Vitaimana
JF-Expert Member
- Nov 2, 2013
- 3,531
- 1,570
Pendekezo: Kianzishwe chama cha kutetea haki za walevi
CHAWATA kiitwe hivyo...
Pendekezo: Kianzishwe chama cha kutetea haki za walevi
RAHA NA KARAHA BIA YA SITA!
Kwa wanywaji wazuri wa bia, chupa ya kwanza huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo. Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
Baada ya kumaliza chupa ya pili kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi.
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wagonjwa wa Ebola waliopona katika nchi ya Liberia. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza.
Bia ya nne huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia, bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu, na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa au Mume wangu sijui yukoje hanijali
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo ---- na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika.
Kweli kabisaVikao hivi vina faida nyie acheni tu. Huku utaelekezwa shule nzuri kumpeleka mwanao, jambo la kufanya kama una kesi mahakamani, fundi ujenzi mzuri na hata mahali pa kupata kiwanja kwa bei poa. Afu kwa ujumla unaburudika...
dah!! "kuzima" raha
faida zake ni [1] umaskini [2] figo maini kwisha [3] na mwisho mauti,,,:hatari:,,​
Asilimia kubwa ya walevi baada ya pombe kuisha kichwani,hujuta na kusema sinywi tena na leo ndiyo mwisho.
View attachment 247886View attachment 247886beautiful as it is
dah!! "kuzima" raha
Mpe maskini pombe anywe alewe asahau/aahirishe matatizo yake
Jamani kwa wale walevi hivi mkinywa pombe mnapata faida gani? Kuna pombe kama GONGO,BIA,WHISKY,KONYAGI. VIROBA nk. hivi mkinywa hizi pombe zaidi ya kupoteza pesa,kulala nje ya nyumba, kutopeleka matumizi nyumbani, ni faida gani ambayo anaipata mlevi?
Wale wataalam wa hii fani waje watujuze
hivi tajiri hanywi pombe :what: