia, wanachofanya ni wajibu na wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi zao, iweje tena walipwe posho za vikao wakati ni majukumu ya kazi yao. Wizi huu haukubaliki kamwe.
 
Hapa kwenye kifungu cha posho za vikao lazima kukomalia, wanachofanya ni wajibu na wanalipwa mishahara kwa ajili ya kazi zao, iweje tena walipwe posho za vikao wakati ni majukumu ya kazi yao. Wizi huu haukubaliki kamwe.
Hapo keshachukua hela zake
 
Bajeti kivuli ya upinzani yaweza kuwa ya kumuokoa mtanzania lakini je magamba wana nia ya dhati kumuokoa mtanzania ili angalau wakubaliane na hoja kama hiyo ya kuondoa posho?
 
Its an alternative thinking. Keep it Up. from 2015, we have people who woll lead this country.

May God of Heven, of Ibrahim, Isack and Jacob bless all those who think critically how to improve Tanzanian's lives. :A S-rose:
 
Wakati wafanyakazi wa kawaida wanalipwa shilingi laki tatu tatu kwa mwezi wao wanazipata kwa siku mbili.kama kuna mikataba mibovu,kanuni za kubana kashfa /tuhuma watawezaje kuwatetea wananchi wakati tayari hizo posho ni kiziba mdomo.wao walitakiwa wawe wa kwanza katika kuwatetea watanzania,lakini hali ilivyo ni tofauti.yote haya yana mwisho
 
Yaani kwa mtazamo wangu 90% ya waheshimiwa wanapigania kuingia bungeni
Kwa minajili ya kujipatia/kuboresha maisha yao binafsi, hawana nia ya dhati kulikomboa taifa letu na umasikini uliokithiri


Mfano leo sheria ikipitishwa kupunguza posho/maslahi ya waheshimiwa hao (m. 12 per month) thubutuuu!!!!!!!!!! Hutaona tena ubunge ukifukuziwa kwa kutumia nguvu nyingi kama sasa
Wana wa janvini, hili mwalionaje?
Are there for its own curiosity or for the nation interests??:peep:

Slaa mwenyewe alijifanya kupigia kelele mshahara wa wabunge upunguzwe, alipo pata ukatibu mkuu akawalazimisha CHAKushindwa wamlipe kama mbunge, na kwanza kupinga hii hoja yako atakuwa Slaa. Na anae bishia hili basi huyo ni mwenda wazimu kabisa, abishe tu ili tumjue sasa
 
Ukishajua itakusaidia nini mdogo wangu? Unataka kuwakaba mnadani? Tulia kula nguru yako na mchunga.

Tunahitaji kujua ili tuone kama kweli wapo bungeni kwa maslahi ya wanyonge au kwa sababu kuna mishahara minono! Maprofesa wanakimbia vyuo vikuu kwenda bungeni, ma-RC wanakimbilia bungeni, huko kuna nini? Enzi za mwalimu mshahara wa waziri ulikuwa sawa na mshahara wa RC na mshahara wa mbunge wa kawaida ulikuwa sawa na mshahara wa DC, leo hali ikoje? Kupigana vikumbo kwenda bungeni kunatufanya sisi wananchi tujue kinachowapeleka huko bungeni, Wapo wabunge kwa nia ya dhati kabisa wanahitaji kusaidia wananchi wao lakini wengi wanafuata maslahi binafsi.
 
Slaa mwenyewe alijifanya kupigia kelele mshahara wa wabunge upunguzwe, alipo pata ukatibu mkuu akawalazimisha CHAKushindwa wamlipe kama mbunge, na kwanza kupinga hii hoja yako atakuwa Slaa. Na anae bishia hili basi huyo ni mwenda wazimu kabisa, abishe tu ili tumjue sasa

Tuwe wapana katika uchambuzi wa masuala ya taifa na mtu binafsi. Unapopigania haki katika jamii na kuielewa jamii na matatizo yake unatakiwa uwe ndani ya jamii hiyo ili ujifunze na kushuhudia yatokanayo. Hoja ya kudandia fulani mbona hakuacha kupokea mshahara haina mshiko kwa vile jambo linalopiganiwa si mtu ila system irekebishe kuhusu mafao ili kufikira huduma nyingine za kijamii.
 
Hivi kwanini mnapenda kuyeyusha mambo ya maana?....nionyesheni sehemu ambayo bajeti kivuli itatoa elimu bure mpaka kidato cha sita.
 
Tunakubali mfumo wa uonevu na kinyonyaji ambao kwa sababu tu ya ujinga wa wananchi na wafanyakazi wa kawaida wamejengewa woga na unafiki unaowafanya washangilie viongozi wanaowanyonya.

Si haki hata kidogo kwa Wabunge na viongozi wengine wa serikali kulipwa mshahara pamoja na posho zingine jumla ikiwa zaidi ya milioni 10 wakati walio wengi mshahara hauzidi laki tano.

Cha kusikitisha ni kwamba hao hao wanaolipwa chini ya laki tano kwa mwezi ndio watetezi wakubwa wa viongozi na wabunge hao. Kama wewe ni mmoja wa hao wasioliona tatizo hapa, basi wewe ni miongoni mwa mazuzu yanayoshangilia kifo chao wenyewe.

Hatuwezi kuendelea kama wanananchi na wafanyakazi wa kawaida ambao ndio walipa kodi ambayo inatumika kuwalipa wateule wachache watabaki na mawazo duni namna hii ambayo tunaweza kuyaita ya kitumwa katika nchi yao wenyewe.

Ni muhimu kupunguza tofauti kubwa iliyopo kati ya mapato ya waheshimiwa hao na wafanyakazi wa kawaida vinginevyo huko tuendako uheshimiwa utatafutwa kwa mtutu wa bunduki kwani kila mmoja atataka awe kwenye nafasi hizo.
 
Nimevutiwa sana na pendekezo la wabunge wa CHADEMA kuwa posho ya vikao ifutwe ili pesa zipelekwe katika kuboresha huduma za jamii.
Huo ni uzalendo wa hali juu kwa waheshimiwa wabunge katika kipindi hiki ambacho taifa letu linapitia katika mawimbi makubwa ya kuwepo kwa matatizo ya kiuchumi na kijamii.

Nachukua fursa hii kuwaomba waheshumiwa wakiongozwa na ZITO waepuke kupokea posho za vikao katika bunge la bajeti na pesa husika zifunguliwe mfuko maalum kwa kusaidia jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. Kama tujuavyo wawapo DODOMA wabunge wetu wanapata posho za aina 2; za vikao na kuishi, hivyo living allowanze waendelee kupokea ili jioni waonekane PAKO NI PAKO na viwanja vingine. ILA SITTING ALLOWANCE WAIEPUKE.

Kuchezwa kwa ngoma, kuanzishwa na mpigaji!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom