digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,237
- 22,355
Wakuu hamjambo?
Katika pita pita yangu mtandaoni nikawa nimekutana na huu wimbo wa Pascal Cassian, muimbaji wa nyimbo za injili katika video hii inayoenda kwa Jina la "UTAKUFA UNAJIONA". Katika wimbo huu mwinjilisti Casian anasema ukiwa wewe ni binadamu wa maisha ya chini hakika unaweza kufa huku unajiona.
Video hii ilitoka kipindi Pascal amepata ajali hivyo kupelekea kupewa rufaa ya kwenda India ili kutibu kibofu cha mkojo ambacho kilionekana kuwa na shida. Gharama za matibabu ilikuwa ni shilingi Millioni 25, alijaribu kuomba misaada lakini Watanzania wachache walijitokeza kumchangia, mtu muhimu sana katika kunusuru uhai wa Cassian ambaye Mimi ninamuona kama mjumbe wa Mungu Mh. Makonda alijitolea na kumtibu ndugu P.Cassian. Hakika namuombea maisha marefu sana huyu mkuu wa mkoa Mh. P. Makonda, na aendelee kuwa na moyo huo huo, katu asichoke kutenda mema.
Mwisho, katika video hii mwinjilisti Cassian ametuasa kuacha kitumia pesa kubwa kwenye misiba bali pesa hizo zichangwe ili kunusuru uhai wa mgonjwa.
Hongera sana Mh. P. Makonda, Mungu akulinde na mabaya yote yaliyo mbele yako, na pole kwa masahibu yalomkuta bwana Cassian.
Sent using Jamii Forums mobile app

nirudishie chenchi nishuke