Posho bandari laki tano kwa siku!

Posho bandari laki tano kwa siku!

Tena hawa hawa walishiriki mkutano wa BMK ambako walikuwa wakilipwa shilingi laki tatu kila kila siku, huku kamati ya akina chenge ikielezwa kulipwa shilingi laki tano kwa kila mjumbe wa kamati hiyo ya uandishi wa katiba.

wakati hayo yakiendelea napendekeza pia kuwepo na kamati maalum ya bunge kwa ajili ya kukagua hesabu na shughuli za bunge ili pia tuweze kusikia ufisadi unaofanyika upande huo kwani kwa mfumo wa nchi hiii hao wanaopiga kelele inawezekana nao sio wasafi kama wanavyotaka kuonekana.

SiwatetePA lakini tutajua zaidi wai Tnaolipwa hizo poshon i wajumbe wa Bodi au wafanyakazi? kama ni wajumbe wa bodi wanakutana mara ngapi kwa mwaka ili kusaini hizi posho? hawa wajumbe wanalipwa mishahara? Je malipo yao ni zaidi ya wajumbe wa bodi nyingine kama vile NSSF, TANAP n.k?

Nafikiri tu!

Menejimenti na Bodi ilipitisha viwango vya safari ambavyo ni Sh 500,000 kwa kada ya juu na Sh 125,000 kwa kada ya chini na ambavyo TPA walianza kuvitumia bila kupewa kibali tangu mwaka 2011 hadi Januari 1 mwaka huu.

Tuwe tunasoma post jamani....
 
laki tano kwa siku? duh, hiyo hatari wakati walimu wanalipwa laki mbili kwa mwezi na wanaishi vizuri tu

Muongozo wa utumishi wa umma unasema kwamba posho ya kujikimu ya juu kwa watumishi wa serikali na Taasisi zake na Tsh 80,000/- @ day kwenye majiji na Tsh 65,000/- @ day kwenye miji.

Je hii, TPA sio Taasisi ya umma? Kwanini wao wawe na posho tofauti na Taasisi nyingine. Au hawa wenzetu wa TPA wanakwenda kwenye miji mingine ambayo wafanyakazi wengine wa umma hawaendi.

Kama Posho ya Tsh 80,000/- and 65,000/- @ day respectively haitoshi, basi haitoshi kwa Watumishi wote wa umma sio TPA peke yao.

Lakini pia from Tsh 80,000/- to Tsh 500,000/- @ day, sioni justification yeyote ile.
 
Mdogo wangu alipata bahati ya kupata kazi chuo cha bandari pale Tandika 2012.wakati mwaka wa masomo 2012/13 unaanza kiliitwa kikao cha kuwatambulisha walimu wote wapya kilichodumu kama 30 mins,baada ya kutoka pale kila mtu alipewa bahasha ya posho kuangalia ina laki tano taslimu.
Ilibidi Dogo arudi kwa cashier kuuliza labda walikosea maana yeye alihisi wamemtega maana alishaambiwa Bandar kuna fitna sana.cashier akamwambia ndio utaratibu.
 
Da mwalimu ukisafiri, au posho yoyote ni 32,500/=
 
Nchi hii sasa imepoteza muelekeo kwa namna wanasiasa wanavyotafuta umaarufu kijinga. Mfanyakazi aliyetumwa kazi na kulipwa posho ya safari ana adhibiwa kwa kosa gani? Anayetakiwa kuadhibiwa au kuwajibishwa kwenye hili ni kiongozi(management) aliyeidhinisha malipo na utaratibu bila kufuata kanuni. Wabunge waliokuwa wanadai na wanalipwa malaki ha shilingi wanawezaje kuona kiwango cha malipo kuwa ni kikubwa hadi kuagiza ulinganifu na kinacholipwa kwenye mashirika mengine? Huu ni ubinafsi uleule uliwafanya wabunge wajiite "waheshimiwa" na sio Ndugu. Wandugu tusikubali kupigiwa nyimbo za kiijinga na kutegemewa kucheza.
 
Hivi kweli ubinafsi unawafanya PAC WASHINDWE kusifia mwajiri anayelipa vizuri na kuwafanya waajiri wengine wafuate mfano huo? Hivi wanapodai mishahara iongezwe wanategemea itaanzia wapi? Ukishaanza kuonea wivu wenzio waliopata zaidi yako tena kwa kufanya kazi ujue wewe ni mchawi uliyekosa vitendea kazi
 
Hii kamati ya zito naipenda sana kwaufanisi ilasasaa naona kazizao kufichua maovu nakuachiahapo,,kuna halmashauiri. Ooo zimeiba mabilion tanga waliiba mpaka cag akadai atafwatilia wanaishoa kuhamishwa sehem,u za kazi wahusika awalipi then tukae kimya tu mpakayesu atakapprudi mnapotangaza hivi mnaongeza hasira kwa wananchi nawanqpojua akuna kinachofwata wanawawekea wivu nahasira na nyie tena....
 
Hivi kweli ubinafsi unawafanya PAC WASHINDWE kusifia mwajiri anayelipa vizuri na kuwafanya waajiri wengine wafuate mfano huo? Hivi wanapodai mishahara iongezwe wanategemea itaanzia wapi? Ukishaanza kuonea wivu wenzio waliopata zaidi yako tena kwa kufanya kazi ujue wewe ni mchawi uliyekosa vitendea kazi

Bandari ni mafisadi, hakuna kitu pale ni wizi tu, matangazo gani yanagharimu bilioni 6
 
WAKATI Msajili wa Hazina amebariki posho mpya za safari za ndani kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kuwa Sh 500,000 kwa siku kuanzia Januari 2, mwaka huu, imebainika kuwa walishaanza kulipana hivyo tangu mwaka 2011.

Hayo yalibainika jana wakati wa Kamati ya Bunge Hesabu za Serikari (PAC), ilipokutana na Menejimenti ya TPA jijini Dar es Salaam.

Kutokana na kamati hiyo kubaini posho hizo, zilianza kutumika hata kabla ya kupitishwa, imeiagiza Menejimenti ya TPA kuhakikisha wafanyakazi wote waliolipwa viwango vipya vya malipo ya safari kabla ya kuruhusiwa na Msajili wa Hazina wanazirejesha.

Agizo hilo la kurejeshwa kwa fedha za posho, limetolewa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, aliyesisitiza kuwa ni makosa kwa taasisi kuanza kutumia viwango vipya vya safari kabla ya kupewa kibali na Msajili wa Hazina.

Aidha, PAC imemuagiza Msajili wa Hazina kuhakikisha anafanya ukaguzi wa haraka kuangalia kama viwango kwa ajili ya safari vikoje na kuweka uwiano wa viwango vya safari kwenye mashirika mengine ya umma.

PAC pia imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu katika matumizi tata ya Sh bilioni 26.

Matumizi hayo ni Sh bilioni 9.6 zilizotumika kwenye mkutano moja wa wafanyakazi, Sh bilioni 6.4 zilizotumika kwa ajili ya matangazo, Sh bilioni 10 zilizotumika kwenye safari na Sh bilioni 43 kwa ajili ya manunuzi ya dharura.

Kwa mujibu wa agizo la PAC, wafanyakazi hao watalazimika kulipa fedha hizo kuanzia mwaka 2011 hadi Januari Mosi, mwaka huu, yaani siku moja kabla Msajili wa Hazina hajatoa kibali kubariki posho mpya Januari 2 mwaka huu.

Menejimenti na Bodi ilipitisha viwango vya safari ambavyo ni Sh 500,000 kwa kada ya juu na Sh 125,000 kwa kada ya chini na ambavyo TPA walianza kuvitumia bila kupewa kibali tangu mwaka 2011 hadi Januari 1 mwaka huu.

Viwango vya awali vilikuwa ni Sh 270,000 kwa ngazi ya juu na Sh 94,000 kwa kada ya chini.

“Ninawaagiza kuhakikisha wale wote walionufaika na viwango vipya vya safari kabla ya vibali kutolewa, kuhakikisha wanarudisha fedha hizo za umma, mtatafuta njia ya kuhakikisha wafanyakazi hao wanarejesha na hata kama ni kukatwa kwenye mishahara,” alisema.

Aidha, Zitto alisema: “ Nifikishieni salamu kwa (Lawrence) Mafuru (Msajili wa Hazina) kuhakikisha mnafanya ukaguzi wa haraka kwenye mashirika mengine kama Ewura, LAPF, NSSF na mengine kuangalia viwango vya safari wanavyolipana na ili kuweka usawa na kwenye mashirika.” Aidha, Menejimenti ya TPA ililiambia Bunge kuwa watahakikisha mamlaka inatumia mfumo wa kisasa katika mahesabu na shughuli nyingine.

“Tulikuwa tunatumia mfumo wa kizamani ambao ulikuwa na matatizo lakini sasa tunataka kununua mfumo mpya wa ERP ambao pia hutumiwa na hata bandari za nchi zingine,” alisema Meneja wa Tehama, Phares Magesa.

Hatua hiyo ya kutaka kufungwa kwa mfumo wa kisasa wa kielektroniki katika hesabu na shughuli za bandari, unatokana na ripoti ya CAG kubainisha kutokuwapo kwa nyaraka zinazothibitisha matumizi kutokana na mahesabu kufanywa kwa mkono.

Katika ripoti hiyo, kwenye fedha zilizotumiwa kwa ajili ya mikutano ya wafanyakazi, zaidi ya Sh bilioni 600 hazina nyaraka ya matumizi yake na kwenye hoja ya matumizi ya matangazo Sh milioni 384 zimekosa nyaraka za matumizi yake.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande alisema uongozi wake umeweza kubadilisha sheria ambazo zilikuwa zikitoa mwanya kwa mkurugenzi kuidhinisha fedha zaidi ya bajeti na kwa kufanya hivyo, wameweza kupunguza matumizi kwa asilimia 30.


CHANZO:
Habari leo

Hakika mwisho wenu unakuja, wa kulia na kusaga meno. Days are counted, where we shall pray and act.
 
Hivi kweli ubinafsi unawafanya PAC WASHINDWE kusifia mwajiri anayelipa vizuri na kuwafanya waajiri wengine wafuate mfano huo? Hivi wanapodai mishahara iongezwe wanategemea itaanzia wapi? Ukishaanza kuonea wivu wenzio waliopata zaidi yako tena kwa kufanya kazi ujue wewe ni mchawi uliyekosa vitendea kazi
 
hii ndo tz yetu wakati vijana wetu wanakosa hela za kujikimu udom wangine wanajilipa laki 5 kwa siku
 
Hii nchi inasikitisha kila mwenye kijinafasi mwizi! NANI ATAKAEKOMBOA TAIFA HILI?

Hajazaliwa bado! Labda tusubiri vizazi vijavyo. Hata wapinzani nao wamekuwa BUTU, hakuna anayewaogopa tena kwa vile nao Kauli na Nyendo zao si safi ambapo ni kinyume na matarajio yetu.
 
Hii sasa kero hongereni Zitto na kamati yako kwa kufichua huu ufisadi.
 
Bandari ni mafisadi, hakuna kitu pale ni wizi tu, matangazo gani yanagharimu bilioni 6
Nimezungumzia Suala la malipo wanayopewa wafanya kazi. Ubadhirifu kwa njia ya mikataba mibovu ni jambo linalotakiwa kuibuliwa katika ukaguzi ambayo ni kazi ya kitaaluma. Wanachofanya wanasiasa ni kuingilia taratibu za ndani wakati walitakiwa kuishia katika kutathimini mfumo katika ngazi za kisera
 
Back
Top Bottom