Centrehalf
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 509
- 145
Wana Jf nimefurahishwa sana na tabia ya dr kitila mkumbo,nimemfuatilia sana tangu zilipoibuliwa tuhuma dhidi yake pamoja na zitto na samson mwigamba.dr amekuwa katika hali ya utulivu mkubwa kuliko watuhumiwa wenzie.maana baada ya kamati kuu kuwavua nyadhifa zao na kuwapa siku 14 dr amejitokeza mara mbili tu kwenye media kuzungumzia suala hilo.kutokana na sababu hiyo nimeanza kuamini kwamba maneno aliyosema kwenye kamati kuu kwamba aliingizwa tu kwenye mkenge na zitto pamoja na mwigamba ni ya kweli.nasema hivyo kwa sababu ukiangalia baada ya wote wa 3 kurudisha fomu zilizokuwa na mashtaka 11 dr mkumbo amekuwa kmya akisubiri hatma yake,tofauti na wenzie ambao wameendelea kuhangaika kwa kisngizio cha kupigania haki yao ndani ya chama hata kabla ya chama kutoa hitimisho.zitto kabwe ndio huyo yuko kigoma akiomba huruma ya wananchi,mwigamba ndio huyo katia timu kwa msajili wa vyama.swali linakuja ni kwanini hawa wawili wanatafuta utetezi nje ya chamachao mapema?na kwa nini yy dr mkumbo katulia akisubira maamuzi ya vikao vya chama? je ni kutofautiana kwa viwango vyao vya elimu ndio kulikowatfautisha? hakika dr mkumbo umenikosha sana na ukimya wako hivyo kuthibitisha kwamba hakika ww ni msomi uliye elimika.GUILTY ARE ALWAYS AFRAID.hongera sana dr mkumbo.nawasilisha.
Naunga mkono hoja ya ukimya wa Dr. Kitilla ila pia
Kuna ukimya wa aina mbili, ule ukimya wa mtu hana la kusema na ule ukimya wa kuamua tuu kutosema!.
Kuna ukimya wa kusubiria hatima, ila ila kama tayari umeishaijua hatima, huna haja ya kuisubiria kimya!.
Dr. Kitilla anaisubiria hatima!, Zitto anaijua tayari!, wala hausubirii!.
Ila pia kuna kimya kingi chenye mshindo mkuu!.
Pia shishangai kama walivyo kuku, kuna kuku akishikwa kuchinjwa, anatulia tuu anachinjwa kama afanyavyo kondoo!, na kuna kuku akishikwa kuchinjwa, lazima akukuruke!.
Kwenye tuhuma zozote, ukimya ni admission of guilt, Dr. Kitilla alikubali tangu day one, kuwa yeye ndie initiator wa ule waraka na kumshirikisha Mngamba!, hivyo kunyamaza na kusubiria ni halali yake!.
Zitto anasingiziwa!, hatma yake iliishaamuliwa siku nyingi!, alikuwa anatafutiwa sababu tuu!, kwa nini anyamaze?!. Atulie tuu achinjwe kama yule kuku kondoo?!.
Pasco.