Posho bandari laki tano kwa siku!

Posho bandari laki tano kwa siku!

Posho ya Dereva na wafanyakazi wa chini ni sh.94,000 hapo TPA; bado kuna watu hawaona kuna kila sababu ya public sector cap. Posho as a reward system is becoming a problem na matatizo haya yapo sehemu yenye vyanzo vya mapato tu.

Yote tisa waliponiacha hoi ni pale jamaa wao alipoulizwa alete rekodi ya posho za awali hili walipe kwa sababu wameanza kujilipa kabla ya ridhaa ya serikari; majibu yake basi eti anadai ajui kwakuwa rekodi azikai kwenye electronic database na mafaili hayaonekani.

Haki ya mungu upuuzi huo unaweza fanywa Tanzania tu, sasa kama mkaguzi wa mahesabu ya serikari anakuja bila ya taarifa unamuonyesha nini na kama huna rekodi unaweza baki vipi kwenye kazi, is it allowed maana clearly there are elements of fraud. Ni vitu vya ajabu watu wameanza kulipana posho miaka miwili kabla halafu wanasema rekodi hawana si kutakuwa na entries on previous accounts records za public; ziko wapi au huyo CAG anakagua nini kwenye matumizi ya shirika.

In other words their lame excuse of not having the records implies sio sisi tu raia ndio wapuuzi hata huyo mkaguzi nae ni wakutiliwa wasiwasi uwezo wake kama unapewa sababu hizo na bado wakaona kuna sababu ya watu kubaki katika nafasi zao; kwakweli sisi bado sana.

Embu Star TV watuhurumie warudi hewani kwenye Internet tu-enjoy kuwaangalia wakulima kuliko kusikiliza habari za hawa jamaa wanachosha.
 
WAKATI Msajili wa Hazina amebariki posho mpya za safari za ndani kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) kuwa Sh 500,000 kwa siku kuanzia Januari 2, mwaka huu, imebainika kuwa walishaanza kulipana hivyo tangu mwaka 2011.

Hayo yalibainika jana wakati wa Kamati ya Bunge Hesabu za Serikari (PAC), ilipokutana na Menejimenti ya TPA jijini Dar es Salaam.

Kutokana na kamati hiyo kubaini posho hizo, zilianza kutumika hata kabla ya kupitishwa, imeiagiza Menejimenti ya TPA kuhakikisha wafanyakazi wote waliolipwa viwango vipya vya malipo ya safari kabla ya kuruhusiwa na Msajili wa Hazina wanazirejesha.

Agizo hilo la kurejeshwa kwa fedha za posho, limetolewa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, aliyesisitiza kuwa ni makosa kwa taasisi kuanza kutumia viwango vipya vya safari kabla ya kupewa kibali na Msajili wa Hazina.

Aidha, PAC imemuagiza Msajili wa Hazina kuhakikisha anafanya ukaguzi wa haraka kuangalia kama viwango kwa ajili ya safari vikoje na kuweka uwiano wa viwango vya safari kwenye mashirika mengine ya umma.

PAC pia imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu katika matumizi tata ya Sh bilioni 26.

Matumizi hayo ni Sh bilioni 9.6 zilizotumika kwenye mkutano moja wa wafanyakazi, Sh bilioni 6.4 zilizotumika kwa ajili ya matangazo, Sh bilioni 10 zilizotumika kwenye safari na Sh bilioni 43 kwa ajili ya manunuzi ya dharura.

Kwa mujibu wa agizo la PAC, wafanyakazi hao watalazimika kulipa fedha hizo kuanzia mwaka 2011 hadi Januari Mosi, mwaka huu, yaani siku moja kabla Msajili wa Hazina hajatoa kibali kubariki posho mpya Januari 2 mwaka huu.

Menejimenti na Bodi ilipitisha viwango vya safari ambavyo ni Sh 500,000 kwa kada ya juu na Sh 125,000 kwa kada ya chini na ambavyo TPA walianza kuvitumia bila kupewa kibali tangu mwaka 2011 hadi Januari 1 mwaka huu.

Viwango vya awali vilikuwa ni Sh 270,000 kwa ngazi ya juu na Sh 94,000 kwa kada ya chini.

“Ninawaagiza kuhakikisha wale wote walionufaika na viwango vipya vya safari kabla ya vibali kutolewa, kuhakikisha wanarudisha fedha hizo za umma, mtatafuta njia ya kuhakikisha wafanyakazi hao wanarejesha na hata kama ni kukatwa kwenye mishahara,” alisema.

Aidha, Zitto alisema: “ Nifikishieni salamu kwa (Lawrence) Mafuru (Msajili wa Hazina) kuhakikisha mnafanya ukaguzi wa haraka kwenye mashirika mengine kama Ewura, LAPF, NSSF na mengine kuangalia viwango vya safari wanavyolipana na ili kuweka usawa na kwenye mashirika.” Aidha, Menejimenti ya TPA ililiambia Bunge kuwa watahakikisha mamlaka inatumia mfumo wa kisasa katika mahesabu na shughuli nyingine.

“Tulikuwa tunatumia mfumo wa kizamani ambao ulikuwa na matatizo lakini sasa tunataka kununua mfumo mpya wa ERP ambao pia hutumiwa na hata bandari za nchi zingine,” alisema Meneja wa Tehama, Phares Magesa.

