Pongezi kwa Mashujaa Wetu Wote. Kazi Inaendelea

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
19,488
Reaction score
26,108
Ningependa kuzungumzia kwa kirefu lengo la kichwa cha mada hii; lakini hiyo siyo dhumuni la haya machache nitakayo yaweka hapa.

Mashujaa, waTanzania wote, hasa vijana mliojitokeza maeneo yote ya nhi yetu kuandamana kupinga uhalifu uliofanyika; na baadhi yenu kupoteza maisha, nawapongeza kwa moyo safi kabisa kwa niaba ya waTanzania wote wapenda haki.

Kazi hii inaendelea, msikate tamaa.

Leo niseme tu kwamba waTanzania tumeipoteza nafasi muhimu kabisa ya kubadilisha hali hii inayo tukabili kwa sababu moja tu; ya kukosa uelewa kwa baadhi ya wengi miongoni mwetu.

Kilichotakiwa kufanyika ni kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano haya ili kazi iwe nyepesi kwa kila mmoja wetu.
Lakini nafasi hiyo tumeipoteza, na sasa italazimu tulipie gharama kubwa sana kwa kupambana na hawa waovu wanaolazimisha kututawala.

WaTanzania, sasa tunao uamzi kati ya mambo mawili:

Mosi, kwa ujumla wetu na umoja kati yetu tuendelee kukataa kwa nguvu zaidi kujisalimisha kwa hawa watu, kwa njia zote hadi wakubali kusalimu amri ili tuwawajibishe kwa maovu yao.

Au, sisi wenyewe kwa kushindwa kupata ushirikiano miongoni mwetu, tujisalimishe kwao, jambo ambalo wao wanalitarajia litokee.
Tukubali kuwa watawaliwa, ambao, watawala watakuwa na uhuru wa kufanya lolote wanalotaka juu yetu.
Wachache miongoni mwetu, kama akina Tundu Lissu; akina John Heche; viongozi mbalimbali wa dini wakionekana kuwa pingamizi, wachukuliwe mmoja mmoja na kutendewa watakavyo watawala ili kutuonyesha mfano wa kutawaliwa.

Hii ndiyo hali halisi tunayo iingia sasa hivi.

Ni juu yetu sasa kulipa gharama kubwa juu ya ujinga wa baadhi yetu ambao hawakuona ulazima wa kutoka ili tuwaondoe madarakani hawa waovu.
Naamini "mjinga" yeyote anao uwezo wa kuuondoa ujinga wake. Ndiyo maana naamini waTanzania wataachana na ujinga huu.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Yes, widespread apathy ni moja ya factor. Factor nyingine nadhani ni umaskini wa Watanzania. Hatuna uwezo wa kuandamana kwa week nzima bila kufanya kazi ya kujipatia pesa ya kuweka kitu mezani. We run out of steam mapema mno!
 
Naona sasa vikundi vya kigaidi vinaenda kutokea kwa mapinduzi
FB_IMG_1761996929927.jpg
 
Factor nyingine nadhani ni umaskini wa Watanzania. Hatuna uwezo wa kuandamana kwa week nzima bila kufanya kazi ya kujipatia pesa ya kuweka kitu mezani. We run out of steam mapema mno!
I respectifully disagree with this notion of poverty being a factor. If anything, that should be the dring force to bring about change!

Inakatisha tamaa sana kwa watu kujitoa mhanga kama walivyo fanya vijana hawa katika hizo siku tatu; halafu wengine wote wawe kama watazamaji tu; tena hata bila kushangilia?
It's so demoralizing!
 
Kalamu, asilimia kubwa ya Watanzania, ni wezi, wavivu, wanafiki, masikini, wajinga, no exposure, wameridhika, na mambo kama hayo,

Sasa ukiwatolea utawala ambao wanafanana nao, watakuona wewe ndio mbaya,

Wataiba wapi tena, wakati tumezoea, atatufanyisha kazi huyu kama punda, wakati nikiuza kagenge kangu kazi imeisha,

Ningeenda mahakamani hata kama nina kosa, nikimpa hakimu rushwa kidogo, kesi imeisha,

Nikikamatwa na traffic nimempa tuhela, ananiachia, wakati Marekani hata kosa la traffic linakupeleka jela,

Ujanja ujanja na utapeli ndio zetu hizo,

Hivi kwa nini unafhani baadhi ya Watanzania walimchukua Magufuli, basi hiyo ndio sababu.

Kwa tabia na slika zetu watanzania, zinashabihiana nao watawala.

Jeshi liliacha nafasi tuchukue nchi tuwakabidhi, tumeshindwa na wenyewe, wametutukana, sasa wafanye nini,

Ila tatizo kubwa zaidi hata hapo vijana walipofikia ni maandamano kutokuwa na kiongozi wa kuelekeza wafanye nini, wameishia kuchoma maboksi ya tume na vituo vya polisi , badala ya kwenda mzizi hasa , ambapo ni tume ya uchaguzi na Ikulu,

Basi tena, tusubilie maumivu
 
Yes, widespread apathy ni moja ya factor. Factor nyingine nadhani ni umaskini wa Watanzania. Hatuna uwezo wa kuandamana kwa week nzima bila kufanya kazi ya kujipatia pesa ya kuweka kitu mezani. We run out of steam mapema mno!
Ukiacha hilo ulilo ongeza, pengine pia bado watu hawajakubaliana juu ya shida na ukubwa wa shida yenyewe, hivyo hawaoni haja ya kujitoa "mhanga". Sina hakika kama litaendana na ujinga alilo weka mwenye uzi. Ila binafsi naliona ktk sura nyingine.

Kifupi nakumbuka siasa za chadema kati ya 2010 na 2015, walifanikiwa kushawishi umma wa Tanzania juu ya mapungufu na maovu ya watawala na kuyaunga makundi mbalimbali ktk kuyakubali hayo. Lakini kwasasa hoja kubwa inayo simama ni haki ya uchaguzi na kuchaguliwa, inayo kwenda sambamba na utekaji/ukamataji wa watu, sioni hoja ya hii ikiwa tunu muafaka ya kuanganisha jamii yote ya watanzania, hasa ukilinganisha na siasa na mafanikio ya 2010-2015. Japo ni kweli huenda jambo hili la uchaguzi/utekaji laweza likasababisha machafuko kama lisipo tazamwa kwa umakini, na kwangu machafuko si lazima yalete mabadiliko. Na kuna watu (external) naona wanatamani sana tupigane
 
Ila tatizo kubwa zaidi hata hapo vijana walipofikia ni maandamano kutokuwa na kiongozi wa kuelekeza wafanye nini, wameishia kuchoma maboksi ya tume na vituo vya polisi , badala ya kwenda mzizi hasa , ambapo ni tume ya uchaguzi na Ikulu
Mkuu 'Nyamaiso", wakati nikisoma bandiko lako na maelezo mengi ya huko juu, nilikuwa na jibu fupi kabisa kwa maoni yako hayo, ambayo kila mara sikubaliani nayo kamwe!

Sasa, nilipofika kwenye hii mistari yako ya mwisho, ndipo nikakutana na jibu, ambalo kumbe unalo tayari.

Katika nchi yoyote ile, iwe ni Marekani au kwingine kokote, huwezi kukuta wananchi wake wengi wakiwa na haya tunayoyategemea waTanzania wote tuwe nayo: haya ya ujasiri wa kukataa kuonewa, kukataa wizi, n.k, n.k..
Marekani hadi wamefikia hapo walipo ni kuwa wamejenga muundo huo kwa miaka na miaka; sisi ndio hivi tunazungushana tu wenyewe kwa wenyewe.

Nisiandike mengi hapa: Jibu langu ni kwamba hata siku moja hutawapata waTanzania wote au hata kwa wingi wao mkubwa kabisa wajitokeza kupigania HAKI. ILA; hao wachache, majasiri, WASIOKATA TAMAA na kuogopa vitisho vya kila namna, ndio watakao likomboa tidfa hili.
WaTanzania hawa tunao wa kutosha kabisa. Ni swala tu la kuunganisha juhudi zao ili ziweze kuzaa matunda.
 
Ningependa kuzungumzia kwa kirefu lengo la kichwa cha mada hii; lakini hiyo siyo dhumuni la haya machache nitakayo yaweka hapa.

Mashujaa, waTanzania wote, hasa vijana mliojitokeza maeneo yote ya nhi yetu kuandamana kupinga uhalifu uliofanyika; na baadhi yenu kupoteza maisha, nawapongeza kwa moyo safi kabisa kwa niaba ya waTanzania wote wapenda haki.

Kazi hii inaendelea, msikate tamaa.

Leo niseme tu kwamba waTanzania tumeipoteza nafasi muhimu kabisa ya kubadilisha hali hii inayo tukabili kwa sababu moja tu; ya kukosa uelewa kwa baadhi ya wengi miongoni mwetu.

Kilichotakiwa kufanyika ni kujitokeza kwa wingi kwenye maandamano haya ili kazi iwe nyepesi kwa kila mmoja wetu.
Lakini nafasi hiyo tumeipoteza, na sasa italazimu tulipie gharama kubwa sana kwa kupambana na hawa waovu wanaolazimisha kututawala.

WaTanzania, sasa tunao uamzi kati ya mambo mawili:

Mosi, kwa ujumla wetu na umoja kati yetu tuendelee kukataa kwa nguvu zaidi kujisalimisha kwa hawa watu, kwa njia zote hadi wakubali kusalimu amri ili tuwawajibishe kwa maovu yao.

Au, sisi wenyewe kwa kushindwa kupata ushirikiano miongoni mwetu, tujisalimishe kwao, jambo ambalo wao wanalitarajia litokee.
Tukubali kuwa watawaliwa, ambao, watawala watakuwa na uhuru wa kufanya lolote wanalotaka juu yetu.
Wachache miongoni mwetu, kama akina Tundu Lissu; akina John Heche; viongozi mbalimbali wa dini wakionekana kuwa pingamizi, wachukuliwe mmoja mmoja na kutendewa watakavyo watawala ili kutuonyesha mfano wa kutawaliwa.

Hii ndiyo hali halisi tunayo iingia sasa hivi.

Ni juu yetu sasa kulipa gharama kubwa juu ya ujinga wa baadhi yetu ambao hawakuona ulazima wa kutoka ili tuwaondoe madarakani hawa waovu.
Naamini "mjinga" yeyote anao uwezo wa kuuondoa ujinga wake. Ndiyo maana naamini waTanzania wataachana na ujinga huu.

Mungu Ibariki Tanzania.

Kusema kweli kuanzia sasa vijana wetu watasakwa sana kupitia kwa mabalozi wa nyumba 10 na watatolewa kafala chini ya Mafwele na Muliro.
 
Ukiacha hilo ulilo ongeza, pengine pia bado watu hawajakubaliana juu ya shida na ukubwa wa shida yenyewe, hivyo hawaoni haja ya kujitoa "mhanga". Sina hakika kama litaendana na ujinga alilo weka mwenye uzi. Ila binafsi naliona ktk sura nyingine.

Kifupi nakumbuka siasa za chadema kati ya 2010 na 2015, walifanikiwa kushawishi umma wa Tanzania juu ya mapungufu na maovu ya watawala na kuyaunga makundi mbalimbali ktk kuyakubali hayo. Lakini kwasasa hoja kubwa inayo simama ni haki ya uchaguzi na kuchaguliwa, inayo kwenda sambamba na utekaji/ukamataji wa watu, sioni hoja ya hii ikiwa tunu muafaka ya kuanganisha jamii yote ya watanzania, hasa ukilinganisha na siasa na mafanikio ya 2010-2015. Japo ni kweli huenda jambo hili la uchaguzi/utekaji laweza likasababisha machafuko kama lisipo tazamwa kwa umakini, na kwangu machafuko si lazima yalete mabadiliko. Na kuna watu (external) naona wanatamani sana tupigane
Natofautiana sana na mawazo yako, lakini nitaendelea kukujibu kwa heshima kama tutaweza kuelewana. Nasema hivi mwanzo kabisa, kwa sababu naona upotoshaji ulio wazi katika hoja zako hapa, na huko kwingine tulipo jibishana hivi karibuni humu humu JF.

Hoja yako ya mwanzo ni kuwa "...watu hawajakubaliana juu ya shida na ukubwa wa shida yenyewe...; mapungufu na maovu ya watawala...."

Na kwa maoni yako, "hoja kubwa inayosimama ni haki ya uchaguzi na kuchaguliwa..." "utekaji/ukamataji wa watu..."
Kwa upande wako huoni haya yote yanayofanywa na watawala kuwa ni ya msingi kwenye jamii kuwaunganisha na kuyakataa!

Katika yote hayo uliyoandika hapa sikubaliani nayo yote.

Hawa waTanzania mlio nao vichwani mwenu ni waTanzania wa wapi hawa, wasiopenda HAKI ya kuwa na UHURU wa kuchagua viongozi wanaowataka wao? Hii dhana inatoka wapi, kama siyo dharau inayotokana na tamaduni za kigeni?
Hawa "watawala" wanaokubaliwa na waTanzania ili wawanyime haki hiyo ya msingi kabisa katika maisha ya binaadam yeyote; wao wameletwa hapa na Mungu kuja kuwatawala waTanzania? Kwa nini muwanyime waTanzania haki hii?
Halafu mtu unajitokeza na uso usio na soni kabisa, kwamba "waTanzania hawajaona shida"?

Kama kunyimwa HAKI na UHURU wa kuwachagua viongozi wetu sisi wenyewe haiwezi kuwa agenda ya kutuunganisha sote, unataka tuunganishwe na jambo gani?

Unataka "ukubwa wa shida" ya UTEKAJI/UKAMATAJI iwe kubwa kiasi gani ndipo iweze kuwastua waTanzania na kuwaunganisha ili waikatae? Kuna kipimo maalum ambacho unacho wewe juu ya shida hiyo; kwamba itakapofikia lengo fulani waTanzania wataungana kuikataa?

Halafu, katika kuhalaisha hoja zako mbovu unageukia kwenye upotoshaji ulio wazi kwa kutumia mfano wa chama CHADEMA kutaka kuonyesha kuwa waliungwa mkono na waTanzania wakati huo kwa siasa walizo zisimamia; wakati huo huo wala hutoi mfano halisi wa siasa hizo.

Unachojifanya kusahau hapa ni kwamba wakati huo kulikuwepo na nafasi nzuri, huru ya kufanya siasa, bila misukosuko. CHADEMA waliweza kuwafikia wananchi na kueleza mapungufu yaliyokuwepo katika utawala wa CCM; na wananchi wakawaelewa na kukubali.

Leo hii hata hudiriki kueleza CHADEMA wamefanywa nini, na viongozi wao wapo wapi

Ili nisichukue nafasi kubwa ya kuyaeleza yote haya, naomba tu utusaidie wewe kutueleza kwa nini Samia na Genge lake aliona ni muhimu sana atumie ulaghai na uongo wa kila aina katika ngazi zote za kufikia hapa tulipofikia kwenye uchaguzi wa kipuuzi huu
 
Kusema kweli kuanzia sasa vijana wetu watasakwa sana kupitia kwa mabalozi wa nyumba 10 na watatolewa kafala chini ya Mafwele na Muliro.
Nalihofia sana hili; lakini hapo hapo kunaweza kuwepo na anguko lao kupitia kwenye njia hiyo hiyo.

Hawa mabalozi watakuja kuwa kiungo hatarishi sana; lakini na wao watambue kuwa wanaishi kwenye jamii hii hii, na hawalindwi na polisi masaa 24!
 
Natofautiana sana na mawazo yako, lakini nitaendelea kukujibu kwa heshima kama tutaweza kuelewana. Nasema hivi mwanzo kabisa, kwa sababu naona upotoshaji ulio wazi katika hoja zako hapa, na huko kwingine tulipo jibishana hivi karibuni humu humu JF.

Hoja yako ya mwanzo ni kuwa "...watu hawajakubaliana juu ya shida na ukubwa wa shida yenyewe...; mapungufu na maovu ya watawala...."

Na kwa maoni yako, "hoja kubwa inayosimama ni haki ya uchaguzi na kuchaguliwa..." "utekaji/ukamataji wa watu..."
Kwa upande wako huoni haya yote yanayofanywa na watawala kuwa ni ya msingi kwenye jamii kuwaunganisha na kuyakataa!

Katika yote hayo uliyoandika hapa sikubaliani nayo yote.

Hawa waTanzania mlio nao vichwani mwenu ni waTanzania wa wapi hawa, wasiopenda HAKI ya kuwa na UHURU wa kuchagua viongozi wanaowataka wao? Hii dhana inatoka wapi, kama siyo dharau inayotokana na tamaduni za kigeni?
Hawa "watawala" wanaokubaliwa na waTanzania ili wawanyime haki hiyo ya msingi kabisa katika maisha ya binaadam yeyote; wao wameletwa hapa na Mungu kuja kuwatawala waTanzania? Kwa nini muwanyime waTanzania haki hii?
Halafu mtu unajitokeza na uso usio na soni kabisa, kwamba "waTanzania hawajaona shida"?

Kama kunyimwa HAKI na UHURU wa kuwachagua viongozi wetu sisi wenyewe haiwezi kuwa agenda ya kutuunganisha sote, unataka tuunganishwe na jambo gani?

Unataka "ukubwa wa shida" ya UTEKAJI/UKAMATAJI iwe kubwa kiasi gani ndipo iweze kuwastua waTanzania na kuwaunganisha ili waikatae? Kuna kipimo maalum ambacho unacho wewe juu ya shida hiyo; kwamba itakapofikia lengo fulani waTanzania wataungana kuikataa?

Halafu, katika kuhalaisha hoja zako mbovu unageukia kwenye upotoshaji ulio wazi kwa kutumia mfano wa chama CHADEMA kutaka kuonyesha kuwa waliungwa mkono na waTanzania wakati huo kwa siasa walizo zisimamia; wakati huo huo wala hutoi mfano halisi wa siasa hizo.

Unachojifanya kusahau hapa ni kwamba wakati huo kulikuwepo na nafasi nzuri, huru ya kufanya siasa, bila misukosuko. CHADEMA waliweza kuwafikia wananchi na kueleza mapungufu yaliyokuwepo katika utawala wa CCM; na wananchi wakawaelewa na kukubali.

Leo hii hata hudiriki kueleza CHADEMA wamefanywa nini, na viongozi wao wapo wapi

Ili nisichukue nafasi kubwa ya kuyaeleza yote haya, naomba tu utusaidie wewe kutueleza kwa nini Samia na Genge lake aliona ni muhimu sana atumie ulaghai na uongo wa kila aina katika ngazi zote za kufikia hapa tulipofikia kwenye uchaguzi wa kipuuzi huu
Ni muhimu kuendelea kuweka hoja kwa ustarabu, hivyo shukran kwa kuishi hilo, tuendelee kujadili hoja.

Kuhusu uchaguzi kuwa kipuuzi, sina hakika unatumia vigezo gani kuja na hitimisho hilo? Kwangu chaguzi zote zilizo chini ya ibara hizi za kuwa alie tangazwa hapingwi (mfumo tulio nao sasa) hazina tofauti yoyote ya kimsingi. Zinaweza kuwa amplified kwasababu fulanifulani tu.

Kuhusu hoja ya kuunganisha watu, ukiniuliza mimi kilicho kera watu zaidi ni huu mtindo mpya wa kukwapua kila kitu ulio asisiwa 2019 na kuendelea, hili linagusa sana watu wengi lakini naami si hoja unayo pigania wewe! kwa maana ikatokea vyama wanapewa nafasi fulani za na haki fulani ktk chaguzi kama ilivyo kuwa kabla ya 2019 bado haitakuwa suluhu ya tatizo, hivyo kwangu naona hoja hii inaweza fifishwa muda wowote kulingana na CCM imemuweka mgombea gani au ina Rais gani ktk wakati husika.

Kuhusu chadema ya wakati huo, kulikuwa clear alternative sera za chama dhidi ya CCM, walikuwa na agenda mama ya ufisadi/ubadhirifu wa mali za umma, katiba mpya, na waliweza vutia makundi ya watu kwa hoja mbalimbali na uimara wa safu za uongozi. Lakini kwasasa ukiniuliza mimi naona wanapata support kubwa (sina maana hawana wafuasi) kwasababu ya huruma ya yale yanayo wakuta, kwa maana nyingine baadhi ya mambo CCM/dola wanayo wafanyia yanawaongezea kukubalika/mvuto mbele ya jamii.

Kuhusu chadema na viongozi wake, kwa sehemu fulani nimegusia hapo juu, lakini mengine ni ukweli ni huwezi kwepa taswira ya kuwa ni mgongano wa ndani kati yao wenyewe. Hili la TAL/Heche/CHADEMA na no reform no election, mimi huwa najiuliza swali binafsi labda ni kuachie na wewe swali hilo, Hivi ingelikuwa ni wewe ndio rais wa nchi kisha wakapatikana watu wenye lengo la kuzuia uchaguzi wa nchi ungefanya nini? Kosa kubwa hapa naliona ni kukosa masikilizano toka pande zote, na kila mtu akaamua kusimamisha misuli dhidi ya mwingine.
 
Kuhusu uchaguzi kuwa kipuuzi, sina hakika unatumia vigezo gani kuja na hitimisho hilo? Kwangu chaguzi zote zilizo chini ya ibara hizi za kuwa alie tangazwa hapingwi (mfumo tulio nao sasa) hazina tofauti yoyote ya kimsingi. Zinaweza kuwa amplified kwasababu fulanifulani t
Nionyeshe katika andiko langu nilipo rejea hizo chaguzi unazozizungumzia wewe. Sasa unataka mawazo yako ndiyo yawe yangu?
Inabidi nirudi hapo juu ulipo anzia kwa kutaka mjadala wa kistaarabu. Wewe siyo mtu wa kwanza katika kuhimiza hilo; nimejadiliani miaka chungunnzima na watu wa aina yako, na wote wakiwa na mbinu hiyo hiyo ya mijadala ya kistaarabu; kama anavyodai Samia Suluhu Hassan siku zote, na alipoona watu wanajuwa mbinu za kupoteza muda kwake na mizungko mingi, kazamia moja kwa moja katika kutafuta njia za kuwanyamazisha.

Kwa hiyo hiyo mbinu ninaifahamu sana; na nikueleze wazi, huwa sina subira kabisa na kuzungushana kusikokuwa na maana yoyote kama unavyotaka sasa kuniingiza. Muda huo sina.
Kuhusu hoja ya kuunganisha watu, ukiniuliza mimi kilicho kera watu zaidi ni huu mtindo mpya wa kukwapua kila kitu ulio asisiwa 2019 na kuendelea, hili linagusa sana watu wengi lakini naami si hoja unayo pigania wewe! kwa maana ikatokea vyama wanapewa nafasi fulani za na haki fulani ktk chaguzi kama ilivyo kuwa kabla ya 2019 bado haitakuwa suluhu ya tatizo, hivyo kwangu naona hoja hii inaweza fifishwa muda wowote kulingana na CCM imemuweka mgombea gani au ina Rais gani ktk wakati husika.
Huu hapa ni mfano halisi kabisa wa kupotezeana muda tu, kujadiliana jambo ambalo ni fikra zisizokuwa na uhalisia wowote.
Nani kakueleza waTanzania hawajali kukwapuliwa kwa mali zao, na kwa sasa Samia kaweka rekodi mpya kabisa. Si ukwapuzi wa mali tu, lakini yeye anatupeleka mbali zaidi katika hatua ya waTanzania kugeuzwa kuwa watwana ndani ya nchi yao!
Hivyo vyama unavyo vizungumzia wewe kupewa(?) nafasi, na hapakuwa na suluhu? Hata sielewi unalenga kitu gani hapa?

Kiufupi, mkuu 'Ajuae' hadi jana au juzi nilikuwa sijawahi kukusoma popote humu jukwaani; lakini kutokana na haya machache tuliyo badilishana hapa, ni wazi kabisa kwangu kuwa wewe ni mtu wa mlengo gani; na ni mlengo wa kupoteza muda tu; kwa sababu sioni lolote jipya na la maana zaidi kujadili kutoka kwako mbali ya kupigania tu maslahi yanayotokana na utawala dhalimu kabisa tuliowahi kuushuhudia katika taifa hili.

Mungu aepushe, lakini kama mwendo utakuwa ni hivi hivi, taifa letu litatumbukia katka matatizo makubwa.

Huko chini ya andiko lako sina nia ya kuendelea nako.
 
Nionyeshe katika andiko langu nilipo rejea hizo chaguzi unazozizungumzia wewe. Sasa unataka mawazo yako ndiyo yawe yangu?
Inabidi nirudi hapo juu ulipo anzia kwa kutaka mjadala wa kistaarabu. Wewe siyo mtu wa kwanza katika kuhimiza hilo; nimejadiliani miaka chungunnzima na watu wa aina yako, na wote wakiwa na mbinu hiyo hiyo ya mijadala ya kistaarabu; kama anavyodai Samia Suluhu Hassan siku zote, na alipoona watu wanajuwa mbinu za kupoteza muda kwake na mizungko mingi, kazamia moja kwa moja katika kutafuta njia za kuwanyamazisha.

Kwa hiyo hiyo mbinu ninaifahamu sana; na nikueleze wazi, huwa sina subira kabisa na kuzungushana kusikokuwa na maana yoyote kama unavyotaka sasa kuniingiza. Muda huo sina.

Huu hapa ni mfano halisi kabisa wa kupotezeana muda tu, kujadiliana jambo ambalo ni fikra zisizokuwa na uhalisia wowote.
Nani kakueleza waTanzania hawajali kukwapuliwa kwa mali zao, na kwa sasa Samia kaweka rekodi mpya kabisa. Si ukwapuzi wa mali tu, lakini yeye anatupeleka mbali zaidi katika hatua ya waTanzania kugeuzwa kuwa watwana ndani ya nchi yao!
Hivyo vyama unavyo vizungumzia wewe kupewa(?) nafasi, na hapakuwa na suluhu? Hata sielewi unalenga kitu gani hapa?

Kiufupi, mkuu 'Ajuae' hadi jana au juzi nilikuwa sijawahi kukusoma popote humu jukwaani; lakini kutokana na haya machache tuliyo badilishana hapa, ni wazi kabisa kwangu kuwa wewe ni mtu wa mlengo gani; na ni mlengo wa kupoteza muda tu; kwa sababu sioni lolote jipya na la maana zaidi kujadili kutoka kwako mbali ya kupigania tu maslahi yanayotokana na utawala dhalimu kabisa tuliowahi kuushuhudia katika taifa hili.

Mungu aepushe, lakini kama mwendo utakuwa ni hivi hivi, taifa letu litatumbukia katka matatizo makubwa.

Huko chini ya andiko lako sina nia ya kuendelea nako.
Naona mkanganyiko wa mambo hapa Kalamu,
Ila nitaheshimu rai yako, sitakupotezea muda zaidi hasa ktk uzi huu.

Ila kwakuwa lengo langu ni kushiriki mijadala hii kwa maslah ya taifa (tofauti na ulivyo weka wewe) siku nikiona una hoja nyingine nitashiriki tena.
 
Sina tatizo na kushiriki kwako; tatizo ni lengo la kupotezeana muda kwa mtindo wa kuzungushana kwenye mjadala.
Hii ni mbinu ambayo nadhani huwa mnafundishwa mahali fulani. Ni mbinu mbovu sana.
 
Halafu sijui hata kama natumia mbinu yoyote, nilikuwa nafanya tu mjadala kwa kujibu au kuweka hoja.
 
Unajuwa, hata Samia Suluhu Hassan na wenzake wote watakueleza kuwa kila kilicho fanyika hadi wakati huu ni njia iliyo nyooka kabisa, ambayo imehitimishwa kwa kumpa ushindi mkubwa yeye.
Sasa ukitaka nikapoteze muda wa kuzungushana na hoja za namna hiyo humu JF, si itakuwa ni kupoteza muda tu?
 
he he , ndio maana baadhi ya watu wanaona ni bora uchaguzi wa urais uwe unaishia ktk halmashauri kuu yao kule! Tuokoe hizo pesa za kampeni na uchaguzi. Maana ni kama huwa wanakuja kutuambia huyu ndio rais wenu ajae baada ya tume kumtangaza huko mbeleni
 
Hata hilo halitakuwa suluhisho; maana matokeo ni yaleyale. Kwa nini mtu huyo anayeitaka sana hiyo nafasi asijitangaze tu yeye mwenyewe na iishie hapo!

Sasa waTanzania wanauliwa tu hivi, kwa sababu ya yeye kutaka kuwa mtawala wa nchi, ya nini kuwa na usumbufu wote huo!
 
Back
Top Bottom