Pongezi Wizara ya kilimo

brokenagges

Member
Sep 29, 2022
43
27
Pongezi kwa Serikali ya Samia kwenye Sekta ya Kilimo.

Kupitia serikali hii ya Rais Samia jitihada nyingi sana zinafanyika katika kufanya mapinduzi ya Kilimo nchini ili ile slogan tunayotembea nayo siku nyingi “Kilimo ni uti wa mgongo wa Mtanzania,” iwe na uhalisia.

Wengi tumeliona hili kupitia kwenye Wizara ya Kilimo ya Mh. Bashe, hii wizara kwa sasa hivi tunaweza kuona kwamba imepata waziri anayeitendea haki kwa kuanzisha mashamba darasa sehemu mbalimbali nchini na kutoa ajira kwa vijana wengi kabisa.

Ningeshauri badala ya kuendelea kuanzisha mashamba mapya Wizara ya Kilimo ingefikiri kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani wakaboresha na kuyajengea miundo mbinu mashamba mengi yaliyopo sehemu tofauti tofauti ndani ya nchi na yanayonayomilikiwa na Jeshi la Magereza na hivyo kuyabadilisha ili magereza wafanye Kilimo chenye tija.

Hapa itakuwa watu wengi sana wamepata ajira, ukizingatia kwamba wafungwa wapo magerezani kwa muda na Kuna wakati watamaliza kuzitumiakia adhabu zao na wataongia mtaani kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Wapo wengine wameingia magereza wakiwa hawana ujuzi wowote, lakini wakitoka mule wakiwa na ujuzi pengine wa kilimo ama ufugaji wanaweza kuja kuchangia katika pato la taifa kwa namna nzuri zaidi na ukizingatia kwamba wapo waliofungwa kwa sababu ya makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja vibaka na waporaji na hiyo yote walifanya kwa sababu hawajui ni nini cha kufanya katika kujitafutia na kupata pato halali.

Pia yale mashamba ya magereza yatazalisha kwa tija, maana watafanya kilimo cha kisasa hivyo wanao uwezo hata wa kulisha nchi na ziada ikauzwa nje. Nasema hivyo kwa sababu ardhi ya magereza ni kubwa sana na sidhani kama inatumika inavyostahili.
 
Back
Top Bottom