Pombe inaharibu maisha yangu nisaidieni

Pombe inaharibu maisha yangu nisaidieni

Nikuulize

Unakunywa hizo spirits zikiwa kavu au una pata kama cocktail?

Unakunywa kiasi gani kwa ule mzinga wa konyagi au kvnt ?

Una kichwa au nguvu ya mwili inastahamili unachokunywa ??

Vipi ulaji wako upoje ?

Maake spirits ilivyo Kali Inahitaji formula kidg tuu utulie,

Jee upo tyr kuacha pombe sii kwa kushurutishwa na mtu ?

Jitahidi kila kitu kiwe na kiasi
 
Mnywaj mwenzangu.
Kwanza pole na maswahiba
Pili, hongera kwa kuwa unajitambua

Tatu, its NOT too late.
ulivyopoteza (fedha na kutofanya mambo ya Msing ) yasikufanye uone ndio umefeli.

Ushaur wa Eli Cohen na @DK HAYA LAND ufanyie kazi.

mm Naongezea.
Kama hauna familia bas tafuta mwanamke usogeze muish kama Familia.
Ww Uko mbali na Familia yako haion maswaiba unayopitia. ila hakuna kitu kinauma kama kuona unaaibisha familia na wao wanaona.

Ukikaa bachelor na unakunywa Konyag hizo lazima zishuke chini. utasikia manyege kila mara.
Utatembea na barmaid had upate Ukimwi.

So far pamoja na ushaur wa hao wadau wawili . tafuta mweza pia wa kucontrol na kukupa majukumu na purpose nyingine ya kuishi.

Pia usiache pombe 😂😂😂😂😂😂
Ila achana na mapombe makali.
Kunywa zako bia .
 
Nje ya mada kidogo ivi inakuaje mtu mzima na akili zake timamu anashawishiwa kufanya jambo na mtu mwengine?
huwa inakuwa kuwaje yaaani?

Mbona me nimecheza sana na wavuta bangi na walevi ila ktk maisha yangu sjawahi ata kuweka kipande cha sigara mdomon mwangu achilia kunywa pombe ?

Na ktk familia yetu kaka zangu 3 wote ndo starehe zao pendwa ulevi, mirungu na ndaga
ila kwa sas ngada hawavuti wamebakia apo kwenye mirungi na ulevi tu.
 
po
Hayo maisha unayoishi tunafanana Kwa kila kitu
le
Nikuulize

Unakunywa hizo spirits zikiwa kavu au una pata kama cocktail?

Unakunywa kiasi gani kwa ule mzinga wa konyagi au kvnt ?

Una kichwa au nguvu ya mwili inastahamili unachokunywa ??

Vipi ulaji wako upoje ?

Maake spirits ilivyo Kali Inahitaji formula kidg tuu utulie,

Jee upo tyr kuacha pombe sii kwa kushurutishwa na mtu ?

Jitahidi kila kitu kiwe na kiasi
Asante kwa ushauri,kula uwa nakula mkuu tena ata nusu ya nyama ila nina ulevi uliopindukia yaani nimeshakuwa addicted kwa usiku mmoja naweza maliza ata 2 kvant ndogo ila nashindwa jizuia nikiongeza tu ni shida
 
Pole sana ungekua hujaamua kuacha ningekushauri usiache maana mkiacha pombe tutakosa watu wa kuwadharau mtaani.
 
po

le

Asante kwa ushauri,kula uwa nakula mkuu tena ata nusu ya nyama ila nina ulevi uliopindukia yaani nimeshakuwa addicted kwa usiku mmoja naweza maliza ata 2 kvant ndogo ila nashindwa jizuia nikiongeza tu ni shida
Infact una kiwango kinachovuka kiasi,,, jitahidi kama moja una uwezo wa kuimaliza na hupati shida komea hapo hapo!!

Usilazimishe kitu kama tyr umetosheka,

Jitahidi upate kiasi mkuu
 
Mambo vipi ndugu zangu?

Leo nimekuja kwenu nipate ushauri maana napitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu kutokana na ulevi wa kupindukia, labda nianze tu kwa kuwapa historia fupi tu ya maisha yangu nilivyoanza kunywa pombe

Kunywa pombe nilianza 2016 nikiwa chuo kikuu na nilianza tu kwa ushawishi wa makundi mabaya na nilianza na pombe kali kwa iyo ilipelekea kuwa nakunywa pombe kali tu na nilikuwa naimudu fresh japo kuzingua ilikuwa mara moja na nimeendelea na pombe hadi leo hii na imeniletea shida nyingi kiuchumi na kiafya tangu kipindi icho maana nimechezea pesa nyingi sana kwa kunywa pombe na ngono nzembe maana nikinywa tu pombe tangu enzi za chuo lazima nitafute mwanamke wa kulala nae na kupelekea mara nyingi kuibuka na magonjwa kama UTI na gono nishawahi pata mara moja

Sasa tangu niingie mtaani na kuanza maisha ya utumishi wa umma imekuwa ni shida tena baada ya kwenda kufanya kazi wilaya fulani kwa wasambaa maana baada ya kwenda kule ndo ulevi ukazidi yaani nikiwa na hela tu akili inanipeleka kwenye pombe yaani mshahara wote unaishia kwenye pombe na ngono tena na malaya wanaojiuza na nikilewa sasa ni kama nakuwa nachanganyikiwa nachezea pesa balaa naweza jikuta nimetumia ata 100k kwa usiku mmoja,kingine ni kupoteza vitu yaani nishawahi kupoteza simu 3 ivi,na card ya benki,pia, nishaokotwa kalibu mara 2 nikiwa Bar nimezima sijitambui watu wananisaidia

Yaani pombe imenikataa kabisa na nimeshakuwa addicted nayo mbaya zaidi natumia izi pombe kali kama konyagi,kvant nk yaani kila nikijaribu kuacha naweza kuacha week 1 ila nikirudi inakuwa ndo toomuch

Nahitaji kuacha kwa sababu pombe inanifanya kuwa maskini na inaharibu afya yangu ,akili na uchumi wangu,mi ni mtumishi wa umma na nalipwa six figure salary kila mwezi ila ukinikuta navyoishi ni kama mtu wa ovyo yaani nazidiwa maisha ata na bodaboda maana hela zote zinaishia kwenye pombe na malaya badala ya kufanya maendeleo, pia nahitaji kuacha maana nakoelekea pia naweza jisababishia matatizo kama kurukwa na akili,magonjwa ,kifo na kuishi maisha ambayo nayachukia.

Na kuna muda hadi najuta kwenda iyo wilaya ya wasambaa kufanya kazi yangu ya kwanza maana ni kama nilirogwa vile maana kule ulevi uliopindukia ulianzia na kupoteza vitu kulianzia uko plus vitisho vya kurogwa mara kibao,imagine kila ukitaka kwenda job unasikia kizungu zungu .

naombeni msaada najitoaje kwenye ili janga maana nahitaji kuacha pombe ila ni kama kuna minyororo ya umasikini imenishika kila nikiwa na hela inanipeleka kwenye pombe na nakuwa sijitambui kabisa akili zinarudi nikishamaliza pesa na najuta sana ila nikipata hela tu akili ni kama inafungwa narudia yale yale na mbaya zaidi.
Hamia kwenye bia hakikisha unanunua kreti na unanywea nyumbani anza na Castle Lager 500ml au Safari Lager 500ml. Ukinywea nyumbani utabadilika maana ili uenjoy itabidi uanze kujipikia supu ama uchome nyama na uwe na fridge. Mwisho wa siku utaanza kunywa kistaarabu na utaizoea pombe utashangaa una bia 8 kwenye kreti haujazigusa mwezi wa pili. Mimi nilianza kufanya hivyo nilivyokuwa nyumbani lakini huku nchi za watu ndio utaratibu.
 
ushauri mzuri sana,Asiache kufunga na kusali🙏
POLE MKUU

Ni ngumu kuacha pombe ila ni rahisi kubadirisha mindset inayokutuma uifate ile pombe.

Hakika hakuna namna yoyote ile zaidi ya kushinda zimwi lenyewe ambalo ni wewe na wala sio pombe.

Kuna watu wengi wameacha pombe , sio kwamba wamepewa dawa wala nini ila waliamua kuishinda kiu kwa kuishinda fikra zao.

Waganga watakula hela zako
Wachungaji feki na mashehe ubwabwa watamaliza pesa zako.

🔥Meditate and pray , haswa mida ya 8 usiku hadi kumi alfajiri

🔥Cha kwanza acha kuona tulizo lako ni mitungi

🔥Badirisha mazingira ambayo yanakuchochea upige mitungi

🔥Achana na marafiki wanaokupa kampani hio

🔥Acha kuona kuwa umeshakuwa mtumwa wa ngono na hakuna namna yoyote unaweza fanya.

🔥 Kama hali ni mbaya mnoo tafuta Sober house ukae hata miezi 6

BILA KUFANYA HIVI TUTAKUZIKA MAPEMA
Mambo vipi ndugu zangu?

Leo nimekuja kwenu nipate ushauri maana napitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu kutokana na ulevi wa kupindukia, labda nianze tu kwa kuwapa historia fupi tu ya maisha yangu nilivyoanza kunywa pombe

Kunywa pombe nilianza 2016 nikiwa chuo kikuu na nilianza tu kwa ushawishi wa makundi mabaya na nilianza na pombe kali kwa iyo ilipelekea kuwa nakunywa pombe kali tu na nilikuwa naimudu fresh japo kuzingua ilikuwa mara moja na nimeendelea na pombe hadi leo hii na imeniletea shida nyingi kiuchumi na kiafya tangu kipindi icho maana nimechezea pesa nyingi sana kwa kunywa pombe na ngono nzembe maana nikinywa tu pombe tangu enzi za chuo lazima nitafute mwanamke wa kulala nae na kupelekea mara nyingi kuibuka na magonjwa kama UTI na gono nishawahi pata mara moja

Sasa tangu niingie mtaani na kuanza maisha ya utumishi wa umma imekuwa ni shida tena baada ya kwenda kufanya kazi wilaya fulani kwa wasambaa maana baada ya kwenda kule ndo ulevi ukazidi yaani nikiwa na hela tu akili inanipeleka kwenye pombe yaani mshahara wote unaishia kwenye pombe na ngono tena na malaya wanaojiuza na nikilewa sasa ni kama nakuwa nachanganyikiwa nachezea pesa balaa naweza jikuta nimetumia ata 100k kwa usiku mmoja,kingine ni kupoteza vitu yaani nishawahi kupoteza simu 3 ivi,na card ya benki,pia, nishaokotwa kalibu mara 2 nikiwa Bar nimezima sijitambui watu wananisaidia

Yaani pombe imenikataa kabisa na nimeshakuwa addicted nayo mbaya zaidi natumia izi pombe kali kama konyagi,kvant nk yaani kila nikijaribu kuacha naweza kuacha week 1 ila nikirudi inakuwa ndo toomuch

Nahitaji kuacha kwa sababu pombe inanifanya kuwa maskini na inaharibu afya yangu ,akili na uchumi wangu,mi ni mtumishi wa umma na nalipwa six figure salary kila mwezi ila ukinikuta navyoishi ni kama mtu wa ovyo yaani nazidiwa maisha ata na bodaboda maana hela zote zinaishia kwenye pombe na malaya badala ya kufanya maendeleo, pia nahitaji kuacha maana nakoelekea pia naweza jisababishia matatizo kama kurukwa na akili,magonjwa ,kifo na kuishi maisha ambayo nayachukia.

Na kuna muda hadi najuta kwenda iyo wilaya ya wasambaa kufanya kazi yangu ya kwanza maana ni kama nilirogwa vile maana kule ulevi uliopindukia ulianzia na kupoteza vitu kulianzia uko plus vitisho vya kurogwa mara kibao,imagine kila ukitaka kwenda job unasikia kizungu zungu .

naombeni msaada najitoaje kwenye ili janga maana nahitaji kuacha pombe ila ni kama kuna minyororo ya umasikini imenishika kila nikiwa na hela inanipeleka kwenye pombe na nakuwa sijitambui kabisa akili zinarudi nikishamaliza pesa na najuta sana ila nikipata hela tu akili ni kama inafungwa narudia yale yale na mbaya zaidi.
Funga sana na kusali,Mwombe Roho Mtakatifu,mlilie Yesu Kristo akuponye.Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma sana atakuponya...
Nilikuwa zaidi yako ila ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu..🙏
 
po

le

Asante kwa ushauri,kula uwa nakula mkuu tena ata nusu ya nyama ila nina ulevi uliopindukia yaani nimeshakuwa addicted kwa usiku mmoja naweza maliza ata 2 kvant ndogo ila nashindwa jizuia nikiongeza tu ni shida
K vant ndogo 2 😎😎😎

Mbona ndogo bro. min -me anashusha ile kubwa yenyewe na anakuwa byeee kabisa.

Anyway. inawezekana pombe kali hauzimudu.

Badili kinywaji.
Piga bia 5 au 6 then sepa home.

tena tafuta bar zenye wahudumu wabibi au inayohudumiwa na mmama mwenye heshima zake .
hata kama ni kiduka cha Mangi.

Na kwakuwa una manyege. the moment umeona ushaanza kumtaman huyo mbibi. bas unalipa unaenda kulala. (Hiki ndio kiwe kipimo cha Ulevi wako)
 
po

le

Asante kwa ushauri,kula uwa nakula mkuu tena ata nusu ya nyama ila nina ulevi uliopindukia yaani nimeshakuwa addicted kwa usiku mmoja naweza maliza ata 2 kvant ndogo ila nashindwa jizuia nikiongeza tu ni shida
Pombe imeharibu maisha ya watu wengi sana. Achana nayo mkuu
Ukiamua kuacha unaweza vizuri tu.
Jipe muda wa kugikiri kwamba je siku ukikutwa una matatizo ya INI AU FIGO utaendelea kunywa??? Jibu utakalo lipata ndiyo dawa ya kuacha
 
Usinywe siku za kazi mkuu.Kunywa weekend
 
Anza kusali kila siku kuanzia saa 6-9 usiku angalau hata kwa dakika 1 tu inatosha mbele za Mungu. Mlililie Mungu wako atakuponya na kukuvusha katika hilo jaribu.
Jitahidi pia kilasiku au angalau ×3 kwa wiki kwenda kanisani kuhudhuria ibada mbalimbali zilizopo, ukiona inafaa onana na kiongozi wa dini yako mshirikishe unahitaji maombi ya namna gani.
Epuka urafiki au ukaribu na watu wenye tabia za ulevi na uzinzi, najua itakuwa ngumu ila ukifanikiwa kujikaza kwa wiki au mwezi utakuwa umejinasua kiasi fulani.
Amini nakuambia ndani yako una kitu kikubwa ambacho shetani hataki kionekane mbele ya uso wa dunia, kwasababu sikuzote shetani hamuingizi mtu fala bwege ktk matatzo.
Huna pakukimbilia kupata msaada kwasasa zaidi ya kumrudia Mungu tu 🙏
Ushauri mzuri sana
 
Mambo vipi ndugu zangu?

Leo nimekuja kwenu nipate ushauri maana napitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu kutokana na ulevi wa kupindukia, labda nianze tu kwa kuwapa historia fupi tu ya maisha yangu nilivyoanza kunywa pombe

Kunywa pombe nilianza 2016 nikiwa chuo kikuu na nilianza tu kwa ushawishi wa makundi mabaya na nilianza na pombe kali kwa iyo ilipelekea kuwa nakunywa pombe kali tu na nilikuwa naimudu fresh japo kuzingua ilikuwa mara moja na nimeendelea na pombe hadi leo hii na imeniletea shida nyingi kiuchumi na kiafya tangu kipindi icho maana nimechezea pesa nyingi sana kwa kunywa pombe na ngono nzembe maana nikinywa tu pombe tangu enzi za chuo lazima nitafute mwanamke wa kulala nae na kupelekea mara nyingi kuibuka na magonjwa kama UTI na gono nishawahi pata mara moja

Sasa tangu niingie mtaani na kuanza maisha ya utumishi wa umma imekuwa ni shida tena baada ya kwenda kufanya kazi wilaya fulani kwa wasambaa maana baada ya kwenda kule ndo ulevi ukazidi yaani nikiwa na hela tu akili inanipeleka kwenye pombe yaani mshahara wote unaishia kwenye pombe na ngono tena na malaya wanaojiuza na nikilewa sasa ni kama nakuwa nachanganyikiwa nachezea pesa balaa naweza jikuta nimetumia ata 100k kwa usiku mmoja,kingine ni kupoteza vitu yaani nishawahi kupoteza simu 3 ivi,na card ya benki,pia, nishaokotwa kalibu mara 2 nikiwa Bar nimezima sijitambui watu wananisaidia

Yaani pombe imenikataa kabisa na nimeshakuwa addicted nayo mbaya zaidi natumia izi pombe kali kama konyagi,kvant nk yaani kila nikijaribu kuacha naweza kuacha week 1 ila nikirudi inakuwa ndo toomuch

Nahitaji kuacha kwa sababu pombe inanifanya kuwa maskini na inaharibu afya yangu ,akili na uchumi wangu,mi ni mtumishi wa umma na nalipwa six figure salary kila mwezi ila ukinikuta navyoishi ni kama mtu wa ovyo yaani nazidiwa maisha ata na bodaboda maana hela zote zinaishia kwenye pombe na malaya badala ya kufanya maendeleo, pia nahitaji kuacha maana nakoelekea pia naweza jisababishia matatizo kama kurukwa na akili,magonjwa ,kifo na kuishi maisha ambayo nayachukia.

Na kuna muda hadi najuta kwenda iyo wilaya ya wasambaa kufanya kazi yangu ya kwanza maana ni kama nilirogwa vile maana kule ulevi uliopindukia ulianzia na kupoteza vitu kulianzia uko plus vitisho vya kurogwa mara kibao,imagine kila ukitaka kwenda job unasikia kizungu zungu .

naombeni msaada najitoaje kwenye ili janga maana nahitaji kuacha pombe ila ni kama kuna minyororo ya umasikini imenishika kila nikiwa na hela inanipeleka kwenye pombe na nakuwa sijitambui kabisa akili zinarudi nikishamaliza pesa na najuta sana ila nikipata hela tu akili ni kama inafungwa narudia yale yale na mbaya zaidi.
🇺🇸Hongera kwanza kwa kulitambua tatizo

🇺🇸Walevi wengi Huwa hawakubali kuwa pombe ni tatizo

🇺🇸 Kuacha pombe hakuhitaji mtu kukushauri ni uamuzi wako binafsi tena wa gafla kuanzia " Sasa sinywi" wale wanaosema wataacha kwa kupunguza kidogokidogo kama wale mateja wa dawa za kulevya Huwa hawaachi

🇺🇸 Shukuru Mungu umegundua mapema unaweza kuwa figo zako zipo salama. Haya mapombe ya Sasa hivi yameua figo za vijana wengi na Sasa wanahudhuria dialysis na hakuna matibabu ya garama na ya kikatili kama hayo one session ni lakini 3 na ni almost ya kudumu
 
Back
Top Bottom