Pongezi kwa wabunge na bunge kiujumla

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
1,000
IMG_20200617_000025.jpg

Napenda kuwapongeza wabunge wa jamhuri la muungano wa Tanzania kupitia kambi kuu mbili za bunge, kwa kumaliza muhura wa takribani miaka mitano.
IMG_20200617_000122.jpg

1:Hongera kwa kambi ya Chama tawala Yani wabunge wa CCM kwa kufumbia macho vitendo vya kinyama, uonevu na kikatili walivyokuwa wanafanyiwa watanzania wenzao kwa sababu tu wana mitazamo tu ya kitofauti na wao. Hakuna mbunge wa CCM aliyesimama wazi wazi kwa hata kukemea vitendo hivi au hata kuonyesha hafurahi vitendo hivi. Hatimae bunge la Job Ndugai ni miongoni mwa mabunge nchini yaliopoteza thamani na hazi yake ya bunge.
IMG_20200617_000114.jpg

2: Pili niwapongeze wabunge wa vyama pinzani kwa ushupavu, uvumilivu na kuto kata tamaa haswa kwa yote waliyokuwa wanapitia katika kipindi Cha miaka mitano. Wengine wamelipishwa faini zisizo na mashiko, wengine kuwekwa vifungoni bila sababu ya msingi na wengine kutiwa ulemavu. Wameonyesha ushujaa wa kutosha.
IMG_20200617_000038.jpg

IMG_20200617_000108.jpg

3. Pia niwapongeze wabunge waliohama vyama na kuhamia Chama tawala kwa kisingizio Cha kusema wanaunga mkono juhudi za Mhe. Raisi JPM na Serikali yake ya awamu ya tano. Lakini Ni mpaka uhame Chama ndio useme unaunga mkono juhudi za JPM? Hiki Ni Kipimo Cha Siasa zetu nchini, kumuunga mkono mtu si mpaka uwe Kwenye kundi lake alipo au Chama Cha Siasa alichopo.
IMG_20200617_000102.png

4: Pia nimpongeze Spika Job Ndugai na naibu spika Tulia Auckson kwa kushusha hadhi, thamani na heshima ya bunge, katika miaka mitano hii Kuna muda ilijionyesha wazi kuwa bunge kimekuwa chombo dhaifu na ambacho kinapelekeshwa na matakwa ya kiongozi mkuu wa mhimili Serikali. Pia nampongeza kwa Mhe. Spika kwa maamuzi ya kionevu juu ya baadhi ya wabunge wa vyama pinzani. Pia nampongeza kwa kuonyesha wazi wazi kuwa bunge lake halipo kwa ajili ya watanzania wote nchini Bali lipo kwa maslahi ya Chama tawala.
IMG_20200617_000052.jpg


Ashkumu so matusi.
IMG_20200617_000043.jpg

IMG_20200617_000030.png

Mapambano ya yanaendelea wenye kustahili pongezi tutawapatia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom