Pongezi kwa Serikali namna walivyo pokea msiba na kuongoza heshima na mazishi Elias Kwandikwa

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,160
Ni vema kuwapa heshima viongozi wetu. Jeshi letu limejitoa kwa dhati na Serikali kwa ujumla,Toka hatua za awali Hadi hitimisho Mazishi.

Sina hakika na gharama zilizotumika Ila inaonekana ni kubwa sana. Maeneo mengi kuagwa mwili, idadi ya viongozi walioshiriki ,idadi wanajeshi.

Mazishi ya Kwandikwa ukiacha Dar, msibani pekee wamehudhuria mawaziri karibu wote, makatibu wizara, wajuu mikoa jirani, ....magari ya serikali zaidi ya 300.

Msiba huo huenda!! Sina hakika umerigarimu taifa hospitali ya wilaya moja Fully equiped. Serikali ina viongozi wengi waliopo na wastaafu nashauri pawepo na protocol maalumu heshima na gharama ya namna Serikali inashiriki, wanadamu hakika tunajua tutakufa. Tuondoe double std na gharama zisizo za Lazima.

Makaburi ya familia pia yanaonekana yamefanyiwa ukarabati yana muonekano mpya. Na Hayati Kwandikwa kasitiriwa katika kaburi mfano Amiri Jeshi JPM!

Rejea you tube : Kifo na mazishi Kwandikwa
 
Nchi haijawahi kua sirious; sisi wengine tunakesho kuwatumikia wananchi ila wengine wanavuruga na kufuja tunayoyakeshea tukiyatafuta.
 
Kwani National Leaders Funeral act inasemaje mbona mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyika inaonekana kama ni Fadhira? He deserved to be laid to rest as the authorties did
 
Kwani National Leaders Funeral act inasemaje mbona mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyika inaonekana kama ni Fadhira? He deserved to be laid to rest as the authorties did
National leaders funeral act haiwahusu mawaziri ni kwaajili ya top leaders tu sema serikali yetu ina shida sehemu fulani katika matumizi yake
 
National leaders funeral act haiwahusu mawaziri ni kwaajili ya top leaders tu sema serikali yetu ina shida sehemu fulani katika matumizi yake
Kwamba expenditures at the funeral zinabadilika kutegemea Na influence ya Mtu Na u karibu wa Departed one Na watawala sio?
 
IKwamba expenditures at the funeral zinabadilika kutegemea Na influence ya Mtu Na u karibu wa Departed one Na watawala sio?
Hapohapo na kwanini gharama za mazishi zibebwe na fedha za mlipa Kodi ihali hapohapo tunataka kuboresha hali ya huduma za kijamii. Tanzania viongozi wa kisiasa wanajipendelea Sana wanaojilipa mishahara na posho nzuri.

Wakiugua wanatibiwa na serikali mpaka wakifa wanazikwa na serikali wakati hapohapo bima ya afya kwa wazee wa kitanzania kizungumkuti watakwambia fedha hakuna 🤣🤣
 
Back
Top Bottom