RoadLofa
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 1,856
- 4,084
Mambo vipi ndugu zangu?
Leo nimekuja kwenu nipate ushauri maana napitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu kutokana na ulevi wa kupindukia, labda nianze tu kwa kuwapa historia fupi tu ya maisha yangu nilivyoanza kunywa pombe
Kunywa pombe nilianza 2016 nikiwa chuo kikuu na nilianza tu kwa ushawishi wa makundi mabaya na nilianza na pombe kali kwa iyo ilipelekea kuwa nakunywa pombe kali tu na nilikuwa naimudu fresh japo kuzingua ilikuwa mara moja na nimeendelea na pombe hadi leo hii na imeniletea shida nyingi kiuchumi na kiafya tangu kipindi icho maana nimechezea pesa nyingi sana kwa kunywa pombe na ngono nzembe maana nikinywa tu pombe tangu enzi za chuo lazima nitafute mwanamke wa kulala nae na kupelekea mara nyingi kuibuka na magonjwa kama UTI na gono nishawahi pata mara moja
Sasa tangu niingie mtaani na kuanza maisha ya utumishi wa umma imekuwa ni shida tena baada ya kwenda kufanya kazi wilaya fulani kwa wasambaa maana baada ya kwenda kule ndo ulevi ukazidi yaani nikiwa na hela tu akili inanipeleka kwenye pombe yaani mshahara wote unaishia kwenye pombe na ngono tena na malaya wanaojiuza na nikilewa sasa ni kama nakuwa nachanganyikiwa nachezea pesa balaa naweza jikuta nimetumia ata 100k kwa usiku mmoja,kingine ni kupoteza vitu yaani nishawahi kupoteza simu 3 ivi,na card ya benki,pia, nishaokotwa kalibu mara 2 nikiwa Bar nimezima sijitambui watu wananisaidia
Yaani pombe imenikataa kabisa na nimeshakuwa addicted nayo mbaya zaidi natumia izi pombe kali kama konyagi,kvant nk yaani kila nikijaribu kuacha naweza kuacha week 1 ila nikirudi inakuwa ndo toomuch
Nahitaji kuacha kwa sababu pombe inanifanya kuwa maskini na inaharibu afya yangu, akili na uchumi wangu,mi ni mtumishi wa umma na nalipwa six figure salary kila mwezi ila ukinikuta navyoishi ni kama mtu wa ovyo yaani nazidiwa maisha ata na bodaboda maana hela zote zinaishia kwenye pombe na malaya badala ya kufanya maendeleo, pia nahitaji kuacha maana nakoelekea pia naweza jisababishia matatizo kama kurukwa na akili,magonjwa ,kifo na kuishi maisha ambayo nayachukia.
Na kuna muda hadi najuta kwenda iyo wilaya ya wasambaa kufanya kazi yangu ya kwanza maana ni kama nilirogwa vile maana kule ulevi uliopindukia ulianzia na kupoteza vitu kulianzia uko plus vitisho vya kurogwa mara kibao,imagine kila ukitaka kwenda job unasikia kizungu zungu .
Naombeni msaada najitoaje kwenye ili janga maana nahitaji kuacha pombe ila ni kama kuna minyororo ya umasikini imenishika kila nikiwa na hela inanipeleka kwenye pombe na nakuwa sijitambui kabisa akili zinarudi nikishamaliza pesa na najuta sana ila nikipata hela tu akili ni kama inafungwa narudia yale yale na mbaya zaidi.