Pombe inafilisi jamani

Pombe inafilisi jamani

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,413
Jamaa kapoteza mali zoote na akawa masikini wa kutupwa sababu ya ulevi, siku moja akapita karibu na jalala akaona chupa za bia. Akashika ya kwanza, akaipasua, kwa sababu yako nimeachana na mke wangu, akapasua ya pili: kwa sababu yako nimeshindwa kusomesha wanangu, akapasua ya tatu kwa hasira: kwa sababu yako nimefukuzwa kazi

akapasua ya nne: kwa sababu yako nimeuza mali zangu zote hadi nimefilisika. Akachukua ya tano akakuta haijafunguliwa imejaa bia akasema: we kaa pembeni, kwanza huu ugomvi haukuhusu tutaongea baadaye inaelekea huna tabia mbaya kama wenzako........

CHEZEA BIA WEWE?
 
Angekunywa viroba yasingemkuta...bei poa ulevi fasta usingizi murua, hangover ya kufaulu mtu...!
 
Kuna huyu alilala bwaksi.
Asubuhi alipoamka akamwambia mkewe -
"wife hii nyumba tuhame haraka"
Mke : "kunani tena?"
Mume : "Jana usiku kila nilipokwenda chooni nikifungua tu mlango taa ya chooni inajiwasha yenyewe! Nikitoka nikitaka kuzima inajizima yenyewe! Hii nyumba ina majini"
Muda si muda mke anaenda chukua maziwa kwenye fridge , ndy kukuta jagi la maziwa limejaa kojo! Kojo limezagaa frijini !
Kumbe bingwa alikua anakojoa jokofuni .
Lahauulaa !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom