Pongezi 12 kwa Rais Samia

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - KAZI IENDELEE

Ni ukweli usiopingika kuwa Salamu hii imebeba maana na uhalisia wa kazi Iendelee kutokana na mambo mazuri yanayofanywa na Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa uchache hizi ni pongezi kwa mambo machache kati ya mengi yaliyofanywa katika kipindi kifupi cha uongozi wake .

Pongezi ya 1
Pongezi kwa Mhe.Rais Samia kwa kufungua fursa za ajira kwa Watanzania.
(a)Kutoa vibali vya ajira katika utumishi wa umma kwa kipindi kifupi na miongoni mwa vibali hivyo ni ajira 44000 alizozitoa hivi karibuni na ajira zinazotolewa kupitia taasisi na mashiriki ya Umma.

(b). Ajira kupitia sekta binafsi na uwekezaji ambapo kutokana na sera yake ya kuvutia na kuiwezesha sekta binafsi kuwekeza kumetengeneza ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa Watanzania.

(c) Ajira kupitia miradi mikubwa inayozinduliwa na kutekelezwa ambayo imetoa fursa za ajira kwa Watanzania wengi. Miongoni mwa miradi hiyo ni SGR, STIGLERS ,Bomba la Mafuta,Miundombinu ya Barabara ,Afya na Elimu .

Pongezi ya 2
Pongezi kwa Rais Mhe.Samia kwa kujali na kuboresha Maslahi ya Wafanyakazi. Katika kipindi kifupi cha Uongozi wake amefanya makubwa yanayohitaji pongezi - kupandisha Madaraja watumishi 190,562 ,kulipa madeni/malimbikizo ya watumishi 65,391 ambapo zaidi ya Tsh.Bilion 90 zimetumika , kupandisha mishahara kwa 23% kwa Mishahara ya kima cha chini ,kupunguza kodi ya mshahara (PAYE) kutoka 9%-8% na mengine mengi.Hongera sana .

Pongezi ya 3
Pongezi kwa Mhe.Rais Samia kwa kuendeleza kwa Kasi Miradi ya Kimkakati yenye maslahi kwa Taifa. Ikumbukwe katika kipindi cha Mwaka mmoja na nusu amezindua vipande vitatu vya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ambavyo ni kipande cha Makutupora-Tabora ,Tabora- Isaka na kipande ya Isaka- Mwanza na vyote shughuli za Ujenzi zimeanza, Ujenzi wa Meli kubwa MV Mwanza wafikia 71% ,Daraja la Kigongo Busisi (51%), STIGLERS mpaka mwezi Agosti 2022 ilikuwa 67% kazi inaendelea.

Pongezi ya 4
Pongezi kwa Mhe.Rais Samia kwa uboreshaji wa Miundombinu na Huduma za Afya nchini. Ndani ya mwaka mmoja na nusu wa Uongozi wake tumeshuhudia ujenzi na ukamilishaji wa Hospitali za Kanda,Rufaa Mikoa, Wilaya ,Vituo vya afya na Zahanati.

Haikuishia hapo tumeona uendelezaji wa Teknolojia ya afya kwa kuleta mitambo ya kisasa ya Afya ikiwemo Uzinduzi wa Mitambo ya CATHLAB katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ,mitambo ya kuzalisha Oksjeni n.k, upatikanaji wa madawa na chanjo kwa makundi mbalimbali ikiwemo Watoto.Mhe Rais ameendelea kuajiri na kuendeleza Wataalamu wa Afya katika taasisi za elimu za ndani na nje ya Nchi .Hongera sana Mhe.Rais Samia .

Pongezi ya 5
Pongezi Mhe.Rais Samia kwa kustawisha Jamii kwa kuyapa Kipaumbele Makundi Maalum. Mhe.Rais pamoja na jitihada zake za kuleta maendeleo kwa wote pia ametilia mkazo makundi maalum ikiwemo Wanawake ,vijana ,wazee na wenye ulemavu na kwa kutambua umuhimu wake ameunda wizara kamili inayoshughulika na Maendeleo ya Jamii na ni ukweli usiopingika kuwa makundi haya yametiliwa mkazo ,Elimu na kampeni za kupinga ukatili zimeendelea kuwezeshwa ili kutoa elimu kwa jamii ,uwezeshaji wa makundi haya kiuchumi pia imekuwa kipaumbele cha Mhe.

Rais Samia katika adhma yake ya kuhakikisha habaki mtu nyuma katika Maendeleo .Hongera sana .

Pongezi ya 6
Hongera Mhe.Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za Kisheria na Haki katika Taifa letu. Ndani ya kipindi cha uongozi wake tumeshuhudia Ujenzi wa Mahakama Kuu katika Mikoa mbalimbali pamoja na Mahakama katika ngazi za Msingi ,Ujenzi na uzinduzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki katika Mikoa mbalimbali, uwezeshaji wa kibajeti katika Mhimili wa Mahakama pamoja na ajira kwa Watumishi wa Mahakama ikijumuisha Majaji wa Mahakama kuu na Mahakama ya Rufaa adhma yake na Serikali yake ni kuhakikisha huduma za Kisheria na upatikanaji wa haki zinafika karibu na Mwananchi na kwa wakati. Hongera sana Mhe.Rais.