Hatua hiyo ya kutaka kufungwa kwa mfumo wa kisasa wa kielektroniki katika hesabu na shughuli za bandari, unatokana na ripoti ya CAG kubainisha kutokuwapo kwa nyaraka zinazothibitisha matumizi kutokana na mahesabu kufanywa kwa mkono.

Katika ripoti hiyo, kwenye fedha zilizotumiwa kwa ajili ya mikutano ya wafanyakazi, zaidi ya Sh bilioni 600 hazina nyaraka ya matumizi yake na kwenye hoja ya matumizi ya matangazo Sh milioni 384 zimekosa nyaraka za matumizi yake.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande alisema uongozi wake umeweza kubadilisha sheria ambazo zilikuwa zikitoa mwanya kwa mkurugenzi kuidhinisha fedha zaidi ya bajeti na kwa kufanya hivyo, wameweza kupunguza matumizi kwa asilimia 30.


CHANZO:
Habari leo

Days are coming soon for you all, with the poor Governance never happened onearth.
 
Hivi zitto Na hao wabunge wanalipwa posho kiasi gani kwa siku,? Majungu chuki na wivu? Hawajatufafanulia hiyo laki tano kina nani wamelipwa Na wana cheo gani na Kwa kazi gAni.,?
 
Wengi mnakomenti kwa jazba Na Ushabiki wa kichama.
 
Hivi zitto Na hao wabunge wanalipwa posho kiasi gani kwa siku,? Majungu chuki na wivu? Hawajatufafanulia hiyo laki tano kina nani wamelipwa Na wana cheo gani na Kwa kazi gAni.,?
Huu ni wizi tu bila kujali cheo.

Kila mtu nchi hii ni mwizi tu.
 
Nchi hii fedha zinaliwa kina kona... Ukijua ukweli utashangazwa na ufisadi kila eneo na watu wanaendelea na maisha kama kawaida.

Vita dhidi ya ufisadi ni vita ngumu, si dhidi ya chama, kabila au watu fulani. Ni mfumo ulioharibika toka juu na watu wanaendesha maisha yao ya pepo ya mabwege, kila uchao. Nani ataiokoa Tanzania ?

Tunamhitaji sana EL. Angekuwepo huu upuuzi ungekoma.
 
Ukiichagua CCM utaibiwa tuu!!,unaambiwa chagua chama na watu wenye sera na maono mbadala wewe hutaki,unakaidi ,unajiona jeuri zaidi na mshabiki wa CCM utaibiwa tuu na mimi nasema mashirika ya umma waibe tu mana watu hawaoni namna nyingine ya kuondoa mfumo huu wa kifisadi.

Unaambiwa CCM ni chama cha majambazi lakini wewe unakataa na unaendelea kuichagua CCM utaibiwa tu hakuna namna nyingine mana wote lazima tukubali kuwa hii nchi ina vyama vingi.Kuchagua chama kingine ni moja ya namna ya kuwajibisha viongozi na mfumo mbovu unaopeana ulaji bila woga wa kupoteza madaraka.
Mwakyembe anapiga kelele kama debe tupu huku akishindwa kufanya ubunifu wa kuwalipa Wafanyakazi wa reli;wakati huohuo wengine wakikiuka utaratibu wa kujiongezea posho na marupurupu.

Hapa nasema waibe tu mana hakuna mmiliki wa hizo hela na muda sio mrefu waziri muusika atasema kuwa pesa walizojilipa hazikua za serikali.Ataungwa mkono na waziri mkuu na mafisadi.

Nasema tena waibe tu mana hata sekta nyingine wanaiba ,panya road nao wanapora mana hamna namna nyingine ya kutajirika kirahisi isipokua kupitia ofisi za umma na pesa za umma zisizo na mmiliki wala msimamizi.


Na mwaka huu tuendelee kuichagua CCM ili tuibiwe zaidi mana hatuna uwezo wa kulinda kura zetu zisiibiwe.
Mana wote lazima tukubaliane kuwa kama hatuwezi kulinda kura zetu tulizopiga wenyewe hatuwezi kamwe kulinda pesa ambazo hata serikali imekuwa ikikana kuwa haizimiliki.

Badala ya kuajiri watumishi waadilifu tunaajiri ndugu na marafiki halafu wanajipangia mishahara mikubwa na wakipewa bado wanaiba na kufoji risiti za matumizi.
Kwa nini mtu asichunguzwe kama zamani.
Mtu ana mwaka mmoja kazini anamiliki mali za thamani ya milioni mia nane na haulizwi kwa nini wengine wasiige na kuwa wezi.
Na mwenye urefu wa kamba ya shoka naye atajiunga na panya road kusaka hizo zilizoibiwa ili naye anunue hata bodaboda.
 
Jamani viwango hivi vimemnufaisha pia waziri wao nina uhakika. Halafu yeye anasema anapiga vita ufisadi. This guy is a publicity seeker otherwise asingekubali kupokea ruzuku ya namna hii.
 
Kwanini serikali isilipe hivyo kwa watumishi wote kama wanaona ndio stahili inayofaa kulingana na hali ya maisha????
 
sioni tatizo, kila mmoja kwa urefu wa kamba yake sasa mana tumechoka
 
Yaani hii serikali ya kikwete hadi ni ya aina Yake utadhani serikali iko sayari tofauti na dunia.naamini juu ya hii dunia hakuna serikali ya kulinganishwa na uozo wa CCM hadi inaitia kinyaa. Kila sehemu ni mabomu ya machozi, one day yes itajulikana watunyonyeni damu yote tu .
 
Back
Top Bottom