Pongezi kwako Vincent Nyerere!

Pongezi kwako Vincent Nyerere!

Hongera sana Vicent hii inaonesha kuwa unajua unachokifanya tangu jimboni kwako na huko ulikoitwa na chama chako ukatete haki isipotee endelea kuchapa kazi kijana 2015 ni yako iko wazi utaweka historia ya kurudia jimbo la Musoma mjini.
 
mtoto wa nje wa familia ya mwalimu kama alivyonadi mzee wetu,baba yetu Beny, ameleta balaa kubwa sana Arumeru, navyokuambia hivi sasa kuna kikao cha siri cha wanakamati ya uchaguzi ya CCM wakitafakari nini kilichotokea, wanalaumiana wao kwa wao.
"vita vya panzi furaha kwa kunguru"
 
Vicent Kiboko Nyerere ni jembe na hapa anasubiliwa kwa hamu na wapiga kura wake, mapokezi yake yameshaandaliwa tutawajuza wana JF akishafika Msm.
 
kwa bahati nzuri wakati wa uchaguzi mkuu nilikuwepo mkoa wa mara vicent nyerere mbinu alizotumia kushinda musoma mjini hasa kuzibiti uibwaji wa kura ndizo hizo hizo alizotumia Arumeru sasa kazi wanayo wakibuni mbinu nyingine na M4c wanakuja na brand new ya kuzibiti mpaka kitaeleweka tu
 
Hongera kwa kazi nzuri iliyomuumbua mkapa,sasa watanzania wanajua Mkapa ni m2 wa namna gani
 
Kwa mwenye taarifa naomba anijibu. JE VINCENT NYERERE ANA ACOUNT HUMU JF? Ni vyema nae akijiunga kama wenzie ili tupate kubadilishana maneno/mawazo pale inapobidi.
 
Kwa mwenye taarifa naomba anijibu. JE VINCENT NYERERE ANA ACOUNT HUMU JF? Ni vyema nae akijiunga kama wenzie ili tupate kubadilishana maneno/mawazo pale inapobidi.
tabu ya wanasiasa hawajiungi kazi yao kusoma tu tumwambie Slaa na Mukama na Maalim wawalazmishe wabunge wao kujiunga humu
 
Ndugu zangu wana JF hata mimi naungana na wapenda mabadiliko wote katika nchi yetu kumpongeza kamanda Vicent J. Nyerere kwa kazi nzuri aliyoifanya kama kampeni manager akisaidiana na mwenzake Mch.Natse.Mungu awabariki kwa kazi nzuri.Nimeamini kweli

MLIANZA NA MUNGU NA MMEMALIZA NA MUNGU na nawaombea MUENDELEE NA MUNGU KATIKA KUTIMIZA NA KUTEKELEZA AHADI MLIZOAHIDI KWA WANAARUMERU.MUNGU AWABARIKI SANA
 
Edward Lowasa nae amechangia kuiua CCM at the same time akiisaidia CHADEMA kwa kitendo chake cha kuwahonga wajumbe ili wampitishe Mkwe wake kwenye kura za maoni na akaharibu kabisa pale alipokuja jukwaani kupiga kampeni kwa ajili ya Sioi. Anajua kuwa Watanzania wanajua kuwa yeye ndo aliyeshiriki kuiua CCM kwa ufisadi wake na wenzie, na kitendo cha kwenda kwenye kampeni ni dalili tosha kuwa aliamua kuisaidia M4C bila kujua huku akiiua CCM. Thanx EL. Pia alitoa pesa zilizotumika kununulia shahada za wapiga kura wa Siyoi.
 
tabu ya wanasiasa hawajiungi kazi yao kusoma tu tumwambie Slaa na Mukama na Maalim wawalazmishe wabunge wao kujiunga humu
Nadhani kunahaja sasa ya kuwataka hawa jamaa wajiunge nasi. Nitamtafuta FB na nitamuomba ajitokeze tujumuike kwa pamoja jamvini.
 
mshikaji ni jembe. amewachapa kiboko magamba mpaka wamefurahi wenyewe. Mwenyewe binafsi nimetokea kumpenda toka pale Mzee Ben alipompakazia mbovu kwamba cyo wa familia ya mwalimu na yeye kujitetea na hakukata tamaa. Yah the man is gud.
 
Tunaposhangilia Kazi nzuri iliyofanywa na vijana wenzetu huku Arumeru Mashariki..Tutafakari je Vijana wa Dsm tumejiandaaje kuiondoa Serikali ya CCM madarakani maana Support yetu isiishie kwenye forums na Mablog...
 
Leo nilikutana na mmiliki wa STAR tv na RFA lunch hour pale serena dsm. Tulisalimiana na nikamshukuru kwa radio yake rfa kutupatia updates za matokeo ya uchaguzi arumeru mashariki mpaka saa za usiku wakati tbc fm hata tbc taifa walikuwa hawafanyi hivyo. Pamoja na kwamba alielewa nafurahia ushindi wa cdm alinipa jibu la kiungwana siwezi kumlaumu

Mkuu kwa kuwa inaonekana wewe unakutana nae. mpe salaam zetu za shukrani kwa uzalendo mkubwa anaouonyesha. maana pamoja na uccm wake amebaki fair na mzalendo kwa nchi yake. Tunamshukuru sana kwa kuiweka Tz mbele ya ukada wake. Hivi sasa Star TV ndio TV pekee inayotoa habari pasipo bias ama upendeleo wowote. Na watangazaji wake wote HONGERENI SANA kwa kubaki proffessional katika kazi yenu.
 
Vincent nyerere ni jembe kwani nimeudhuli ktk kampeni nimekubali
 
Back
Top Bottom