Pongezi ya 7
Pongezi kwa Mhe.Rais Samia kwa kuendeleza na kuboresha Mahusiano ya Kidiplomasia. Ni ukweli usiopingika kuwa mahusiano mazuri baina ya mataifa ni chachu ya Maendeleo na katika kipindi kifupi tumeshuhudia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na mahusiano mazuri kati yetu na wenzetu ,kwa sasa bidhaa na mazao yanayozalishwa Tanzania yanauzwa katika Mataifa mbalimbali na hivyo kuongeza tija kwa wakulima na kuliingizia taifa fedha za kigeni ,kupitia mahusiano mazuri tumeendelea kutangaza utamaduni na utalii wetu ,tumepata fursa kwa Watanzania hususani wataalamu wa lugha ya kiswahili kwenda kufundisha kiswahili katika mataifa mengine ikiwemo Afrika Kusini na mwisho lakini sio kwa umuhimu Watanzania kushiriki katika fursa za Elimu na Ajira za kikanda na Kimataifa.

Pongezi ya 8
Pongezi kwa Mhe.Rais Samia kwa uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Kilimo. Kilimo ni sekta muhimu na ya kimkakati iliyoajiri na yenye uwezo wa kuajiri watu wengi zaidi.Kwa muktadha huo Mhe.Rais ameongeza Bajeti ya Kilimo kutoka Bilioni 294.16 hadi Bilioni 751 kwa mwaka 2022/23 ikiwa ni ongezeko la Bajeti la zaidi ya 150% ,utofauti huu wa kibajeti ikilinganishwa na mwaka uliopita ni dhahiri kuwa Rais amedhamiria kutuvusha ,ni wajibu wa Viongozi waliopewa dhamana kufikia na kuvuka matarajia ya Mhe.Rais kwa kuhakikisha kuwa Watanzania wanaona matunda ya uwekezaji huu.

Muhimu zaidi katika Sekta ya Kilimo kunao mradi maalum BUILDING BETTER TOMMORROW unaolenga kuwawezesha Vijana kuwekeza katika Kilimo .Hili ni jambo jema na linahitaji pongezi.

Pongezi ya 9
Pongezi kwa Mhe.Rais Samia kwa kuboresha huduma za Elimu Nchini. Katika kipindi kifupi tumeshuhudia ujenzi wa Madarasa 15,000 kwa shule za msingi na Sekondari ,ununuzi wa vifaa saidizi kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum ,Uongezwaji wa Bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Ujenzi wa Vyuo vya VETA na sasa ni kwa wilaya zote ambazo hazina Vyuo vya VETA ,ujenzi na uboreshaji wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu ,Mpango wa Ujenzi wa Chuo Kikuu cha TEHAMA Dodoma, Kidato Tano na Sita Elimu kuwa bila malipo pamoja na ajira lukuki katika kada ya Elimu.

Haya ni mafanikio makubwa na ni kazi nzuri imefanyika chini ya Uongozi wa Mhe.Rais Samia ,hongera sana.

Pongezi ya 10
Pongezi kwa kuendeleza na kuboresha Shirika la Ndege(ATCL) pamoja na Usafiri wa Anga Nchini. Serikali chini ya Mhe.Rais Samia katika mwaka wa fedha 2022/23 ina mpango wa kununua ndege mpya tano ikiwemo ndege moja aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili aina ya Boeing 737-9, ndege moja ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F na ndege moja ya Dash-8 Q400 ununuzi wa ndege hizi Tano kutaongeza idadi ya ndege zinazoendeshwa na ATCL kifikia 16 .

Sanjari na ununuzi wa Ndege hizi Serikali inaendelea na Ujenzi ,Ukarabati na upanuzi wa Viwanja vya ndege katika Mikoa mbalimbali nchini lengo ni kuhakikisha Watanzania wa Mikoa yote wanapata huduma ya usafiri wa Anga. Kazi nzuri hongera sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Pongezi ya 11
Pongezi kwa kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Taifa letu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kipindi kifupi akiwa Mkuu wetu wa Nchi ,tumeshuhudia Ulinzi na Usalama wa Mipaka ya Nchi yetu pamoja na usalama wa Raia na Mali zao.

Lakini pia pongezi kwa namna ambavyo ameendelea kuyawezesha Majeshi yetu kwa Kuajiri watumishi wapya ,Mafunzo na uwezeshaji wa Kibajeti na hivyo kuwaondolea changamoto katika majukumu yao na hivyo kufanya kazi kwa weledi .

Pongezi ya 12
Pongezi ya jumla. Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa mambo yote mazuri aliyoyafanya ikiwemo machache yaliyoanishwa katika andiko hili na mengine mengi ambayo hayapo kwenye andiko hili fupi, Kazi nzuri inafanyika ya kuwaletea maendeleo Watanzania kwa hakika anaiishi ahadi yake ya kuendeleza Mema yote yaliyoanzishwa na watangulizi wake na kuanzisha Mema mapya.

HONGERA SANA
MHE.SAMIA SULUHU HASSAN
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.🇹🇿

KAZI IENDELEE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom